Wakuu hiki Kitabu kilichozinduliwa leo kuhusu familia kina maana gani?

elishaezekiel

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
563
1,461
Naona wanasheria wanawake kwa kushirikiana na Serikali ya sweden ( Serikali ni watu kama mimi na wewe basically) wamemualika rais wetu kuzindua document fulani leo kuhusu familia

Hii imenipa wasiwasi mkubwa hasa kama Serikali itaanza kujipatia nguvu za kisheria kuregulate familia.... ambapo ni wazi itapendelea jinsia ipi kwa kisingizio cha kuikomboa jinsia hiyo. Hofu zaidi ni watu walioandaa document hiyo Wanasheria wanawake. Haki za wanaume zimelindwa kweli kwenye hii document?

Ni hatari kwa sababu itakapokua rahisi mtu kwa hisia zake tuu kujiamkia asubuhi na kuona anaonewa then amtupe mwezio kortini. Nawaonea huruma sana wanaume wanaofurahia ndoaa kuanzia sasa. Kutakua na kesi za ajabu ajabu huko mbeleni.

Marekani divorce rate inapita asilimia 50 na waanzilishi wa kesi nyingi ni wanawake kwa kisingizio cha kuumizwa hisia au mwanaume kutotimimiza mahitaji kwa hisia zake na mtazamo wake.

Ushauri wangu ni kwamba jamii zetu nyingi ni patriarchy na jamii zetu zimesimama kihivyo. Familia ziachwe kuwa patriarchy. America wanashuhudia anguko la familia kwa sababu tuu wanaona ni sahihi kuweka upendeleo na kuona kana kwamba wanaume wanasitahili kukandamizwa na kwamba haki za wnaume zinaonekana kuminywa. Mambo ya almony na family support

Unapoweka haki za Mwanamke weka wazi na haki za mwanmme, gender equity iweke msisitizo wa haki za wanaume as well. Hakuna vita ya Mwanamke na mwanamme ambayo mwanmke anaweza kushinda hata kama sheria itaegemea upande huo wa ke

Familia zetu zibaki traditional kama tunataka kukeep jamii zetu kwani familia zinajengwa hivo. Mkiitungia sheria kali familia wanaume hatutakubali, tutawala sana na hatuakubali commitment na ke yoyote, tutawacha. Hakuna mtoto kwa sababu hao ndiyo watakua mwiba kwa wanaume. Hawa wanawake wanasheria wengi feminism imewahadaa.
 
SSH amekuwa mwanaharakati wa jinsia badala ya role yake kama RAIS

Kila akikaa maongez yake n jinsia jinsia ×3 Kama dozi

Mwambien anaongoza jamii za kiafrika na si jamii za kizungu sisi tuna Mila na drsturi zetu

Hao wanaojiita deep state mhimil uliojichimbi ndan y mihimil mingne inaangalia TU
 
Umewasilisha hoja kwa hisia sana japo ndio ukweli wenyewe huo. Ninaziona athari za kuwa na rais mwanamke anayetanguliza maslahi ya jinsi yake kuliko majukumu mapana ya urais wake. Nimeanza kuamini kwanini jamii zetu hazikuwa tayari kuongozwa na rais mwanamke. Ukifuatilia vizuri kauli zake nyingi zimejaa uharakati wa kijinsia tu ni hatari sana na hii italeta shida kwenye jamii zetu hasa familia nyingi zitaanguka.
 
Mama anaupiga mwingi....

....na badooo (2025 - 2030) loading...

Itakuwa hata ukimkonyeza mkeo asipofurahia anakuburuza mahakamani tu....

Mfumo dume chalii....
IMG-20211028-WA0209.jpg
 
SSH amekuwa mwanaharakati wa jinsia badala ya role yake kama RAIS

Kila akikaa maongez yake n jinsia jinsia ×3 Kama dozi

Mwambien anaongoza jamii za kiafrika na si jamii za kizungu sisi tuna Mila na drsturi zetu

Hao wanaojiita deep state mhimil uliojichimbi ndan y mihimil mingne inaangalia TU
Hasira zake kwa bwana hafizi znahamia kitaaa dadeeeeeek
 
Hii ni mbaya sana Rais ni mkuu wa nchi na sio mwana harakati hasa wa jinsia

Pia jamii yetu bado haijaandaliwa vya kutosha kielimu mira na tamaduni zetu bado zina kinzana sana mfumo wa kimagharibi
Tunapaswa kuwa sisi kama sisi na sio kuiga kila kitu.
 
Naamini rengo la Rais ni jema pia kwa upande wake, labda kumekuwa na makosa kidogo kwenye kuweka sheria baada ya kosa kufanyika, kama hiyo ya kwenda mahakaman au mtu flani kupewa nguvu zaidi ya mwenzake, kama ni kwenda mahakaman basi ingekuwa ni kwa wote pasipo kujali ni mwanamke au mwanaume, (gender equality).

Lakini pia kwa namna moja au nyingine, huko mwanzo ni kweli mwanamke amekuwa akikandizwa sana, amekuwa chini kwa sababu ya jinsia yake, hivyo ni vema haya mabadiliko kuwepo pia, hii ikatoe fursa kwa dada zetu na mama zetu waliopo kwenye ndoa, na wanaotarajiwa, na hakuna kipindi kizuri vha kufanya haya, isipokuwa kipindi hiki cha Raisi mwanamke, huu ni muda wao sasa.

Hivyo kama kumekuwa mabadiliko haya ni vema basi kukawa na mashauri mazuri zaidi yenye kuboresha hizi sheria, nikiwa na maana kuwa zisiwe sheria za kutoka kumkandamiza mwanamke hadi kuanza kumkandamiza mwanaume, bali ziwe sheria za ukweli, haki sawa na mabadiliko yenye hekima. Maana kama hizi sheria zikija kumkandamiza mwanaume, akirudi tena Raisi mwanaume atazivunja na kutakuwa akuna kilichofanyika.

NIMEMALIZA
 
Back
Top Bottom