Wakazi wa kata ya Chome wanaoishi nje ya kata hiyo wameunga mkono jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya barabara ya urefu wa kilomita 15

TAMU YA LEO

Member
Mar 26, 2020
8
45
Same
Wakazi wa kata ya Chome wanaoishi nje ya kata hiyo wameunga mkono jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilomita 15 baada ya serikali kutengeneza barabara ya Sanga Chome Kakoa kilomita 9 kati ya 24.

Hamad Waziri Hamad mkazi wa Chome alisema kuwa kutokana na barabara hiyo kutopitika kutokana na ubovu hususan kipindi cha mvua kumepelekea shughuli nyingi za kimaendeleo kukwama.

Alisema serikali ya awamu ya tano imekuwa na nia njema ya kuwajengea barabara kwa kilomita 9 kati ya 24 na hivyo wameona ni vyema kushiriki kwa kuongeza nguvu ili kuweza kuondoa changamoto hiyo.

''Wakazi waliopo nje ya hapa watachangia fedha na sisi tutajitoa kwa nguvu kazi lengo ni kuhakikisha tunaunga mkono jitihada za serikali kutuboreshea barabara yetu''alisema
Kwa upande wake Mhandisi Joseph Kakore ambaye ni mwakilishi wa wakazi wa Chome wanaoishi nje ya eneo hilo ambapo alisema umoja wao unaunga mkono jitihada za serikali kutatua kero hiyo kwani barabara hiyo ni muhimu kwa ustawi wa kata hiyo sanjari na kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Alisema barabara hiyo matengenezo ambayo yatahitajika ni pamoja na umwagaji wa vifusi vya moramu ujengaji wa mitaro na njia zakuchesha maji ambapo kazi zote zitaenda kwa ubia kati ya wakazi wanaoishi Chome na wale waliopo nje ya kata hiyo.

Napendael Mlay mtendaji kata ya Chome alisema kuna baadhi ya maeneo korofi likiwemo kituo cha afya Shengena hadi soko la kata na kuwa barabara hiyo ina mchango mkubwa hususan kufikisha huduma kwa wakazi wa kata hiyo.

Kwa mujibu wa mtendaji huyo barabara hiyo ambayo licha ya kufikakatika hifadhi ya taifa ya msitu wa Shengena vile vile ni kiungo muhimu kwa ustawi wa wakazi wa kata hiyo yenye wakazi zaidi ya 5000 ambapo kukamilika kwa barabara kutawezesha kurahisisha usafirishaji.

Meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA)wilaya ya Same mhandisi Felician Msangi alisema tayari ofisi yake itashirikiana na wadau hao kuhakikisha lengo lao linatimia na kuwa tayari upembuzi yakinifu ulishafanyika kwa ajili ya ujenzi katika kiwango cha changarawe.

Mwisho.
 
MCHARO

Member
Apr 16, 2009
8
45
Kata ya Chome ina kwamishwa na Barabara na nitasema kwa nini

1.Chome ina Msitu wa Hifadhi ya Dunia ambao ni fursa kubwa kwa Utalii, kikwazo ni Barabara na TFS wanalifahamu.

2. Chome haina Soko la Kisasa japo kuwa na Kilimo kinacholeta Maeneo mengi ya Same na Mikoa Mbalimbali. Soko la Chago ni dogo halina hata Choo. Changamoto kwenye Biashara ni Barabara ya Ndiveni- Mhero - Ikokoa.

3. Kituo cha Afya Shengena licha ya kuhudumia Wakazi wa Kata na Tarafa Lakini hakina Mochwari ya kuhifadhi Maiti. Barabara ni kikwazo kwenye Shughuli za Jamii.

Tunamuomba Mheshimiwa Raisi Magufuli, Waziri Mkuu Mkuu, Waziri wa Utalii na Waziri wa Ujenzi watembelee Kata ya Chome na kujionea hali ya Barabara ili kutangaza Fursa za Mlima Shengena, Utalii wa Hifadhi ya Chome ili kuinua Uchumi wa Nchi. Mkuu wa Wilaya ya Same na TARURA wamejaribu kutatua Changamoto zilizoko ndani yao lakini kuna kosekana Uongozi wa kutoa

Msukumo wa Kasi ya Awamu ya Tano ndani ya Kata.
 
