singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
MCHAKATO wa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar unaendelea huku kukiwa na taarifa ya kuwepo viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani, pamoja na matukio ya makusudi yenye lengo la kuogofya wananchi ili wasishiriki kupiga kura za marudio muda utakapowadia.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ilikwishatangaza tarehe rasmi ya kurudiwa kwa uchaguzi wa Rais na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi, kutokana na kufutwa ule wa Oktoba 25, mwaka jana. Uchaguzi huo ulielezwa kufutwa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kuwepo kwa kasoro kwenye mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa ZEC, wananchi wa Zanzibar sasa watapiga kura Machi 20, mwaka huu kuchagua viongozi hao. Chama cha Wananchi (CUF) tayari kimekwishatangaza kutoshiriki ambapo Katibu wake Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad aliijulisha Tume hiyo ya Uchaguzi ya Zanzibar kuwa amejiondoa katika kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hatua iliyowafanya wanachama wa chama hicho nao kukataa kushiriki.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa tayari kuna vuguvugu lisilo jema visiwani humo kutokana na baadhi ya watu wasio na mapenzi mema na visiwa hivyo kutisha wenzao wanaoonekana kukubali kurudiwa kwa uchaguzi huo na kuthibitisha kushiriki.
Jambo hilo halikubaliki na linapaswa kudhibitiwa mapema na vyombo vya usalama vinavyohusika, ili uchaguzi huo wa marudio ufanyike kwa utulivu na amani. Hadi juzi vyama sita vya siasa vilikwishaithibitishia ZEC kuwa vitashiriki uchaguzi huo. Vilieleza sababu za kufanya hivyo kuwa ni pamoja na kutekeleza kwa vitendo haki ya kidemokrasia ya kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza Zanzibar.
Vyama hivyo ni SAU, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Kijamii (CCK),Tanzania Labour (TLP), TADEA na Chama cha Wakulima (AFP). Katika maelezo yake yaliyonukuliwa na gazeti hili jana, Mgombea urais wa AFP kwenye uchaguzi huo, Said Soud alieleza juu ya kuzuka kwa hofu miongoni mwa wananchi kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani hasa katika kisiwa cha Pemba.
Kwa mujibu wa Soud, kuna watu wameanza kuwatisha wafuasi wa vyama vilivyothibitisha kushiriki uchaguzi huo, ili wasipige kura kwa kuweka alama ya X kwenye nyumba zao na kuwasambazia vipeperushi vyenye ujumbe unaoonesha kuwepo kwa nia ya kuvunja amani wakati wa uchaguzi huo.
Kutokana na maelezo yake, baadhi ya watu kisiwani Pemba wana msukumo wa kufanya vurugu kutokana na imani waliyojijengea kuwa uchaguzi visiwani humo hauwezi kufanyika bila CUF kushiriki, jambo analosema kuwa si la kweli.
Kutokana na hofu hiyo, mgombea huyo alisema kuwa aliamua kumuomba Rais John Magufuli kusaidia kuimarisha ulinzi katika eneo hilo kwa sababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, ili wenye kutaka kuuvuruga uchaguzi huo wasipate nafasi, kwa kuwa ndio njia pekee ya kidemokrasia inayoweza kuipa Zanzibar viongozi halali. Shime Watanzania wenzetu wa Zanzibar, msiruhusu uvunjifu wa amani