Wakurugenzi Duniani Wanalipwa 'Pakubwa'

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Kumekuwa na mjadala kuhusu ukubwa wa malipo ya baadhi ya Wakurugenzi Wakuu (CEO) na Wakurugenzi wa kawaida (average executives) katika mashirika ya umma (hata private) Tanzania (ambayo yanapaswa kujiendesha na ikiwezekana kuleta faida), ukilinganisha na watumishi wa kawaida (average worker).

Katika pitapita yangu nimekutana na discussion paper ya mwaka 2008 waliyoandika Ebert, Torres na Papadakis wa taasisi yenye mamlaka kamili, International Institute for Labour Studies, iliyo chini ya International Labour Organization (ILO). Chapisho hili linaitwa Executive Compensation: Trends and policy issues.

Makala hii ilikuwa inatazama mwenendo wa malipo ya wakurugenzi kwa nchi sita (6) duniani, ambazo taarifa zake zilikuwa wazi – Afrika ya Kusini, Hong Kong (China), Ujerumani, Australia, Uholanzi, Ujerumani na Marekani.

Kwa ufupi chapisho linaonesha kuwa kuna tofauti ya mishahara kati ya nchi na nchi, lakini pia kila nchi Wakurugenzi wanalipwa mishahara mikubwa ukilinganisha na wafanyakazi wa kawaida. Na haya ndiyo waliyogundua:

  • Bila kujali marupurupu mbalimbali, Wakurugenzi (CEO na average executives) walioneshwa kulipwa mara 71 hadi 183 ya malipo ya mtumishi wa kawaida.
  • Ukiongeza marupurupu, malipo yao yaliongezeka na kuwa mara 103 hadi 521 ya malipo ya mfanyakazi wa kawaida!!!
  • Wakurugenzi waliopo Afrika ya Kusini na Hong Kong (China) walionekana kulipwa kidogo, ukilinganisha na wenzao walioko Marekani, lakini hata hivyo wakurugenzi wa nchi hizi walikuwa wakilipwa mara 48 hadi 148 ya mshahara wa mfanyakazi wa kawaida.
  • Mkurugenzi mkuu (CEO) aliyepo Afrika Kusini alikuwa analipwa zaidi ya 50% ya mkurugenzi wa kawaida (average executive).
  • Mwaka 2007, wastani wa mshahara wa Mkurugenzi Mkuu kwa Afrika ya Kusini, ulikuwa analipwa Dola 1,370,824 (sawa na Shilingi za kitanzania Bilioni tatu (3)) kwa mwaka. Hii ni sawa na shilingi za kitanzania milioni 250 kwa mwezi. Huku Mkurugenzi wa kawaida akilipwa Dola 934,378 (sawa na Shilingi za kitanzania bilioni mbili (2)) kwa mwaka (sawa na Shilingi milioni 170 kwa mwezi).
  • Ripoti hii ilitumia taarifa kutoka makampuni mbalimbali, mojawapo ya makampuni ya Afrika Kusini yaliyotajwa katika taarifa hii ni Standard Bank (ndugu wa Stanbic Bank), AngloGold Ashanti na Telkom.

Kwa kumalizia, kuna andiko fupi Forbes 2014. Linazungumzia mishahara ya baadhi ya kampuni Marekani kwa mwaka 2013. Chapisho linasema kwa mwaka 2013, Mkurugenzi Mkuu alikuwa analipwa (wastani) mara 774 ya malipo ya mtumishi wa kima cha chini.

Toka mwaka 1978 hadi mwaka 2013, malipo ya CEO Marekani yaliongezeka kwa 725% huku ya mfanyakazi wa kawaida yakiongezeka kwa 127% tu.

Mwaka 1978, CEO alikuwa ana “take home” mara 26.5 ya mfanyakazi wa kawaida, lakini kwa mwaka 2013 take home ya CEO ilipanda na kuwa mara 206 ya malipo ya mfanyakazi wa kawaida.

Nawasilisha.