MCHARO

Member
Apr 16, 2009
8
45
  1. Wakazi walioko Nje ya Chome wanaitwa "Wacharo"
  2. Barabara iliyo tengenezwa na TARURA ni Msanga hadi Ndiveni.
 
Nehady

New Member
Jun 7, 2020
1
45
Tumesubutu tumeweza
Hiki tulikitamani na Leo tumeonyesha kwa Vitendo.
Chome ni Kijiji ambacho kina lango la kuingilia Mlima mrefu wa Shengena ambapo kila mwaka huingiza kipato kikubwa.
Shuhuli za kiuchumi ni Kilimo Cha Vitunguu, Kabichi Karoti Maharage na mengineyo mengi.
Tunaiomba Serikali itusaidie fungu la kutosha na ikiwezekana ijengwe kiwango Cha lami.
Pia naomba ikiwezekana Barabara hii iingizwe Tanroad kwani kutokana na milima mikali na miamba Tarura bado hawatoweza kuikabili Barabara hii.
Hongera kwa Serikali yetu ya awamu ya 5 kwani ni sikivu itasikia maombi ya Wana Chome.
Nizungumzie shule ya sekondari Chalao kidogo kua tunaomba Serikali iifanye kuwa na vidato vya 5 na 6 kwani ina maabara ya kisasa nazani kwa Kanda ya Kaskazini ni maabara ya kisasa na yapo shule 3 tu kwa Kanda.
Mengi zaidi karibuni Chome

Umoja wetu Nguvu yetu.
Nelson Mndeme
 
Uko Sahihi kabisa Chalao Sekondari ni Miongoni mwa Shule 3 zenye kidato cha 1 hadi 4 ikiwa na Maabara Tatu zinazojitegemea kwa Masomo ya Fizikia, Kemia na Elimu ya Viumbe.
 
hyperkid

JF-Expert Member
Jun 7, 2019
3,174
2,000
Tumesubutu tumeweza
Hiki tulikitamani na Leo tumeonyesha kwa Vitendo.
Chome ni Kijiji ambacho kina lango la kuingilia Mlima mrefu wa Shengena ambapo kila mwaka huingiza kipato kikubwa.
Shuhuli za kiuchumi ni Kilimo Cha Vitunguu, Kabichi Karoti Maharage na mengineyo mengi.
Tunaiomba Serikali itusaidie fungu la kutosha na ikiwezekana ijengwe kiwango Cha lami.
Pia naomba ikiwezekana Barabara hii iingizwe Tanroad kwani kutokana na milima mikali na miamba Tarura bado hawatoweza kuikabili Barabara hii.
Hongera kwa Serikali yetu ya awamu ya 5 kwani ni sikivu itasikia maombi ya Wana Chome.
Nizungumzie shule ya sekondari Chalao kidogo kua tunaomba Serikali iifanye kuwa na vidato vya 5 na 6 kwani ina maabara ya kisasa nazani kwa Kanda ya Kaskazini ni maabara ya kisasa na yapo shule 3 tu kwa Kanda.
Mengi zaidi karibuni Chome

Umoja wetu Nguvu yetu.
Nelson Mndeme
Kwakweli upareni kuna vilima korofi,
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,062
2,000
Tatizo la Chome ni kukosekana viongozi imara wanaoweza kusimamia shughuli za maendeleo za eneo hilo.walioko wamekalia siasa uchwara miaka nenda rudi.Chome ni sehemu nzuri sana ila haipewi kipaumbele ndo maana imechelewa kupiga hatua.Ila kwavile wamelitambua hilo wapambane sasa kwa dhati.
 
year 2006

Member
Jan 14, 2016
81
125
Hakika bara bara ta Chome imekuwa tatizo hasa ndiveni hadi kilindini lazima uwe na gari ya juu ndio upite hiyo njia,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom