Walimu 251,000 wa Shule za Msingi kuhitajika mwaka 2025

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
wanafunzi.jpg

TAKRIBAN walimu 251,000 waliofuzu watahitajika kukidhi mahitaji ya shule za msingi nchini Tanzania ifikapo mwaka 2025 kutoka walimu 135,000 waliokuwepo tangu mwaka 2005, FikraPevu inaandika.

Hali hiyo inafuatia kasi ya ongezeko la idadi ya watu nchini licha ya ukuaji mdogo wa uchumi usioendana na kasi hiyo.

Ripoti ya ‘Tanzania: Idadi ya Watu, Afya ya Uzazi na Maendeleo’ ya mwaka 2006 inaeleza kwamba, walimu wa kutosha waliofuzu watahitajika ili kuendeleza mabadiliko ya kielimu na upanuzi.

Inaelezwa kwamba, mwaka 2005, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilieleza kwamba kulikuwa na uwiano wa wanafunzi 56 kwa kila mwalimu, lakini kwa sasa uwiano wa wanafunzi na mwalimu katika shule za msingi umepanda baada ya muda kutokana na ongezeko la uandikishaji baada ya mwaka 2000.

Soma zaidi hapa => Walimu 251,000 wa Shule za Msingi kuhitajika mwaka 2025 | Fikra Pevu
 
Back
Top Bottom