Wakulima wadogo hali si shwari tena

Wakulima wadogo hali si shwari tena

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,439
Reaction score
3,951
Serikali ingilieni kati, Mbolea imekuwa na masharti magumu kununua, sasa hivi hakuna kupima kwa kilo, kila mkulima analazimika kununua mfuko wa Kilo 50 ambao bei yake ni sh 50,000-55,000 wengine hawana mashamba makubwa ya kutumia mfuko wa 50kg ukizingatia mifuko ya 25kg haipatikani kwa urahisi, viwatilifu vya kuulia wadudu (dawa) zimekuja kwa bei ya ghali sana wengine kama Manyara wamepiga dawa zaidi ya mara 3 wadudu hawafi tuna wasiwasi na hizi dawa, , dawa zilizotoka mwaka jana tumezitafuta hazipo madukani kwanini? kwa mwaka jana shamba langu nilipiga dawa mara moja tu wadudu wakafa kwa sasa nimenunua dawa moja wapo nimepiga wadudu hawafi nimerudi dukani nikaambiwa nipige dawa mara 3 nikawauliza kama wanajua kazi ilivyo ngumu kubeba mtungi wa dawa mgongoni isitoshe unamlipa mtu wa kupiga dawa unamipa mara ngapi kwa kila tripu.

Basi naomba serikali waliangalie swala hili popote pale ambapo dawa zina feli hii haipo kwenye historia ya miaka ya hivi karibuni kuwa ukipiga dawa wadudu hawafi, gharama kwa wakulima wadogo ni kubwa sana hata mbegu zenyewe bei ni ile ile pamoja na serikali kutangaza kuwa wametoa tozo kwenye mbegu za kilimo.

Itakuwa vyema kama dawa hizi za kuulia wadudu wa mashambani ziwe kwa bei rahisi, mbolea ishuke bei na mbegu ishuke bei ili WENGINE TUSIMAME NA KILIMO. maana kama viuatilifu (dawa) zitakuwa ghali, mbolea masharti magumu kupata na mbegu bei ghali tu hii kilimo tunayosema itatufikisha wapi mwisho wa siku tutaacha kulima na tutafute maisha mengine.

Baada ya kuyasikia haya nimeomba off mapumziko ya wiki 2 ili nikabiliane na hawa wadudu maana mashamba yamevamiwa.
 
Hali si shwarii wadudu wamegoma kufa kabisaa.

Mkuu achana Na serekali waziri wa kilimo ni jiwe kama bosi wake anapwaya kwenye hicho cheo.

Bei ya dawa ni kubwa Na ni changamoto kupiga dawa heka 50 au 100 si mchezo
 
Hilo la mbolea ya kupima mbona nasikia serikali ndo imetilia mkazo? Kwamba sheria hairuhusu kuuza mbolea ya kupima kwani inapoteza nguvu kwa kuachwa wazi...ila bei ya mbolea kwa mfuko haikamatiki, mbolea kama SA na CAN tulizoea bei za chini kwa sasa 50,000 wakati mwezi September mwaka Jana ilikuwa 32000/ kwa SA.
 
ni shida sasa wakulima wadogo wenye nusu heka watafanyaje
 
Hili la mbolea viwanda vya mbolea vitakiwe pia vifungashe mbolea katika uzito wa chini ya kilo 50 ingawaje nimewahi mbolea iliyofungwa kwenye mifuko ya kilo 5
 
KWA MARA YA KWANZA MWAKAHUU KWA WAKULIMA WA PAMBA TUMETUMI GHARAMA KUBWA NA WADUDU HAWAFI..SISI HUKU WILAYA YA CHATO NDO TUMEOPPIGWA HASARA NA DAWA ZISIZOUA.TULIKUWA NA DAWA NZURI UNAPULIZA MARA TATU LAKINI MWAKAHUU KWA EKARI MOJA NIMEPULIZA MARA KUMI NA HAKUNA KITU WADUDU WANAENDELEA KUTOBOA MATUNDA.BODI YA PAMBA NA TPRI WANATUDANYA TU KUWA ETI TUNAKOSEA KUPUULIZA..TUMEWAMBIA WACHAGUA SHAMBA MOJA WALIPUULIZE NA KULISIMAMIA KWA MWEZI TUONE MATOKEO HAWATAKI..WAKULIMA WA PAMABA MWAKAHUU NI HASARA KUBWA SANA
 
kijijini kwangu, unapanda vizuri kesho unakuta panya wamefukua na kula mbegu zote za mahindi.
hutakiwi kukata tamaa, ila kuboresha mbinu za kupambana na changqmoto.
 
