KERO Wakazi wa Magengeni, Kijitonyama, hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko baada ya chemba za maji machafu kufumuliwa na kuachwa yakitiririka siku tatu

KERO Wakazi wa Magengeni, Kijitonyama, hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko baada ya chemba za maji machafu kufumuliwa na kuachwa yakitiririka siku tatu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
980
Reaction score
3,646
Wakazi wa Mtaa wa Magengeni, Kijitonyama, wamejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya ujenzi ulioanzishwa na jamaa mmoja kusitishwa kwa siku tatu huku ukiwa tayari umesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, ujenzi huo umesababisha kuzibwa kwa njia za maji taka, barabara kuharibika, na zaidi ya yote, uchimbaji wa chemba za maji machafu umeongeza hatari ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu. Mazingira hayo pia yamekuwa mazalia ya mbu, jambo linaloongeza hatari ya malaria kwa wakazi wa eneo hilo.

“Tuna hofu kubwa kwa sababu chemba hizi zinatoa maji machafu, na hakuna hatua zilizochukuliwa. Pia, hakuna njia rahisi kwa wagonjwa wa dharura kutolewa ndani ya mtaa huu kwa haraka,” alisema mmoja wa wakazi wa Magengeni.

Kero kubwa zaidi kwa wakazi ni kwamba hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu shughuli za ujenzi huo. Hata wanachama wa kundi la WhatsApp la serikali ya mtaa hawakufahamishwa, jambo linaloibua maswali kuhusu usimamizi wa maendeleo katika eneo hilo.

Wananchi sasa wanatoa wito kwa mamlaka husika kuingilia kati haraka kurekebisha hali hiyo na kuhakikisha usalama wa afya zao.

 
Back
Top Bottom