Wakuu wa Mikoa wapatiwa Semina ya utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Prisca Ulomi, WHMTH

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamekutana na Wakuu wa Mikoa yote nchini Jijini Dodoma na kuwapa semina ya kujenga uelewa wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi ili kurahisisha utekelezaji na usimamizi wa Mfumo huo katika ngazi ya mikoa na halmashauri zote nchini.

Akizungumza wakati wa semina hiyo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa wakuu hao wa mikoa ndio wasimamizi wa shughuli zote na vipaumbele vya Serikali katika Mikoa yao hivyo wana jukumu kubwa la kuwahamasisha wananchi na wadau katika utekelezaji na matumizi ya mfumo huo na kuhakikisha ifikapo mwezi Aprili, 2022 asilimia 75 ya watanzania wawe na Anwani za Makazi na Postikodi katika maeneo yao ya makazi, maeneo ya biashara na ofisi

Ameongeza kuwa Wakuu wa Mikoa wana jukumu la kuzielekeza halmashauri kukamilisha utayarishaji na uidhinishaji wa majina ya barabara na mitaa na kutengeneza sheria ndogo za utekelezaji na matumizi ya mfumo wa Anwani na Makazi na Postikodi katika ngazi ya halmashauri

Dkt. Ashatu ameishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa utayari, ushirikiano mkubwa na ushauri kwa Wizara ya kisekta kutenga bajeti ya sekretarieti ya mikoa ili kuweza kufanikisha malengo ya Serikali ya kila mwananchi kuwa na Anwani za Makazi.

Kwa upande wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa mbali na vipaumbele vingi walivyonavyo katika Wizara hiyo Mfumo wa Anwani na Makazi ni muhimu hasa katika kuimarisha huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi

Amesema kuwa kupitia utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi Idara ya Uendelezaji Miji itahakikisha miji inapimwa na kupangwa vyema ili kurahisisha ufikishaji wa huduma mbalimbali za Serikali kwa jamii.

 
Mbona huo mradi umeshazinduliwa kipindi Cha JK Tena walianzi Dodoma,au mleta Post ulikuwa hujazaliwa,au viongozi wanafikili sisi Ni wasahaulifu Sana?
 
Hivi kweli jambo kama hili ni la kuwakusanya watu kutoka nchi nzima Dodoma?....huyu Ummy si alikataa hawa watu kuzunguka hovyo ili wasimamie zile hela?

Sasa wanagawana posho tena kwa jambo kama hili.....alafu hii tabia ya kutengeneza posho za lazima sijui kwa nini huyu Rais analiangalia tu.

Katika kusimamia mambo kama haya hatutaacha kumkumbuka JPM maana hakuna namna.
 
Back
Top Bottom