Walimu kugoma Oktoba mosi

Walimu kugoma Oktoba mosi

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
• Wanaidai serikali sh bilioni sita

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa mwezi mmoja kwa serikali kulipa malimbikizo yao ya madeni ya walimu yanayofikia bilioni 33.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, rais wa chama hicho, Greisoni Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.

‘Tumetoa mwezi huu wa tisa uwe wa mwisho kuililia serikali, baada ya hapo tutaamua hatua gani tufanye, maana tumekutana na makatibu wakuu wa wizara zinazowahudumia walimu lakini bado tunaishia kupewa ahadi hewa,” alisema Mukoba.

Mukoba aliongeza kuwa Agosti 14, mwaka huu, walikutana na makatibu wakuu wanaowahudumia walimu pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma, wakatakiwa kuwasilisha madai yao yote.

“Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho, tuliwafahamisha kuwa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 33 na mwisho wa kikao hicho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili,” aliongeza Mukoba.

Mukoba alisema wiki mbili zilipofika, walienda kuonana tena na Katibu Mkuu, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuwasilisha vitabu vyenye madai mbalimbali ya walimu.

“Madai hayo tuliyaambatanisha kwenye barua Na CWT/004/UTMS/VOL.11/94 na madai hayo sasa yamefikia sh bilioni sita,” alisema Mukoba.

Mukoba aliishangaa serikali kuanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now”, huko walimu ambao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo, wana maisha magumu kutokana na mishahara kuwa midogo na kuzidi kwa malikimbizo ya madeni yao.

“Walimu ambao ndiyo watelekezaji wakuu wa mpango huu japo hawaelewi au hawajapewa semina elekezi, lakini ndio watekelezaji wakubwa.

Naishangaa serikali kuwadharau walimu na nakuhakikishia mpango huo hautafanikiwa kama walimu hawapati haki zao,” alisema Mukoba.

Mukoba aliionya serikali ikamilishe madai ya walimu ili wafanye kazi kwa moyo tofauti na sasa ambapo wengi wamekata tamaa.

‘‘Walimu wa nchi hii wamekata tamaa. Mioyo yao imekufa ganzi kwa sababu serikali imekataa kuwalipa malimbizo yao.

Kwanini serikali imeamua kuwatendea jeuri walimu kiasi hiki?” alihoji Mukoba.
 
hawa watu wanaigiza na sijui lini watakamilisha filamu yao
ilio jaa unafiki , uliokosa mshikamano na umoja, uliojaa undumilakuwili
ni hivi ''charity begins at home'' kama kweli Walimu wamedhamiria waanze
na CWT ndio adui wao mkubwa serikali inafuata vinginevyo mnaigiza huu ni
ushauri tu.
 
Ushauri wako ni sawa na nguvu za giza. Au umetumwa na serikali?
 
Hiki chama nacho ni janga la kitaifa. Kila siku tunatoa mwezi mmoja lakini mwisho wa siku hawafanyi chochote. Mbona wafanyakazi wa TAZARA waligoma na matokeo tumeyaona.

Waalimu hasa wa shule za msingi hawawezi kugoma kwa sababu:

1. Chama cha waalimu kina mamluki wengi. Wengi wao hujitajirisha kwa fedha za michango ya waalimu. Mipango mingi ya migomo huishia hewani kwa sababu viongozi wa chama baada ya siyo sehemu ya waalimu na hivyo adha ya waalimu haiwahusu.

2. Baadhi ya madai ya waalimu ni ya kughushi hasa baada ya kushirikiana na watendaji wa Halmashauri. hivyo, ukifika muda wa kugoma kikweli kweli hujichomoa kwa sababu wanajua kuwa madai yao siyo ya haki.

3. Waalimu wakuu hawapo pamoja na waalimu wengine kwa sababu wao hupewa nafasi hizo na viongozi wa juu wa Halmashauri na wanapata nafasi hizo bila kustahili. Hao nao hutumia vibaya fedha za matumizi ya kawaida inayoitwa "capitation". hawawezi kuingia kwenye migomo kwa sababu watapoteza nafasi zao.

4. Waalimu wengi ni wale ambao wamefeli na hatimaye baadhi wametumia vyeti vya wenzao au vya kufoji. Kwa sababu baadhi yao mambo yao yanafahamika hawawezi kufurukuta kwani kufanya hivyo ni kujihatarishia maisha.

5. Waalimu wana tatizo kubwa la kuwa na uwezekano mdogo wa kubadilisha fani/aina ya kazi labda awe ameenda kusomea fani nyingine. Mwalimu anachoogopa ni kuwa akifukuzwa kazi atakwenda kufanya nini? Ndiyo maana huwezi kusikia Wahandisi wamegoma kwa sababu wengi wao kwanza wana uwezo wa kujitafutia kazi zingine na ndiyo maana hawahangaiki kuomba kazi kwa Mkurugenzi wa Wilaya.

Ushauri wangu kwa waalimu ni kuwa kama kugoma kumeshindikana basi mjitoe kuchangia hicho chama kwa kuandika notisi ya mwezi moja kwa mwajiri kumtaarifu kuwa unasitisha michango yako katika chama. Hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya kazi ya mwaka 2004(ibara nimeisahau) - kama ibara hiyo haijafutwa.

