Tumesubutu tumeweza
Hiki tulikitamani na Leo tumeonyesha kwa Vitendo.
Chome ni Kijiji ambacho kina lango la kuingilia Mlima mrefu wa Shengena ambapo kila mwaka huingiza kipato kikubwa.
Shuhuli za kiuchumi ni Kilimo Cha Vitunguu, Kabichi Karoti Maharage na mengineyo mengi.
Tunaiomba Serikali itusaidie fungu la kutosha na ikiwezekana ijengwe kiwango Cha lami.
Pia naomba ikiwezekana Barabara hii iingizwe Tanroad kwani kutokana na milima mikali na miamba Tarura bado hawatoweza kuikabili Barabara hii.
Hongera kwa Serikali yetu ya awamu ya 5 kwani ni sikivu itasikia maombi ya Wana Chome.
Nizungumzie shule ya sekondari Chalao kidogo kua tunaomba Serikali iifanye kuwa na vidato vya 5 na 6 kwani ina maabara ya kisasa nazani kwa Kanda ya Kaskazini ni maabara ya kisasa na yapo shule 3 tu kwa Kanda.
Mengi zaidi karibuni Chome
Umoja wetu Nguvu yetu.
Nelson Mndeme