Nawasalimu wakubwa kwa wadogo.
Poleni na hizi mvua za tangu leo asubuhi ( kwa wakazi wa Dar).
Namshukuru Mungu ni siku nyingine, nipo mzima wa afya.
Nikienda kwenye lengo la uzi moja kwa moja.
Mimi ni kijana wa miaka 23,
Elimu yangu nilifanikiwa kupata O- level, A- level hadi chuo kikuu.
Kwa bahati mbaya nimeshindwa kuendelea na masomo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu.
Mungu akipenda mwakani kuna uwezokano nitaanza upya tena. Naamini hivyo.
Kwasasa nipo hapa mjini sina ramani ya maisha na nyumbani huko mkoani fursa hazipo za kutafuta hela. Najua nitadoda na kuwa mzigo kwa ndugu.
Nipo hapa nikiomba fursa yeyote halali ya kufanya wakati nasubiria mwaka mpya wa masomo.
Binafsi nina ufanisi wa kazi za Bustani. ( I can design botanical gardens in a mesmerizing and abundant appearance).
Nimezunguka kwenye bustani za hapa Dar es salaam bila mafanikio ya kupata fursa, sina connection.
Kwa heshima na busara zote naomba mnisaidie jinsi ya kupata hizi fursa.
Nitafurahi nikipata nafasi nyumbani kwa mtu kazi yangu iwe ku design na kutunza bustani nipo tayari nipatiwe hifadhi na chakula tu, mshahara atafikiria kwa utendaji kazi na ufanisi.
Nimekwama sana wana jamiiforums, hapa nilipo Mungu ndio anajua, kiufupi nimejishikiza sehemu kwa muda nikiangaika kupata mchongo wowote na sehemu ya kujisitiri.
Nawashukuru wote, karibuni mnisaidie mwana jamiiforums mwenzenu, tunapita tu hapa Duniani tusaidiane inapo bidi.
Ukiguswa naomba unitafute PM
Amina.
Sent using Jamii Forums mobile app

!...plus ujifunze kisukuma
!