Wale tulikua na magari na sasa hatuna tunatumia daladala tukutane hapa

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Habari wakuu

Kwa wale ambao mlikua mnamiliki vyombo vya usafiri na sasa hamna kwa namna moja au nyingine mkajikuta tu gari umeuza, imepata ajari na kuharibika kabisa

hivi mnaweza vipi kuendana na hali hii ya kuanza kutumia usafiri wa daladala za hapa jijini Dar es salaam?

Kiukweli hapa nipo na wakati mgumu hasa baada ya hiki kivits changu kupata ajari na kukongoroka kabisa huku nikiwa sina pesa ya kununua gari jingine

hali hii imenifanya nirudi kwenye kugombea daladala yaani ni full tafrani, muda wa wiki moja tu nimechoka, naona fedhea na aibu nahisi watu na majirani wananisema nimefulia

Hivi hali hii huwa mnaikabili vipi watu wa humu?
kesho kazini muda unaenda nazidi kupata mawazo ya usafiri tu hapa
 
Vumilia utazowea tu!

Halafu maisha yako usitizame wanadamu watasema nini, kikubwa haumdhuru MTU, ridhika na hali yako ya sasa huku ukipambania yajayo.

Endelea kukomaa na ujikubali bila kukata tamaa, maisha kuna hali mbalimbali zakupasa ukabiliane nazo kwa shukrani na sio manung'uniko.

Afya yako mtaji mkubwa kwako, aliekupa ridhiki bado you hai utaipata tena kikubwa subira.
 
Ni mda sahihi wa mapumziko ya suti...
Ni mda sahihi wa kuishi bila pressure...
Ni mda sahihi wa kupata changamoto mpya....
Ni mda sahihi wa kujipanga vizuri.......
Ni mda sahihi wa kujua na kutafakari makosa yako....
Ni mda sahihi wa kukabiliana na changamoto mpyaa.....
Ni mda sahihi wa kutafta hela ya kudumu...
Ni mda sahihi wa kujifunza upande B....
Ni mda sahihi wa kushusha/kupunguza mahitaji.....
Ni mda sahihi wa kuongeza interaction na watu....
Ni mda sahihi wa kuwajua wanafiki wako...
Ni mda sahihi wa mawazo, mipango na akili kutanuka....
Ni mda sahihi wa kukubali na kuyaishi mabadiliko....
Ni mda sahihi wa afya ya akili na mwili wako.....
 
Kwa bongo na mafoleni yote hayo na joto pesa yote inaishia barabarani,kama daladala inakuzingua kwa bongo kuna usafiri wa kushare BAJAJI huo utakusaidia.
 
Habari wakuu

Kwa wale ambao mlikua mnamiliki vyombo vya usafiri na sasa hamna kwa namna moja au nyingine mkajikuta tu gari umeuza, imepata ajari na kuharibika kabisa

hivi mnaweza vipi kuendana na hali hii ya kuanza kutumia usafiri wa daladala za hapa jijini Dar es salaam?

Kiukweli hapa nipo na wakati mgumu hasa baada ya hiki kivits changu kupata ajari na kukongoroka kabisa huku nikiwa sina pesa ya kununua gari jingine

hali hii imenifanya nirudi kwenye kugombea daladala yaani ni full tafrani, muda wa wiki moja tu nimechoka, naona fedhea na aibu nahisi watu na majirani wananisema nimefulia

Hivi hali hii huwa mnaikabili vipi watu wa humu?
kesho kazini muda unaenda nazidi kupata mawazo ya usafiri tu hapa
Mimi huwa majrani ndg na marafiki huwa nawaweka njia panda tough to forecast me, huwa naweza park gari week 1 au 2 napanda daladala, then narudia kwenye kapaso....(mixed lifestyles)
 
Back
Top Bottom