Habarini za Jioni Ndugu wana JF.
Kwa pamoja wote tunao litakia mema taifa letu tuungane kukataa vurugu zisizo na tija kwa maslahi ya wachache wanaotumiwa kuliharibu taifa letu tulilolirithi kutoka kwa Babu zetu. Kupigana, kuvurugana, kutukanana na kutoheshimiana si utamaduni wa watanzania na wala si utanzania.
Haishangazi kuona vinara wa kuhamasishwa vurugu hizi ni watu ambao tayari wamekana uraia wa Tanzania kwani watu hawa hawana uzalendo na taifa ili.
Binafsi nasikitishwa sana na tabia zisizo na utu za wachochezi wa vurugu hizi kwani wamekuwa wakishawishi watu wafanye vurugu kwa mlengwa wa kudai haki, hii si sawa.
Watu hawa hawana uchungu hata kidogo na damu za watanzania na wamezamiria kutushawishi ili tuuwane sisi watanzania tunaoishi huku ili wao waendelee kuingiziwa commission na mabeberu.
Kwanza inashangaza kuona watu hawa wananadi sera za kimagharibi juu ya Afrika kwa minajili ya haki za kibinadamu, Tujiulize hawa wazungu tunao waita wasimamizi wa haki za kibinadamu kwetu TZ je wanatupenda?
Wanafurahi kutuona tunakuwa wamoja au tukigawanyika? Ni lini wazungu wametutendea haki sisi waafrika? Mara ngapi ndugu zetu weusi wanauawawa na polisi wa mabeberu tena kikatili kwa kigezo cha uafrika wao?.
Kimsingi tukubali Kuna wenzetu wachache wametugeuka na kuamua kuwa vibaraka wa wazungu Ili kushirikiana na Wazungu kutuangamiza.
Ni vyema Vijana wa kitanzania tumetambua mapema hila na njama zao zisizo na tija juu ya taifa letu na tuwaambie bila kuwaficha hawa wachochezi kuwa taifa Ili ni bora kuliko hivyo visenti wanavyopewa na hao wazungu. Mungu atawalaani kwa ujila wao wanaoupata Ili kulisaliti taifa letu.
Mabeberu wanatamani tuvurugane Ili waje wachukue Mali zetu kama wanavyofanya mataifa mengine kama Congo n.k , Tukumbuke njama hizo pia zilitumika kumuondoa Shujaa wa Africa Muamar Gadaffi pale Libya na sasa wanataka kutumia njama hizo kila Nchi ya Afrika yenye Mali.
Sasa tuwafikishie Ujumbe kuwa Tanzania haitakubali njama zao na tunakataa kugawanywa kwa mlengwa wa kisiasa au udini, Tunakataa kuuwana wenyewe kwa wenyewe, Tunakataa Maisha ya shida na taabu wanayotaka tuishi kwani wanatamani tukose chakula na tutaabike kwa njaa Ili wake kwa minajili ya kutusaidia kumbe wanabeba Mali zetu kama wanavyofanya Congo n.k
Tunakataa uhuni wao na njama za hila zisizo na mlengwa chanya kwa Nchi yetu.
Cha mwisho niwakumbushe watanzania wanaorubuniwa na mabeberu kushawishi vurugu hizi kuwa nafasi ya kutubu bado ipo wakatubu dhambi hii ya kushawishi watanzania wafanye vurugu ilihali wanajua kitawachowakuta ndiyo maana wao hawakushiriki.
Tanzania ni Yetu Sote, Kwa Pamoja tujenge Nchi yetu. Tanzania Kwanza, Mengine baadae.