Walevi wa saa za kazi wasionewe haya

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
WILAYA ya Nzega mkoani Tabora imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais John Magufuli la kuzuia unywaji wa pombe saa za kazi, kwa kuwatia mbaroni watu 25 wanaodaiwa kukutwa wakiutumia muda huo kwa kunywa pombe.

Tukio la Nzega limethibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nzega, Juma Majura aliyesema ametii agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Jacqueline Liana la kuhakikisha wananchi wanautumia muda wa kazi kwa kufanya kazi za uzalishaji mali na si kulewa au kujihusisha na shughuli zisizo na tija kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Alisema ukamataji huo umehusisha vilabu vya pombe za kienyeji aina ya Komoni zinazotengenezwa kwa kutumia mahindi, huku akisisitiza wengi wa waliokamatwa ni wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Liana alikiri kutoa agizo, huku akisema ugomvi wake na watu hao ni kunywa pombe saa za kazi, akisisitiza wanaweza kufanya hivyo baada ya muda wa kazi, lakini mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali katika eneo lake.

Hakika, hiyo ndiyo nia njema ya Serikali ya Rais Magufuli, ya kumtaka kila mmoja ashiriki katika kuinua uchumi wa nchi. Ndiyo maana, kwa utekelezaji wa agizo hilo, tunachukua fursa hii kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Nzega kwa juhudi za kuhakikisha watu katika wilaya yake wanazama katika kufanya kazi, badala ya kuzama katika mitungi ya pombe za kienyeji inayowadhoofisha kiakili, kimwili na hata kiuchumi.

Agizo hilo la Rais Magufuli wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa Machi mwaka huu, lililenga kuwafanya Watanzania kuishi kwa kipato halali, badala ya njia za ujanjaujanja, ikiwa ni pamoja na kujinufaisha kwa fedha na rasilimali za umma. Ni njia ya kumfanya kila Mtanzania aifanyie kitu nchi yake, badala ya kusubiri nchi imfanyie kitu.

Kwamba, wana wajibu wa kufanya kabla ya kuanza kuilalamikia serikali kuwa haitimizi majukumu yake. Ndiyo maana Rais Magufuli akasisitiza watu lazima wafanye kazi, badala ya kukaa vijiweni na kwamba watakaokamatwa wakinywa pombe, au wale wanaocheza michezo ikiwemo ya Pool nyakati za kazi, wakamatwe na wawekwe ndani hata kwa saa mbili ili kuleta nidhamu ya uwajibikaji.

Tunadhani wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wa kuufanya katika kumsaidia Rais Magufuli kuwarudisha watu katika nidhamu ya kufanya kazi. Hebu tujiulize, kuna ugumu gani wa kijana mwenye nguvu aamke asubuhi na kuishia kucheza Pool wakati wazazi wake wakihenyeka shambani?

Ukiwauliza, majibu yao ni mapesi, eti hakuna kazi. Lazima tuachane na dhana hii kwani uwezo wa serikali wa kuajiri raia wake katika utumishi wa umma hauzidi asilimia tano ya Watanzania wote, hivyo wengine wana uwanja mpana wa kujikita katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, badala ya kuutumia muda mwingi kufanya porojo, kunywa pombe na kucheza pool.

Kama kila kijana ambaye ni nguvu kazi ya taifa akiamua kubaki kucheza Pool au kwenye starehe na ulevi muda wote, nani atainua uchumi wa nchi hii? Katika hili la uwajibikaji, hakika kila mmoja akitimiza wajibu wake, Taifa la Tanzania litasonga mbele kwa kasi na hivyo kutimiza ndoto na dhamira ya Rais Magufuli ya kuiona nchi ikiachana na utegemezi. Ifike mahali falsafa ya `Hapa Kazi Tu’ isiishie hewani, bali tuitimize kwa pamoja ili kuyafikia malengo yetu ya uchumi wa kati
 
hao watu uliwapa kazi wakakataa kufanya? Kama hawana kazi wafanyeje?
 
Back
Top Bottom