  1. http://www.ilo.org/wcmsp5/groups/public/---dgreports/---inst/documents/publication/wcms_193236.pdf
  2. Report: CEOs Earn 331 Times As Much As Average Workers, 774 Times As Much As Minimum Wage Earners
  3. The pay gap between CEOs and workers is much worse than you realize
  4. CEO-To-Worker Pay Ratio Ballooned 1,000 Percent Since 1950: Report
  5. CEO Pay Continues to Rise as Typical Workers Are Paid Less
 
sawa wacha walipwe tu
mi siwezi kufika uko
ila mwanangu atafika
 
Watanzania tumejaa wivu na majungu, naposema watanzania namjumlisha hadi rais maana katika hali ya kawaida rais huwezi kuzungumzia mshahara wa mfanyakazi hadharani, huo ni wivu.

Kuna baadhi ya wakurugenzi kutokana na aina ya kazi inayofanywa na shirika wanaloliongoza huwezi kuwalipa mshahara mdogo, kwa mfano huwezi kusema umlipe mkurugenzi wa Tpdc mshahara wa milioni 2 wakati kwa kiwango chake anakutana na wakurugenzi wa makampuni makubwa ya gesi na mafuta duniani,lazima alipwe vizuri ili awe na confidence ya kujadiliana.

Huwezi kumpeleka mtu mwenye njaa akajadiliane mkataba na alieshiba hadi kubakisha chakula utegemee kutakua na uwiano au ulinganifu katika majadiliano.

Lazima baadhi ya wakurugenzi walipwe vizuri, tuache wivu na majungu,mtu anaesaini mikataba ya mabilioni umpe mshahara wa milioni 2 haiwezekani hata mimi sitakubali. Alafu tuache unafiki sijui ishu za uzalendo na nini, hayo hayapo, yanazungumzwa kinafiki, tuache unafiki, wivu na majungu.
 
CEO ni watu wakubwa kwenye kampuni, strategy na mikataba watayopitisha ndio itaamua uelekeo wa kampuni. Nje CEO analipwa kulingana na kiasi shirika ilichoingiza kutokana na strategy zilizoidhinishwa na CEO na kuwajibishwa kama mambo yataenda mrama. Tanzania CEO wapo kwaajili ya upigaji tu mashirika yao hayana mipango wa kufufua biashara hadi yanakufa ila wao wanalipwa pesa ndefu na kufanya meetings nje ya nchi bila sababu za msingi, mwisho wanaenda kuomba pesa hazina wakati inabidi mashirika ya umma ndiyo yachangie hazina. CEO kulipwa pesa ndefu ni sawa kama shirika linafanya vizuri
 
Kama wale wahujumu uchumi wa ttcl, atcl, reli n.k, kila mwaka ni kuomba pesa za uendeshaji wa mashirika, mwisho wa siku wale wa trl waliimba pesa za operation wakaishia kulipana mishahara. Ujinga mtupu
 
Ndio tatizo lao lilipo mtu ajaonyesha thamani yeyote ndani ya shirika watu wanatetea mishahara mikubwa wanayopata based on the title only.

Hiyo nakala should tell him kwanini Marekani ma CEO wanamishahara mikubwa mtu anasimamia kampuni BP au Google zinazozalisha faida ya mabillioni huyo utamlipa kiasi gani unadhani; hawa watanzania waseme faida hiko wapi walau ata kuonyehs umuhimu wao.

Kwanza hakuna hata competition ya uajiri sio kwamba hawa wakurugenzi eti wakiacha huko kuna watu wapo tayari kuwakamata wala hakuna uhaba wa ma CEO ni watu wanaochaguliwa kisiasa tofauti kabisa na nchi nyingine mtu anapewa malengo ya shirika na muda wa kufikia leo kuna watu malengo waliojiwekewa wenyewe awajayafikia ndani ya muda. Mkata unaisha anapewa nyongeza ya mkataba on what justification na mshahara nyongeza huu sasa ndio upuuzi wenyewe.
 
Kama wale wahujumu uchumi wa ttcl, atcl, reli n.k, kila mwaka ni kuomba pesa za uendeshaji wa mashirika, mwisho wa siku wale wa trl waliimba pesa za operation wakaishia kulipana mishahara. Ujinga mtupu
Ajabu hawa watu bado wanakazi zao haya mambo yanawezekana Tanzania tu halafu tunashangaa kwanini tu miongoni mwa nchi maskini
 
Back
Top Bottom