Wake wa kaka zangu

Wake wa kaka zangu

mchalomba

Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
19
Reaction score
2
Jamani wana JF nisaidieni ushauri.

Sisi tulizaliwa 7, wavulana 3, na wanawake 4.

Bahati mbaya wazazi wetu wote walishatangulia mbele ya haki.

wavulana wote wameoa na wasichana wameolewa.

Kwa upande wetu sisi 7 tunapendana. Kwa wasichana huwa tunatembeleana, tunasaidiana, kwa kifupi tuko karibu sana. Tatizo kwa hawa wifi zetu. Yaani kitu cha ajabu hawapendani wao kwa wao utafikiri wake wenza jinsi wanavyochukiana. Pia wanatuchukia sana sisi wifi zao. Ajabu hata watoto wao hawaruhusiwi kwenda kwa baba mkubwa au mdogo, kwa shangazi ndio kabisa sikumbuki kuwa walikuja lini kwangu.

Tofauti na mimi nilikoolewa, huwezi tofautisha kati ya sisi tuliolewa na wifi zetu, tunapendana tunashirikiana na hata watoto wetu wanapendana sana, wakiwa likizo wanatembeleana, yaani wamekuwa zaidi ya ndugu, wamekuwa marafiki kwani kila mara kwa mara wanapokuwa likizo wanakuwa pamoja wakati wanaishi mikoa tofauti.

Natamani wake za kaka zangu hata wapendane tu wao kwa wao, acha wasitupende sisi mawifi lakini wao wapendane na washirikiane ili wawainue waume zao. Kwani kutokana na tabia ya kuchukiana naona hata Mungu anafunga mibarakwa kwa kaka zangu kwani mambo yao hayaendi vizuri kabisa.
 
Huo uwifi na ushemeji uliopitiliza ndio chanzo cha Usaliti, kama munasalimiana na kuongea haina haja ya kila siku tuonane si unajua shetani mbaya
 
Kila familia mkuu ndivyo hivyo hivyo,usidhani ni kwenu tuu!muhimu ninyi ndugu pendaneni msikubali kukaliwa na hao wa kuja
 
Aisee pole sana!!!!!! lakini unge jaribu kuzungumza na kaka zako kwanza kabla hujaja hapa ili tujue wao wana changamoto gani katika hili!
japo naelewa hao wifi zako si ndugu zako ni wamkataba hao ndo zao zikivunjika watakuwa wanasema yule alikua wifi yetu na si wifi yetu! pia wao kwa wao si ndugu xo undugu wa mkataba ni mgumu sana mpaka kidogo urejee mkataba, ambao wanajua wao na waume zao so zungumza na kaka zako kwanza kwani ndio walifunga huo mkataba!
wewe unawapenda wifi zako wote kama ndio tumia uzoefu wako wapendane kama hapana basi ndio mfumo wa maisha!
 
Kwani shosti pakacha kuvuja si nafuu ya mchukuzi au? as long as nyie na kaka zenu mnaelewana inatosha,hao wifi wasikushughulishe sana wewe,wapendane wasipendane kila mmoja kaletwa na njia yake wamekutana kwenye hapa mjini tena kwa sababu ya kakazenu kwahiyo usijichoshe akili,kumbuka kua wao ni wifi na watabakia kua wifi tuu,wakiundoka wao
watakuja wengine....
 
Usiumize kichwa,pendaneni nyie ndugu na msaidiane hao mawifi muwaache kama walivyo watakuja kujielewa siku moja na watajirud
 
Huo uwifi na ushemeji uliopitiliza ndio chanzo cha Usaliti, kama munasalimiana na kuongea haina haja ya kila siku tuonane si unajua shetani mbaya

Acha habari za ajabu labda wawe wamelaniwa!, na sisi tuko saba kama wao ila kwetu wakike ni 2 na me ni 5! tunapendana sana watoto wa ndugu zangu wanapendana mno sijawahi ona mambo ya ajabu kama unayo waza wewe kutokea!
 
Kwani shosti pakacha kuvuja si nafuu ya mchukuzi au? as long as nyie na kaka zenu mnaelewana inatosha,hao wifi wasikushughulishe sana wewe,wapendane wasipendane kila mmoja kaletwa na njia yake wamekutana kwenye hapa mjini tena kwa sababu ya kakazenu kwahiyo usijichoshe akili,kumbuka kua wao ni wifi na watabakia kua wifi tuu,wakiundoka wao
watakuja wengine....

ninaowahurumia sana ni watoto. Unajua kwa ujinga wao hata kaka zetu wamekuwa kama mazezeta vile wanasikiliza wake zao, hata watoto shule ni shida.
Yaani watoto wetu na wakwao wanakuwa na utofauti kubwa sana utafikiri sio ndugu. Watoto wananiumiza sana.
 
Pole Mpenzi lakini mambo mengine ukilazimisha sana utakuta jambo lisilo kuridhi zidi kumuomba mungu awape upeo wakujua ndugu zake...
 
Huo uwifi na ushemeji uliopitiliza ndio chanzo cha Usaliti, kama munasalimiana na kuongea haina haja ya kila siku tuonane si unajua shetani mbaya

cha maana tunaheshimiana licha ya kupendana. Pia tunawafundisha watoto wetu wapendane na wajue ni ndugu, hata ikitokea mmoja wetu hayupo duniani wajue wana wazazi na ndugu wa kumshauri na kushirikiana.
 
Back
Top Bottom