Mkuu, naomba kutofautiana na wewe katk hili kama ifuatavyo:
- Suala hili umelikuza sana kulihusisha na jamii ya kimasai badala ya kulichukulia kama la mfugaji yeyote au kosa la huyo mchunga ng'ombe ambaye kwa utashi wake kaamua kuchungia shambani.
- Ukiangalia hilo shamba kwenye picha ni kama mkulima alishalitelekeza na hivyo kuvutia mchunga ng'ombe kupitisha mifugo yake shambani.
- Lakini pia hilo shamba linaweza kuwa la huyo mfugaji kaamua kulisha mifugo yake baada ya kuona pengine mavuno hakuna. Ulimpata mwenye shamba ukasikia malalamiko yake au unatanguliza hukumu kwa wafugaji tu..?
Tuwe makini katk kuangalia uhalisia tukitaka kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji. Vinginevyo tutaufanya mgogoro kuwa mkubwa ikiwa pia utahusu kabila fulani badala ya kushughulika na mwenye kosa.
Eng. WFM