Ni vurugu tupu mkuu...wanasema eti wachangiane!
Nilikuwa nahitaji kilo 315 ya UREA imekuwa ngumu sana kupata yani napata kilo 300 ambayo ni mifuko 6 sasa iyo 15 naipata wapi vinginevyo nichukue kilo 25 ila ile kumi itakayo baki basi tena nijue pa kuipeleka ila bei sasa ndo ngoma na mifuko ya kilo 25 ndoma kuipata haipatikani kwa urahisi.
 
Kumbe kulima si mchezo.
Alafu wasio na ajira wanaambiwa wakalime.
ukiambiwa watu wakalime basi hakikisha mbolea, dawa na trekta vina ushuru mdogo, serikali ilitangaza kuwa tozo zote kwenye mbegu ziliondolewa lakini wauzaji wana kisingizio kuwa mbegu waliyo nayo ni stok ya zamani ambayo walikuwa wameshalipia zile tozo ila Waziri wa Kilimo ajue kwamba wanasiasa hawana mashamba na hawamo kati ya wakulima wadogo watuache.
 
Hili swala serekali iliangalie Kwa jicho la tatu na iliwekee nguvu na mkazo Kama ilivyoshughulikia vyeti fake. Kilimo ndo uti wa mgongo,ukivunjika huwezi,j kusimama na kumbuka kinaajiri zaidi ya 75% .
 
KWA MARA YA KWANZA MWAKAHUU KWA WAKULIMA WA PAMBA TUMETUMI GHARAMA KUBWA NA WADUDU HAWAFI..SISI HUKU WILAYA YA CHATO NDO TUMEOPPIGWA HASARA NA DAWA ZISIZOUA.TULIKUWA NA DAWA NZURI UNAPULIZA MARA TATU LAKINI MWAKAHUU KWA EKARI MOJA NIMEPULIZA MARA KUMI NA HAKUNA KITU WADUDU WANAENDELEA KUTOBOA MATUNDA.BODI YA PAMBA NA TPRI WANATUDANYA TU KUWA ETI TUNAKOSEA KUPUULIZA..TUMEWAMBIA WACHAGUA SHAMBA MOJA WALIPUULIZE NA KULISIMAMIA KWA MWEZI TUONE MATOKEO HAWATAKI..WAKULIMA WA PAMABA MWAKAHUU NI HASARA KUBWA SANA
Hivi uwanja wa ndege si ndio mahitaji yenu wanachato? Tumieni uwanja kuulia wadudu
 
tatizo ni kwamba dawa tulizotumia mwaka jana zikaua hazipo tena madukani zimeletwa zingine tofauti hii biashara sijui ni ya nani
KWA MARA YA KWANZA MWAKAHUU KWA WAKULIMA WA PAMBA TUMETUMI GHARAMA KUBWA NA WADUDU HAWAFI..SISI HUKU WILAYA YA CHATO NDO TUMEOPPIGWA HASARA NA DAWA ZISIZOUA.TULIKUWA NA DAWA NZURI UNAPULIZA MARA TATU LAKINI MWAKAHUU KWA EKARI MOJA NIMEPULIZA MARA KUMI NA HAKUNA KITU WADUDU WANAENDELEA KUTOBOA MATUNDA.BODI YA PAMBA NA TPRI WANATUDANYA TU KUWA ETI TUNAKOSEA KUPUULIZA..TUMEWAMBIA WACHAGUA SHAMBA MOJA WALIPUULIZE NA KULISIMAMIA KWA MWEZI TUONE MATOKEO HAWATAKI..WAKULIMA WA PAMABA MWAKAHUU NI HASARA KUBWA SANA
 
Hilo la mbolea ya kupima mbona nasikia serikali ndo imetilia mkazo? Kwamba sheria hairuhusu kuuza mbolea ya kupima kwani inapoteza nguvu kwa kuachwa wazi...ila bei ya mbolea kwa mfuko haikamatiki, mbolea kama SA na CAN tulizoea bei za chini kwa sasa 50,000 wakati mwezi September mwaka Jana ilikuwa 32000/ kwa SA.
Miaka nenda rudi tunatumia vibaba mhenga, sema wabongo bado sana kila kitu kama mikondoo mitamba tu, wacha vikaze zaidi!
 
Hivi mihogo pia inahitaji mbolea wakuu. Aina gani na wakati gani wadau...?

Thanks.
 
kijijini kwangu, unapanda vizuri kesho unakuta panya wamefukua na kula mbegu zote za mahindi.
hutakiwi kukata tamaa, ila kuboresha mbinu za kupambana na changqmoto.
Hao panya dawa yao ni kuwala tu!, hivi huko kwenu hakuna watu wanaokula panya?, waalikeni Wamakonde wawasaidie kuwapunguza.
 
Back
Top Bottom