Ninachojua ni kuwa wengi wenu mnakatwa michango bila ridhaa yenu wakati makato hayo siyo ya lazima. makato ya lazima katika mshahara wa mtumishi kwa mujibu wa sheria ya kazi ya mwaka 2004 ni kwa ajili ya kodi na mfuko wa hifadhi ya jamii. Makato mengine kama ya chama cha wafanyakazi, mwenge na ziara ya rais ni wizi kwa sababu ya unyonge wenu.

Waalimu mnapoteza fedha zenu kidogo kwa kukichangia chama ambacho kinageuka kuwa balaa kwenu. Chama cha waalimu kina fedha nyingi ndiyo maana wanafikiria kuanzisha benki kitu ambacho siyo lengo la vyama vya wafanyakazi. Mnaidai serikali iongeze mishahara kwa sababu ni midogo lakini hamkumbuki kuwa mnpoteza mishahara yenu kwa anjili ya kuchangia chama ambacho hakina tija.
 
hawa watu wanaigiza na sijui lini watakamilisha filamu yao
ilio jaa unafiki , uliokosa mshikamano na umoja, uliojaa undumilakuwili
ni hivi ''charity begins at home'' kama kweli Walimu wamedhamiria waanze
na CWT ndio adui wao mkubwa serikali inafuata vinginevyo mnaigiza huu ni
ushauri tu.

Afadhali hawa wanabweka, kuna mamillion ya wafanyakazi kwenye sekta mbalimbali nchi hii, japo wanalipwa mishahara yao kwa wakati lakini wanafanya kazi kama watumwa wa karne ya kumi saba na hawafikirii japo kubweka kama hawa.
 
hawa walimu ni kama wale wazee wastaafu wa East Africa - hakuna mgomo mule.
 
chini ya mkoba haitatokea wakamilishe mission ya kugoma
 
Wanajamvi

Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kimetoa mwezi 1 serikali kulipa malimbikizo yao ya madeni yanayofikia bilioni 33.

"Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho,tuliwafahamisha kuwa walimu wanadai serikali zaidi ya biln 33 na mwisho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili"

Rais wa Chama hicho G. Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.
source. Jana akizungumza na waandishi wa habari jijini
 
Akaanza hivyo ujue ndiyo anania ya kuwapotezea waalimu. hakuna mgomo wowote wa wazi ambao waalimu wataweza kuufanya. Mgomo wa siri siri tu ndiyo wamefanikiwa kwani tayari tumeshayaona katika matokeo ya mitihani.
 
• Wanaidai serikali sh bilioni sita

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa mwezi mmoja kwa serikali kulipa malimbikizo yao ya madeni ya walimu yanayofikia bilioni 33.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, rais wa chama hicho, Greisoni Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.

‘Tumetoa mwezi huu wa tisa uwe wa mwisho kuililia serikali, baada ya hapo tutaamua hatua gani tufanye, maana tumekutana na makatibu wakuu wa wizara zinazowahudumia walimu lakini bado tunaishia kupewa ahadi hewa,” alisema Mukoba.

Mukoba aliongeza kuwa Agosti 14, mwaka huu, walikutana na makatibu wakuu wanaowahudumia walimu pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma, wakatakiwa kuwasilisha madai yao yote.

“Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho, tuliwafahamisha kuwa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 33 na mwisho wa kikao hicho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili,” aliongeza Mukoba.

Mukoba alisema wiki mbili zilipofika, walienda kuonana tena na Katibu Mkuu, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuwasilisha vitabu vyenye madai mbalimbali ya walimu.

“Madai hayo tuliyaambatanisha kwenye barua Na CWT/004/UTMS/VOL.11/94 na madai hayo sasa yamefikia sh bilioni sita,” alisema Mukoba.

Mukoba aliishangaa serikali kuanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now”, huko walimu ambao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo, wana maisha magumu kutokana na mishahara kuwa midogo na kuzidi kwa malikimbizo ya madeni yao.

“Walimu ambao ndiyo watelekezaji wakuu wa mpango huu japo hawaelewi au hawajapewa semina elekezi, lakini ndio watekelezaji wakubwa.

Naishangaa serikali kuwadharau walimu na nakuhakikishia mpango huo hautafanikiwa kama walimu hawapati haki zao,” alisema Mukoba.

Mukoba aliionya serikali ikamilishe madai ya walimu ili wafanye kazi kwa moyo tofauti na sasa ambapo wengi wamekata tamaa.

‘‘Walimu wa nchi hii wamekata tamaa. Mioyo yao imekufa ganzi kwa sababu serikali imekataa kuwalipa malimbizo yao.

Kwanini serikali imeamua kuwatendea jeuri walimu kiasi hiki?” alihoji Mukoba.

Nyie CWT Mikwala tu mnajifanya mnawatetea walimu hali ikiwa tete nyie mnarudi nyuma, Siwaamin kwa lolote msemalo. MKOBA umesahau yaliyomkuta Dr Ulimboka?
 
Ninachojua ni kuwa walimu wapo kwenye mgomo kazini siku nyingi, huu wa sasa labda wanapanga kugoma kwenda kazini.
 
Walimu wanapiga kazi vizur Mukoba na Cwt yako hebu sepa huko. Kwanza hiki chama inabidi kifutwe haraka sana....
 
Si kwamba walimu watagoma wanakumbushana kujiandaa kwa matokeo mabaya kwa drs la 7 na matokeo mabaya zaidi ya kidto cha 4 hapo mwakani 2iombe tu serikali ijiandae kisaikolojia kuingia darasani kuliseat kwa mara nyingine.
 
Back
Top Bottom