Wakufunzi wa vyuo vya elimu ya juu ni chanzo cha kutoa Graduates wasio na sifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakufunzi wa vyuo vya elimu ya juu ni chanzo cha kutoa Graduates wasio na sifa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rich Dad, Aug 17, 2011.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wengi wao hasa ma-professor ni wababaishaji! Wanajifanya hawana muda, na mara nyingi huwa hawamalizi syllabus. Wakiulizwa wanatoa majibu mepesi tu, kwamba upo university, no more spoon feeding. <br />
  Hiyo haitoshi, vitisho ndo usiseme. Wanafurahia sana pale idadi kubwa ya wanafunzi inaporudi kuja kufanya supplementary exams. <br />
  Nchi za wenzetu ni tofauti, lecturers wanafurahi wanapoona wanafunzi wao wameelewa kile walichofundishwa na hivyo ku-pass final exams.
   
 2. K

  Karry JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ni kweli kabisa wahadhiri wanachangia hivyo wanafunzi unakuta muda mwingi wanapambana na kufaulu mitihani hata kwa mbinu chafu badala ya kuelewa masomo
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hebu fafanua kwenye red...
   
 4. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Ila pia baadhi ya wanafunzi hawako serious hata kidogo! Wengi hawaingii madarasani, hawafanyi asignments, hawasomi, research wanadesa, we unategemea nini? Wanafunzi wengi wa vyuo kutwa utawaona wanazurura tu mjini na kuendekeza ulevi n.k. Wakifeli ndio wanaanza visingizio ooh maprofesa hawafundishi..
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hii ni skendo kubwa mkuu Rich Dad, na ni hatari kwa maendeleo ya elimu yetu pia kwa wanafunzi wetu. Hebu naomba utubandikie majina ya hao Ma-professor/wakufunzi wa vyuo ili tuweze kufuatilia.

  Naimani JF ni zaidi ya hapa kwenye kompyuta, hivyo kuna members wengine wako responsible na hizi inshu wanaweza kusaidia nakapata ufumbuzi wa hili tatizo.
   
 6. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kweli hawa maprofesa,madokta mimi huwa nawashangaa sana ,kuna kitu hawana kwanza hawajali wapo wapo usanii ukubwani,anakusaidia umeshamwomba mpaka umechoka kuna mmoja alinifanyiaga vituko ,nlishia kujiuliza huyu alisoma ili aje atese watu au ni hulka binafsi.
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Mi naona wahadhiri wa elimu ya juu wako juu ya sheria, sidhani kama kuna chombo chochote kinachowaangalia ama kuhoji utendaji wao. Ndo maana katika taasis hizi maamuzi ya mhadhiri huwezi kuyapinga. Akiamua kuchelewesha kazi ya mwanafunzi hakuna anayepinga wala kuhoji.
   
 8. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,084
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi nao hawapo serious na shule. Wanaendekeza sana anasa siku hizi!
   
 9. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Siku zote mtafutaji huwa hachoki. Hivyo kama wewe unania ya kweli na shule soma kwa bidii kuliko kupotea muda wako kwa kuwafuatilia hao wakufunzi wako. Kumbuka aliye juu usimngoje chini mfuate hukohuko juu bana. Ukipoteza muda kumsubiri hapo chini lazima ile kwako.
   
 10. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Our eucation has got what we call a colonial legacy.Kuna kupeana adhabu indirectly Tz.

  Kutokana na hayo mimi binafsi sikupenda soma nchini.Huku Maprof n rafiki zangu,nikiwa na shida naweza enda hadi nyumbani kwake.

  Mfano:Not long ago I did my first research.Prof was ready to help to the extent I never imagined.Sikumoja nilishinda kwake nikifanya naye kazi hadi saa nane za usiku.Furaha yake ilikuwa ni kuona mwanafunzi wake anafanikiwa.
  Pia sasa kuna mwanafunzi mwenzangu alifeli,Prof alimtafuta il amfundishe zaidi jamaa ajiandae na mtihani vizuri.

  Changamoto:Hii fani ina watu wanaojivuna kwa kuwa ni wachache na wanabembelezwa sana.
  Kuna favour kibao mfano kuingiza magari bandarini,kwenda kusoma na kulipiwa na serikali bila shida.Nafikiri serikali yetu ina nia njema lakini ukoloni bado upo mioyoni mwa wengi wao.

  We can start a network of youth who are interested at lecturing.Then the same network can lead a campaign to educate these people respect ethics of their work.
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Wahadhiri wengi wababaishaji, darasani wanaishia kusomea watu slides ambazo hawajaziandaa wao, wanataka uandike kile walichokisema tu. Kwa kifupi wanalazimisha kukariri. Asilimia kubwa ya walionifundisha pale UDSM wapo hivyo, nashindwa kuelewa huo udokta waliupata vipi.
   
 12. n

  nyantella JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Naomba kujua jinsia yako na ya prof. wako please ili nifanye maamuzi sahihi!
   
 13. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Siku hizi wanachuo wengi hawako kimasomo nali ki anasa zaidi. Ni mwendo wa kukopi na kupaste assignment na reserch za waliotanglia. MF. Thesis ya UDSM utaikuta kama ilivyo Mzumbe mtu anapata MBA. Nadhani ma lecture wana kazi ngumu ya kupambana na hali hii.
   
Loading...