Wakenya wakutwa na silaha za kivita Tarime

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
RAIA wawili wa Kenya pamoja na mkazi wa wilayani Mkoa wa Mara, Tarime wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na bunduki ya kivita na risasi 21.

Kamanda wa Polisi wa Tarime Rorya, Gemini Mushi alitaja raia hao wa nje waliokamatwa ni Masiaga Matinde (35) na Ambrose Maibo ambao ni wakazi wa Ntimaro Masangura Wilaya ya Kurya katika Mkoa wa Nyanza, Kenya.

Mtuhumiwa ni Mtanzania, Chacha Samson aliyekamatwa na raia hao wa Kenya wakiwa na bunduki aina ya AK 47 (SMG) baada ya msako ulioendeshwa ndani ya wiki moja.

Kamanda Mushi alisema Februari 12, mwaka huu polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema wakidai kuwapo mtuhumiwa wa ujambazi sugu kutoka Kenya anayeendesha uhalifu akishirikiana na wengine katika mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na mji wa Isebania, Kenya.

“Tulifuatilia nyendo zake na kufanikiwa kumkuta amelala chumba namba 12 katika nyumba ya kulala wageni Paris Pub iliyopo Sirari. Alipopekuliwa alikutwa na risasi za SMG 20 akiwa amezificha uvunguni,” alisema Kamanda.

Kamanda Mushi alisema baada ya kumkuta akiwa na risasi 20, walimhoji akawaambia ilipo bunduki wanayotumia.
 
hawa watu ni hatari kwa usalama wa nchi yetu na raia wake...wadhibitiwe na wafikishwe mbele ya sheria haraka!
 
Ujambazi pale Sirari ni tatizo sugu polisi wanawajua majambazi sijui kwa nini hawawakamati rushwa imetawala sana
 
Hii system ya kulinda nchi tuliipata kutoka urusi .mahotelini ,maofisini ,mashuleni,,uraiani,magerezani,kwenye majeshi, kwenye vyama vya kisiasa, hao watu wapo
 
Back
Top Bottom