georgina george
Senior Member
- Dec 19, 2012
- 114
- 30
Salaam Zenu Wakuu!
Mimi ni mama wa watoto watatu, wote wa kike. Watoto wote hao nilijifungua kwa njia ya operation. Wakati wa mimba ya kwanza niliambiwa na Daktari kuwa siwezi kujifungua kwa njia ya kawaida hivyo nilifanyiwa Emergency Caesarian ili kunusuru maisha yangu pamoja na mtoto. Mimba mbili zilizofuata nilifanyiwa a Planned Caesarian. Pamoja na watoto wote watatu kuzaliwa kabla ya muda (premature), thank Lord, watoto wote wamekua vizuri wakiwa na afya njema.
First born yuko Kidato cha 2 mwaka huu, wa pili Class 5 na watatu yuko Chekechea.
Mwaka jana (2013) mimi & my husband tuliamua kutupa karata zetu za mwisho, japo mwenzangu mwanzoni alikataa akishauri kuwa watoto watatu wanatosha regardless of being the same gender. Nilitumia busara sana kumshauri mwenzangu kuhusu kutengeneza mtoto mwingine wa nne na wa mwisho. Lengo langu likiwa at least kubahatisha a baby boy, Lord knows!
Mnamo Aug, 2013 sikuona siku zangu, obviously nilijua kitu kimenasa!
Nisiwachoshe sana; in short lipo tatizo linalonipa wasi wasi ambalo ndilo lengo kuu la kuleta hapa jamvini thread hii.
Nimekuwa niki hudhuria clinic mara kwa mara na pia Daktari alifanya calculations zake na kunijulisha kuwa tarehe yangu ya kufanyiwa OP itakuwa 15.04.2014.
Nilipotimiza wiki ya 34 ya ujauzito wangu, niliamua kufunga safari na kwenda kwa mama yangu mzazi ili nipewe uangalizi wa karibu. Nilipofika kwa mama mzazi, baada ya siku mbili au tatu hivi nikwenda clinic (hospitali nyingine) pia Daktari wa pale naye alifanya calculations zake akitumia kadi ya clinic niliyokwenda nayo toka hospitali ya mwanzo. Huyu Daktari wa pili aliniambia kuwa nitafanyiwa OP tarehe 11.05.2014! Nilimwambia kuwa ni tarehe 15.04.2014, Daktari huyu alikataa na kuniambia kuwa yeye yuko sahihi na kwamba yule wa kwanza alikosea hesabu.
Tatizo langu: Binafsi hii variation ya siku takriban 27 kati ya hesabu za hawa madaktari wawili inanichanganya sana wakuu! Naogopa risk zitakazojitokeza endapo huyu Daktari wa pili atakuwa amekosea hesabu zake.
NINAOMBA USHAURI WENU WANA JF PAMOJA NA MADAKTARI WALIOPO HAPA JF.