Wakopaji wa fedha

Uzi wa maana sana huu,naamini wenye hii tabia wataacha mara moja kwasababu ni makusudi na kujitoa tu ufahamu

Inashangaza mtu kurudisha hela bila kuzingatia makato
Joanah umepatia kabisa, yaani ni kujitoa ufahamu' kwa makusudi kabisa! Mtu mzima unashindwaje kujua kuwa kuna makato?

Kama hawa viumbe hawaachi hii tabia
wasishangae siku wakikwama wakakuta milango yote imefungwa na hakuna wa kuwasaidia tena.
Wema wetu usitufanye tuonekane wajinga.
 
Yaan ukampa kadi? 🙄🙄🙄Kadi ya benki? Mbongo huyo unampa kadi hata angekuwa bilionea as long as ni mbongo sithubutu😂😂🤣...watu mna moyo🙌🙌
 
Kwa sasa ukimpa mtu mkopo hesabu kama umetoa sadaka tu.

Kuna mtu kanililia sana nimsaidie $2500 kumnunulia na kumtumia vitu Bongo. Kanililia shida saana.

Nimemsaidia, kunirudishia ananizingua.

Nikasema ilikuwa tufanye deals kubwa zaidi, lakini kwa style hii sitaweza na unazibia wengine wote watakaokuja baada yako, kwa sababu Wabongo mnaonekana si waaminifu.
 
Yaan ukampa kadi? 🙄🙄🙄Kadi ya benki? Mbongo huyo unampa kadi hata angekuwa bilionea as long as ni mbongo sithubutu😂😂🤣...watu mna moyo🙌🙌
Aisee ni mtu wa heshima sana, hapo ndio nilijua kuwa Pesa haina heshima, kila mtu ni kibaka akipata nafasi(ndio lugha iliyotamkwa na msuluhishi), Alinifuata mahali ambapo nilikuwa siwezi kutoka, nikampa kadi.
 
Kabisa, kama mtu anakukopa kiroho safi kabisa, lakini kulipa anaona kama anakusaidia wakati ulimkopesha, Wakati mwingine anakulipa kidogo kidogo wakati alimpa kwa mara moja.
hakika! kuna watu wana fikra za ajabu kweli, anakukopa anakwambia nitakupa siku flani, ila kwa sababu umenyaza anaona uyu hana shida nayo anapotezea, na siku nyingine anaweza kuja kukukopa bila aibu kabisa !
 
Ina hitaji moyo Sana , hiyo ndiyo njia ya kupima kama MTU ana shukrani au la .

Kama umegundua Hana shukrani nazani utakua ushajua cha kufanya .
 
Mnafanya nini kuwapenda wawapendao maana hata makahaba huwapenda wawapendao nanyi mkopeshapo msitizamie kurudishiwa maana hata wenye dhambi hufanya hivyo pia bali nyinyi mtoapo toeni kwa moyo wala mstalajie kupokea kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…