Wakazi Mkoani Sumbawanga watozwa faini Zaidi ya milioni 7 kwa uvunjaji sheria ya usafi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
uchafuuuuu.jpg


Wakazi wa manispaa ya Sumbawanga ikiwa ni pamoja na wamiliki wa Hoteli, Migahawa, Bar na nyumba za kulala wageni, wamejikuta wakikumbwa na mzigo wa kulipa faini ya zaidi ya shilingi milioni saba, baada ya kupatikana na makosa ya uvunjaji wa sheria ya usafi wa mazingira, na kukaidi agizo la Rais la kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Bw Hamid Njovu, akiongea mjini Sumbawanga amesema manispaa hiyo inatarajia kuwafikisha mahakamani wakazi wanne ambao wameshindwa kulipa faini ya shilingi elfu 50 kila mmoja, na kwamba zoezi hilo la usafi wa mazingira ni endelevu na la kudumu, na kwamba wakazi wote wanatakiwa kushiriki usafi siku hiyo ya jumamosi kuanzia saa moja hadi saa nne asubuhi na shughuli zote zikiwa zimefungwa.

Akiongelea kuhusu suala la usafi kwenye manispaa hiyo ya Sumbawanga, afisa usafi na mazingira Bw. Hamidu Masare amesema mji huo unaweza kuzalisha kati ya tani 80 hadi 90 za taka ngumu kwa siku, na kwamba halmashauri hiyo ina uwezo wa kuzoa zaidi ya tani 100 kama magari yote matatu yakiwa katika hali nzuri, hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi zima la usafi wa mazingira.

Chanzo: ITV
 
Kama kesi iko mahakamani hiyo milioni saba iko wapi hapo? Ngoja tuone kama mahakama inaongozwa na sheria au ilani ya CCM.
 
Mbona mji wa sumbawanga in mchafu sana tena maeneo ya masoko ambayo yanamilikiwa Na Halmashauri yenyewe?
 
Back
Top Bottom