Wakenya waishtaki Tanzania

mafiyang'ombe

Member
Apr 16, 2011
5
1
Raia kumi wa Kenya wameituhumu Serikali ya Tanzania, kwa kukamatwa kwa kuwateka jijini Maputo nchini Msumbiji Januari 2006, ambako walikuwa wakiishi kihalali wakitafuta fursa za biashara, na kisha kuwapakiza kwenye ndege ya kijeshi na kuwaleta nchini Tanzania kwa nguvu.

Kwa upande wake, serikali ya Tanzania kupitia mawakili wake imepinga madai hayo na kuitaka mahakama ya Afrika kutupilia mbali maombi ya watuhumiwa. Tanzania inasema watuhumiwa hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuletwa kupitia ndege ya jeshi la Msumbiji.

Wakenya hao wanahoji kuwa kesi yao nchini Tanzania imechukua muda mrefu kwa kuahirishwa mara kwa mara bila sababu. Aidha wanadai kuwa kesi imeendeshwa bila wao kuwa na mawakili wa kuwatetea.

Mawakili wa serikali ya Tanzania pia waliieleza Mahakama ya Afrika kuwa, wawili kati ya raia hao wa Kenya waliofariki wakiwa magereza, walikufa kwa kifo cha kawaida, na kesi iliahirishwa mara kwa mara kutokana na mawakili wa walalamishi kukosa kufika mahakamani siku za kesi.

Wakenya hao walikamatwa miaka kumi iliyopita na kuhukumia kufungwa miaka thelathini jela, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji na ujambazi wa kutumia silaha lililofanyika katika benki ya NMB Tawi la Moshi, mwezi May,2004.

Mahakama ya Africa kuhusu haki za binadamu na za watu iliundwa mwaka 2006 na kuanza kazi zake rasmi mwaka mmoja baadae. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi februari 2016, Mahakama imepokea kesi 74, ambapo 25 kati ya hizo zimekwisha shughulikiwa, huku kesi 4 zikipelekwa katika Tume ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu nchini Gambia.

Chanzo: BBC
 
Mbona Wakenya wanaionea Tanzania hivi.Fursa za Tanzania wanajimilikisha tena wanataka waanze na kudai tena ma-fidia
 
Kwa upande wake, serikali ya Tanzania kupitia mawakili wake imepinga madai hayo na kuitaka mahakama ya Afrika kutupilia mbali maombi ya watuhumiwa. Tanzania inasema watuhumiwa hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuletwa kupitia ndege ya jeshi la Msumbiji.

Utekwe Msumbiji na kuletwa tanzania ? Kesi hii ya aina yake mpakani au uwanja wa Ndege wa Msumbiji walipitishwaji?
Je ukamataji haukuwa na baraka za Serikali ya Msumbiji?

Sijui kama move hii haina Mkono wa Serikali ya Kenya wakati huu wa pilika pilika ya bomba la gesi toka Uganda!
 
Naona majambazi wamepata pa kupumulia, yaani wakishindwa ktk mahakama zote za Tanzania wanakimbilia huko Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika. Nyambafu. Uzuri ni kuwa hiyo mahakama ya Afrika haina mamlaka ya kuwatoa jela, yenyewe huwa inaishia kushauri tu kama kweli haki za binadamu zilivunjwa au la.
 
Utekwe Msumbiji na kuletwa tanzania ? Kesi hii ya aina yake mpakani au uwanja wa Ndege wa Msumbiji walipitishwaji?
Je ukamataji haukuwa na baraka za Serikali ya Msumbiji?

Sijui kama move hii haina Mkono wa Serikali ya Kenya wakati huu wa pilika pilika ya bomba la gesi toka Uganda!

Wakenya hao walikamatwa miaka kumi iliyopita na kuhukumiwa kufungwa miaka thelathini jela, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji na ujambazi wa kutumia silaha lililofanyika katika benki ya NMB Tawi la Moshi, mwezi May,2004.
 
Naelewa sana ! Labda wewe hujaelewa hoja yangu!
Hoja yangu iko kwenye madai yao mapya eti kuwa wakati ule walipokamtwa wao wanadai walitekwa na kwa maana hiyo hawakufanya Kosa bali walibambikiwa kesi hapo upo?
 
