Cathode Rays
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 1,738
- 1,495
Wakuu hivi tunaposali kabla ya kula huwa tunabariki chakula au tunaomba Mungu akibariki chakula?
Kwangu mimi ni
(1) fursa nzuri kujinyenyekeza kwa Mungu na kurudisha Shukrani kwake kwa upaji wake wa Chakula. Ni wakati pia kuifanya familia yangu ijue si tu kwa sababu ya kazi ya baba yao ndiyo maana wanakula bali upaji wa Mungu....unaweza kuwa na Chakula lakini usiweze kula.....
(2) fursa nzuri kuomba Mbele za Mungu aweze kuwagusa wengine wenye uhitaji wa Chakula na akunjue mkono wake wenye Neema na kuwapatia Chakula