Wale tunaowaficha wake zetu mipango yetu tukutane hapa

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Kwenye maisha ya ndoa unatakiwa uwe na akili sana na kufanya maamuzi sometimes magumu ili maisha yaendelee. Kuna wanaoamua kufuata mfumo dume kutokana na aina ya wake zao, wengine mfumo shirikishi umewasaidia wafike mbali kimafanikio. Leo tushirikishane wale walioamua kufuata mfumo dume. Je, kitu gani kiliwafanya kufikia hatua hiyo?

Back in 2014 nilihamishiwa mkoa flani kikazi baada ya kufika jambo la kwanza nilinunua kiwanja sq meter 924. Kumshirikisha mke wangu akakakataa kabisa tusijenge kisa kipo porini sana, nikajaribu kumuelewesha kuwa ndio mji unakoelekea pia ni kwa kimepimwa so ni security tosha hakiwezi kuvamiwa wala kusogeza mpaka.

Wife alitia ngumu sana hakutaka kushiriki hata hela aliyoniahidi atatoa kwenye biashara zake niongezee kwenye ujenzi akagoma. Akaja na hoja bora tujenge Dar aisee nikafikiria Dar sina ndugu wa kumuamini nimtumie hela asimamie ujenzi nikaona ujinga NIKAPIGA CHINI.

Nikaamua kijenga bila kumshirikisha chochote mpaka 2018 namaliza ujenzi by the time umeme umefika maji yapo na barabara zimeboreshwa. Nimempeleka site nyumba imekamilika anahamaki kuwa kumbe maeneo yalikuwa mazuri na mji umetanuka "ananisifia nina akili sana" kumbe alininyima support. Ningefuata ushauri wake mpaka sasa sina nyumba na familia imeongezeka.
 
Hapo ulimshirikisha,ila ulitumia busara kama msemo usemao akili za kuambiwa changanya na za kwako,!
Kila kitu kina sababu mkuu...ukiona baba yako anaenda tofauti na maza ujue sio bahati mbaya. Ndio nilichofanya mimi baada ya kuona hakuna mwelekeo nikimshirikisha nikaamua kuaply mfumo dume
 
Baba yetu ana hiyo principle toka nazaliwa....bahati mbaya sijui inakuaje ..akianza biashara bila kumshirikisha mama inakufa ndani ya muda mfupi...kwahyo endeleeni tu na tabia zenu mbaya!

Hata sisi hatuwashirikishi kwenye projects zetu kwahiyo bila bila
 
Umepata nguvu sababu matokeo yamekuwa chanya. Shida ni ukatae ushauri wa mwenzio halafu matokeo yawe hasi.
Mkui mm ni mwajiriwa nahamishwa muda wowote hataki tujenge kwenye kiwanja surveyd kisa hapajaendelea.. wakati ukinunua kiwanja hakijapimwa ukiondoka tuu migogoro kibao
 
Umefanya safi kumwambia kama una kiwanja ila usithubutu kuficha kama una mali nje yeyote maana ukikata kamba ghafla unawafaidisha madalali(matapeli) watauza tu.
Nilimshirikisha kua nimenunua kiwanja kukiona hataki tujenge hapo so nikaamua kujenga baada ya kujenga nikampeleka akashangaa pamechangamka na kuna kila huduma akanipongeza je ningekubali tusijenge hapo familia imeongezeka ingekua je?
 
Safi ni vyema ulivyomwambia kama una mali nje.
 
Baba yetu ana hiyo principle toka nazaliwa....bahati mbaya sijui inakuaje ..akianza biashara bila kumshirikisha mama inakufa ndani ya muda mfupi...kwahyo endeleeni tu na tabia zenu mbaya!

Hata sisi hatuwashirikishi kwenye projects zetu kwahiyo bila bila
Hakuna kitu hapo. Na kuna wanaaake ukiwashirikisha wanakua positive wengine bila facts wanakwamisha... kuna wengine wakiona unataka kufanya kitu wanajua una hela wanaanza kuleta mahitaji yasiyo na msingi
 
Kwenye maisha ya ndoa unatakiwa uwe na akili sana na kufanya maamuzi sometimes magumu ili maisha yaendelee. Kuna wanaoamua kufuata mfumo dume kutokana na aina ya wake zao, wengine mfumo shirikishi umewasaidia wafike mbali kimafanikio. Leo tushirikishane wale walioamua kufuata mfumo dume. Je, kitu gani kiliwafanya kufikia hatua hiyo?

Back in 2014 nilihamishiwa mkoa flani kikazi baada ya kufika jambo la kwanza nilinunua kiwanja sq meter 924. Kumshirikisha mke wangu akakakataa kabisa tusijenge kisa kipo porini sana, nikajaribu kumuelewesha kuwa ndio mji unakoelekea pia ni kwa kimepimwa so ni security tosha hakiwezi kuvamiwa wala kusogeza mpaka.

Wife alitia ngumu sana hakutaka kushiriki hata hela aliyoniahidi atatoa kwenye biashara zake niongezee kwenye ujenzi akagoma. Akaja na hoja bora tujenge Dar aisee nikafikiria Dar sina ndugu wa kumuamini nimtumie hela asimamie ujenzi nikaona ujinga NIKAPIGA CHINI.

Nikaamua kijenga bila kumshirikisha chochote mpaka 2018 namaliza ujenzi by the time umeme umefika maji yapo na barabara zimeboreshwa. Nimempeleka site nyumba imekamilika anahamaki kuwa kumbe maeneo yalikuwa mazuri na mji umetanuka "ananisifia nina akili sana" kumbe alininyima support. Ningefuata ushauri wake mpaka sasa sina nyumba na familia imeongezeka.
aiseee
 
Hakuna kitu hapo. Na kuna wanaaake ukiwashirikisha wanakua positive wengine bila facts wanakwamisha... kuna wengine wakiona unataka kufanya kitu wanajua una hela wanaanza kuleta mahitaji yasiyo na msingi
Shida iko hapo tu...mnakuwa hamna vission moja..anywys ndo maisha lakini
 
Back
Top Bottom