Serikali ya Tanzania wao wanadai kuwa jamaa walikua watuhumiwa wa ujambazi waliotorokea Msumbiji baada ya kufanya tukio Moshi NMB, na serikali ya Msumbiji ikawamata ikawapakia kwenye ndege ya kijeshi mpaka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania.

Watuhumiwa wanadai kuwa waliowakamata ni serikali ya Tanzania na sio msumbiji, wakiwashutumu kwa ujambazi walioufanya Tanzania, na wanakana mashtaka.

Sasa anayetakiwa kuthibitisha hilo ni Serikali ya Msumbiji kama ni kweli iliwakamata ikawakabidhi Tanzania ambako walikuwa wanatafutwa au Tanzania ndio iliwakamata na kuwabambikizia kesi kama wanavyodai.
 
Na kwenye kesi yao hawakuwa wakenya pekee,kulikuwa na watanzania pia,na pia Kuna watanzania waliofia jela waliokuwa pamoja nao, ila wakenya huwa wanajiona ni very special pamoja na ukibaka wao.
 
Raia kumi wa Kenya wameituhumu Serikali ya Tanzania, kwa kukamatwa kwa kuwateka jijini Maputo nchini Msumbiji Januari 2006, ambako walikuwa wakiishi kihalali wakitafuta fursa za biashara, na kisha kuwapakiza kwenye ndege ya kijeshi na kuwaleta nchini Tanzania kwa nguvu.

Kwa upande wake, serikali ya Tanzania kupitia mawakili wake imepinga madai hayo na kuitaka mahakama ya Afrika kutupilia mbali maombi ya watuhumiwa. Tanzania inasema watuhumiwa hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuletwa kupitia ndege ya jeshi la Msumbiji.

Wakenya hao wanahoji kuwa kesi yao nchini Tanzania imechukua muda mrefu kwa kuahirishwa mara kwa mara bila sababu. Aidha wanadai kuwa kesi imeendeshwa bila wao kuwa na mawakili wa kuwatetea.

Mawakili wa serikali ya Tanzania pia waliieleza Mahakama ya Afrika kuwa, wawili kati ya raia hao wa Kenya waliofariki wakiwa magereza, walikufa kwa kifo cha kawaida, na kesi iliahirishwa mara kwa mara kutokana na mawakili wa walalamishi kukosa kufika mahakamani siku za kesi.

Wakenya hao walikamatwa miaka kumi iliyopita na kuhukumia kufungwa miaka thelathini jela, baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji na ujambazi wa kutumia silaha lililofanyika katika benki ya NMB Tawi la Moshi, mwezi May,2004.

Mahakama ya Africa kuhusu haki za binadamu na za watu iliundwa mwaka 2006 na kuanza kazi zake rasmi mwaka mmoja baadae. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi februari 2016, Mahakama imepokea kesi 74, ambapo 25 kati ya hizo zimekwisha shughulikiwa, huku kesi 4 zikipelekwa katika Tume ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu nchini Gambia.

Chanzo: BBC
Nawaunga mkono Wakenya, hata kama wana makosa ya jinai. Kuwa na makosa hakumaanishi usitendewe ubinadamu. Kwa jinsi ninavyoijua Tanzania ya wakati wa JK, mambo kama haya mara nyingi yaendeshwa kwa hisia za mtu tu. Maadam ni Wakenya..... basi. Halkadhalika, Watanzania wengi wanateseka na mfumo huu wa kutojali sheria. Ila kwa Watanzania ni vigumu kushtaki. Na hata wakishtaki ni vigumu kupatiwa haki. Tanzania ni moja ya nchi zenye ukiukaji mkubwa haki za binadamu duniani. Kwa kweli ni ajabu kwa nini haijamulikwa kimataifa na kuaibishwa au kuchukuliwa hatua. Nina imani kuna kesi nyingi tu zinazofaa kupelekwa ICC, kama ile ya mwandishi wa habari aliyeuawa kidhuluma na serikali kushindwa au kutotaka kuwahukumu waliofanya hivyo. Ile ni ICC material na mark my word, tunafanya kazi, siku moja itaibuka.
Hatuwezi kuwa na nchi ambayo inaendeshwa kwa vitisho, ubabe na umuungu mtu, tangu Nyerere, kisa tu wananchi wake wapole au hawajui sheria na haki zao. Inabidi ifike mahali hata nchi yako uisute.
Baada ya kusema hayo, nadhani Magufuli atakuwa tofauti kidogo.
 
Back
Top Bottom