Wako wapi watakao fuata baada ya hawa kuondoka?

Wako wapi watakao fuata baada ya hawa kuondoka?

Background Check

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2019
Posts
378
Reaction score
577
Yupo mwandishi mmoja nguli sana Afrika, hapa namzungumzia Chinua Achebe, huyu ni mwandishi kutokea katika nchi ya Nigeria, alifariki mwaka 2013.

Ameandika maandishi mengi hasa katika mashairi na riwaya za kusisimua kwelikweli. Chinua si tu mwandishi wa riwaya za kawaida, alijikita katika riwaya tundulizi na zenye kuacha maswali kwa msomaji.

Nimebahatika kusoma vitabu vyake kadhaa katika maktaba zetu hapa nchini Tanzabia. Miongoni mwa vitabu nilivyo visoma kutoka kwa mwandishi huyu ni pamoja na "Things Fall Apart" cha mwaka 1958, "No Longer at Ease" kilichapishwa mwaka 1960, "Arrow of God" chapisho la mwaka 1964 na "A Man of the People" cha mwaka 1966.

Niweke baya vitabu vyote hapo vinanizidi umri hata baba na mama yangu bado hawawezi kulinga na umri wa vitabu nilivyovitaja.

SASA KILICHONIVUTA niandike uzi huu ni hiki kitabu cha "Things Fall Apart" cha mwaka 1958 anauliza "Where are the young suckers that will grow when the old banana tree dies"

Kwa lugha ya hapa nyumbani anauliza hivi;
"Iko wapi migomba chipukizi itakayoota baada ya migomba ya zamani kufa?"

Nimejitahidi kuandika kiswahili chepesi ili tuelewe maana ya swali hili maridhawa.

Mwandishi ametolea mfano wa mgomba (mti wa ndizi) kama alama ya maisha halisi yetu sisi binadamu. Ndugu zangu wa Mbeya, Upareni, Uchagani Bukoba na kwingineko, mnafahamu fika kuhusu tabia za mmea huu, pindi unavyozidi kukua, pembeni yake huanza kuchipua vitoto vya mgomba (chipukizi). Mchakato huu huleta matumaini kuwa mgomba mzee unaenda kufa lakini tayari kuna chipukizi zimeshaandaliwa kuja kuchukua nafasi ya mgomba unaoenda kumaliza muda wake.

Ufafanuzi huu wa mfano wa falsafa na mtazamo wenye nguvu kuhusu mzunguko wa maisha. Ipo hali isiyoepukika ya mabadiliko, na desturi.

Kimsingi swali la Chinua, alikuwa anauliza wako wapi wataalam watakao saidia jamii/taifa pale wataalamu waliopo watakapo ondoka?, aidha kwa umauti, kustaafu, kufungwa, kubadili imani yao njema waliyokuwa nayo (kukengeuka) nakadharika.

Anauliza Chinua, wako wapi viongozi watakaofuata baada ya viongozi waliopo kuondoka katika nafasi zao, kwa vyovyote vile aidha kwa vifo, magonjwa, umri na hali nyingine zitakapo amua kuwaweka pembeni?

Anauza kuhusu madaktari mahiri, wandishi wa habari mahiri, wanasheria wabobevu, anauliza kuhudu wahadhiri wabobevu, watu wema, wanasiasa, wazazi, viongozi, wako wapi wanausalama wa taifa wabobevu, nk. Hiyo ndo fasihi, aliyoiandika mwanafasihi kwa zama zake.

Mwisho japo si kwa umhimu, Sentensi hii ni moja aliitumia Chinua "THINGS FALL APART BECAUSE AN ARROW OF GOD IS NO LONGER AT EASE" akaigawanya na kupata vitabu vitatu "Things fall apart", "an arrow of God" na "No longer at ease".

Akimaanisha kuwa mambo yanaharibika kwa sababu mshale tuliopewa na Mungu tutumie kujilinda haupo tena upande wetu (ambao ni utamaduni na mila zetu).

Mambo yanaharibika kwa sababu nguvu za Mungu haziko tena kwenye amani.

Nyakati anaandika huyu Chinua Uchebe maneno haya ni imani yangu zilikuwa zama za akina Keneth Kahunda, Nkwame Nkuruma, Julius Nyerere, Jomo Kenyatta, Nelson Mandera, Thomas Sankara, Patrick Lumumba, nk...

Leo chinua Achebe hayupo, alifariki March 21, 2013.
Nashukuru Mungu kwa maisha ya mtu huyu, mtu mwandishi katika zama zake.

Nauliza leo mimi machepele wa Tanzania. "Iko wapi migomba chipukizi itakayoota baada ya migomba ya zamani kufa?"

Na je ni migomba gani unatamani tuikumbuke na tuwe kama hiyo?.
 
Back
Top Bottom