Wakuu wa Wilaya ni vyema wakapitia Ukurugenzi

dyeanka

Member
Jun 19, 2016
96
70
Ndugu wana Jf salaam,
Kwanza nianze kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwateua wakuu wa wilaya ambao kwa kweli kwa sehemu kubwa ni vijana na sio vijana tu pia wasomi. Nimaniyangu kwamba watamuakilisha Rais ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao.

Pamoja na pongezi hizi kwa mh. Rais lakini ningependa kutoa mapendekezo yangu katika swala zima la uteuzi wa wakuu wa wilaya ingekuwa vyema sana kama wakuu wa wilaya wangekuwa wamepitia kwenye ukurugenzi ilikusudi kuwe na usimamizi madhubuti katika miradi ya maendeleo. Nasema haya kutokana na wakurugenzi wengi huwa wanawadanganya wakuu wa wilaya bila hata kugundua kama wqnadanganywa na wakurugenzi.

Katika kuthibitisha haya tufanye tathimini ya wakurugenzi 22 walio pewa ukuu wa wilaya kwenye wilaya tofautitofauti watakavyo tekeleza majukumu yao vyema.

Wito kwa mamlaka za uteuzi wakizingatia haya wakati wa uteuzi kutakua na usimamizi mzuri shughuli za serikali pamoja na miradi ya maendeleo lakini pia wanaweza kwenda na kasi mh. Rais
 
Ni wazo zuri ila sema wakurugenzi wengi ni wezi wazoefu (isipokuwa labda wanawake). Panahitajika kufumuliwa halmashauri, kuanzia wakuu wa idara mpaka wakurugenzi wawekwe wenye maadili, lakini sehemu kubwa ya wakurugenzi, wakuu wa idara ni wezi na waongo waongo. Zaidi nigependekeza wanawake wapewe nafasi
 
Kwenye hiyo LIST ya wakuu wa wilaya kuna watendaji kibao walioko wilayani kawapa ukuu wa wilaya.Kachukua watendaji wale wa Hapa kazi TU sio wenye vyeo na bla bla nyingi
 
We utakuwa hujui unachosema, wakuu wa wilaya, wengi ni wanasiasa,wakati wakurugenzi ni watumishi wa umma, kwa hiyo unataka kila mkurugenzi awe na kadi ya chama, kitu ambacho utumishi unakataza
 
Mkuu Hapana, sio kweli kwamba kila mtumishi wa umma haruhusiwi kuwa mwanachama wa Chama cha siasa!!

Wakurugenz wa halmashauri wanaruhusiwa kuwa na kadi za Chama wakipendacho, Rejea Kanuni F. 20(1)(2) pamoja na Kanuni F. 21 za Kanuni za Kudumu za utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009 utawajua watumishi gani waliopigwa marufuku kujihusisha kwenye siasa na wale walioruhusiwa pamoja na masharti yake !!
 
Mkuu nitaipitia ninayo soft copy
 
We utakuwa hujui unachosema, wakuu wa wilaya, wengi ni wanasiasa,wakati wakurugenzi ni watumishi wa umma, kwa hiyo unataka kila mkurugenzi awe na kadi ya chama, kitu ambacho utumishi unakataza
Mkuu vp kuhusu hao wakurugenzi 22 walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya nao walikuwa na kadi za chama?
Lakini pia kama haitoshi kuna wana jeshi wameteuliwa nao nimakada wa chama?.

Rais ana nahitaji watendaji makini na sio makada wa chama kama unavyofikiri ondoka ktk fikra hizo.
 
Nimesema wengi sio wote, nielewe kwa hilo.
 
Mkuu Hapana, sio kweli kwamba kila mtumishi wa umma haruhusiwi kuwa mwanachama wa Chama cha siasa!!

Wakurugenz wa halmashauri wanaruhusiwa kuwa na kadi za Chama wakipendacho, Rejea Kanuni F. 20(1)(2) pamoja na Kanuni F. 21 za Kanuni za Kudumu za utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009 utawajua watumishi gani waliopigwa marufuku kujihusisha kwenye siasa na wale walioruhusiwa pamoja na masharti yake !!
Mkuu ungemkumbusha pia kuwa wakati huu wa Rais Magufuli haangalii sana makada wachama kwa sababu kilichotokea wakati huu wa uteuzi wa wakuu wa wilaya pia wameteuliwa wanajeshi ambao sio wanasiasa.
 
Hao former DED ambao sasa ni DC watakuwa walimu wazuri kwa current DED jinsi ya kuiba na si kuzuia wizi. Chezea mfumo ccm wewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom