Wakuu, Nihame Kijiwe Changu??

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,643
Reaction score
4,185
WAKUU,

KAMA KAWAIDA YANGU NIME_CHILL HAPA MITAA YA SAVEI MKABALA NA MLIMANI SITI,
KIJIWENI KWANGU NAPOFANYIA BIASHARA YANGU YA KUUZA MAHINDI YA KUCHOMA YA 500/= NA KIPANDE 200/=,

MARA IKAJA SUZUKI_SWIFT MOJA,
IKAPAKI KIJIWENI,
NDANI KULIKUWA NA DADA MWEUPE KINOUMAH- AKANUNUA HINDI MOJA, AKAWASHA NDINGA AKASEPA KUELEKEA NJIA YA CHUO KIKUU.

BAADA YA SAA 2 ILE GARI IKAREJEA,
AKAHITAJI MAHINDI MENGINE 6 ILI WAWAPELEKEE NDUGU ZAKE KWAO,
NIKAMWAAMBIA KUWA LABDA NIYAMENYE KISHA NIYACHOME MAANA'KE YALIYOPO TAYARI NI VIPANDE TU!

AKASEMA,
SIO TATIZO, NIMCHOMEE TU ATASUBIRI.

SASA WAKATI NACHOMA YALE MAHINDI
AKAPITA MCHIZI WANGU MMOJA, AMBA'E NI JIRANI YANGU KULE KITAA CHA KIGAMBONI_TOANGOOMA NILIKOPANGA CHUMBA CHANGU CHA BUKU 6 KWA MWEZI,
AKANISABAHI

" @Seneta_Wa_Mtwiz
niaje kiongozi,
Umeadimika sana
I see!
Hata JF sikuoni kabisa mkuu."

NIKAMWAMBIA,
"Daaaaaaaah!
Ni changamoto tu za maisha niliibiwa simu yangu!"

YULE DADA NILIYEKUWA NAMCHOMEA MAHINDI AKAPIGWA NA BUTWAA KINOUMAH!!!

AKASHUKA KWENYE GARI KWA MSHANGAO HUKU ILE FIGA YAKE MATATA KAMA YA #HAMISA_MOBETO IKITAMALAKI VEMA!!!

AKAONGEA KWA MSHANGAO,

"Whaaaaat!!!!
Are you really Seneta Wa Mtwiz who always uses to make humor on JF?"

NIKAMWAMBIA,
"Kawaida tu,
Kuna tatizo kwani?"

AKAJIBU,
"It is typical impossible to find a person doing odd jobs of this kind manage to access highly respected social utility like JF-
Are you truly the one?!?!."

HUKU AKIWA NA KIGAGAZIKO CHA HALI YA JUU,
NIKAMWAMBIA,
HAYA MAISHA TU.

TUKAPIGA SOTRY KADHAA,
NIKAMCHEKESHACHEKESHA NA STORI ZA HARMORAPA-
NIKAMALIZA KUCHOMA MAHINDI YAKE NIKAMKABIDHI.
ALIYAPOKEA, AKAYALIPIA LAKINI AKASITA KUONDOKA.

ALIONEKANA KUWA NA NENO FULANI,
ILA ALISHINDWA KUONGEA.
AKAPANDA NDINGA AKASEPA HUKU AKINIPUNGIA MKONO KWA TABASAMU NA BASHASHA!!!

SASA MIDA HII
NIMEKUTA UJUMBE MTU KANI_PM,
ASEMA;
"Meeting you for that little while at Survey,
I've been very interested in making a certain sensitive talk with you.

I always use to pass there going to Ardhi University where I have some activities to attend.

Can U arrange for that seneta please?"

------
SASA WAKUU,

MIMI BADO SIJAMJIBU!!!

NAJIULIZA,
HUYU DADA ANATAKA KUNUNUA MAHINDI YA KUCHOMA AU ANA LENGO GANI LINGINE HUYU??

AU NIHAME KILE KIJIWE?!?
MAANA ASIJE KULETA MAMBO YA KUTEKANATEKANA!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahahhaaa huyo seneta kwa vyovyote vile atakuwa anamtaka huyo dada mchoma mahindi.
Na huyo dada atampenda tu maana kashaona hiyo swift ya seneta. Pia ule weupe wa seneta umemchanganya huyo dada maana Hamisa Mobeto si haba.
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Akili za usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…