Wako wapi wachezaji hawa wa zamni wa Simba na Yanga?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Wanamichezo wote nawasalimu,pamoja na salamu zangu naomba kujua walipo wachezaji wafuatao:

1. Malota soma-Simba
2. Juma Kampala-Yanga
3. Mohamed Bakari Tall-Simba
4. Idd Seleman Mayor-Simba
5. Yanga Bwanga-Yanga
6. Elisha John-Yanga

Hakika wachezaji hawa ni miongoni mwa wachezaji bora katika taifa letu
 
Mungu awape pumziko Elisha John na Yanga fadhiri Bwanga
Aamin. Ingawa hawa wachezaji walicheza katika vipindi viwili tofauti. Wakati Yanga Fadhili Bwanga alivuma miaka ya 1970s akiwa Dar Young Africans, Elisha John alitingisha miaka ya mwanzo ya 1980s akitokea Coastal Union kwenda Simba SC kisha Young Africans

Usajili wa Elisha John kutoka Simba kwenda Yanga ulivunja rekodi ya fedha ya uhamisho pamoja na kwamba soka lilikuwa la ridhaa wakati huo huku akiwa analipwa mshahara mnono tofauti na wenzie kitendo kilicholeta mtafaruku kwenye timu ikiwepo kuletwa mgomo baridi miongoni mwa wachezaji wengine
 
Kama sijasahau Hutu Elisha John alipoenda Yanga wachezaji wenzake kama unavyosema walimgomea mpaka ndani ya uwanja wakitaka kila kitu afanye yeye kisa amenunuliwa kwa bei kubwa,sikumbuki aliondokaje Yanga kurudi Coastal union
 
Huyo hapo Marehemu Yanga kabla ya mauti
Screenshot_20191111-153610_Chrome.jpeg
 
Kama sijasahau Hutu Elisha John alipoenda Yanga wachezaji wenzake kama unavyosema walimgomea mpaka ndani ya uwanja wakitaka kila kitu afanye yeye kisa amenunuliwa kwa bei kubwa,sikumbuki aliondokaje Yanga kurudi Coastal union

Hakucheza sana maana kiwango chake kilishuka sana baada ya uhamisho huo kwani inasemekana hata wazee wa Coast hawakumpa baraka kwa hiyo kuna mambo ya miba yaliendelea
P
 
Al
Kuna mchezaji alikuwa anachezea Simba anaitwa Aluu Ally je kwa sasa yupo wapi?
Aluu Ally alicheza na kina Omar Mahadhi Bin Jabir, Mwinyi Kidekeo, Filbert Rubibira, Adam Sabu, Thuweni Ally, George Kulagwa na wengineo

Kwavyovyote kama atakua hai basi umri utakua umekwenda sana kama au zaidi ya kina Leodger Tenga, ila yuko wapi na anafanya nini kwasasa kwakweli sina taarifa zake
 
Aluu Ally alitokea Morogoro na alichukuliwa na Simba akiwa anasoma kidato cha tatu ktk shule ya Forest hill.Alikuwa zao la umiseta na klabu ya Jogoo na alipojiunga na Simba 1976 aliendelea na masomo yake pale Azania.Alipomaliza kidato cha nne alitimkia zake Uarabuni ambako kipindi hicho kilikuwa wimbi la wachezaji wengi kukimbilia Uarabuni. Simba ikawapoteza kina Yusuf Kaungu, Shaban Baraza, Haidari Abeid, Khalid Abeid,Lumelezi,Thuweni Ally, Kikwa, Mustapha,Innocent Haule, huku Yanga ikiwapoteza kina Yanga Bwanga na Pan Africa ikwapoteza kina Bona Max, Kassim Manara, Adolf Rishard na wachezaji wengine wamenitoka
 
Yusuf Kaungu Kwa sasa yupo wapi?
 
Wanamichezo wote nawasalimu,pamoja na salamu zangu naomba kujua walipo wachezaji wafuatao:

1. Malota soma-Simba
2. Juma Kampala-Yanga
3. Mohamed Bakari Tall-Simba
4. Idd Seleman Mayor-Simba
5. Yanga Bwanga-Yanga
6. Elisha John-Yanga

Hakika wachezaji hawa ni miongoni mwa wachezaji bora katika taifa letu
Mbona umemsahau DOTTO RUTA MOKILI?
 
Nakummbuka nikiwa UAE miaka ya 1998-2002 alikuwa naye akiwa Sharijah, UAE. Kutokea kipindi hicho sina taarifa zake na hata hii ya Yanga Bwanga kutangulia mbele za haki nimefahamia humu JF sports.

Hivi hatuna taasisi za kimichezo za kutunza kumbukumbu za wachezaji hawa
 
Back
Top Bottom