Wakati umefika

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,682
8,233
Wakati umefika

Mosi

W
akati umefika kwawananchi kushinikiza serikali kubadili sheria ya malipo kwa marais wastaafu na mawaziri wakuu waliostaafu. Imefika wakati wa kufunga mkanda kwa hawa viongozi ambao wanachota pesa za walipa kodi baada ya kustaafu wakati walipokuwa madarakani walikuwa wanaangalia matumbo yao zaidi na si maslahi ya walipa kodi.



Mfano hai waliostaafu A. Jumbe, A.Mwinyi, B. Mkapa, Salim A Salim,Sumaye, Msuya, Warioba, Malecela etc. Napunde tu fisadi papa naye atastaafu wakati anawalinda mafisadi wenzake pamoja na anayejiita mototo wa mkulima ambaye hana huruma na walipa kodi wa nchi hii. Wote hawa kwa njia moja au nyingine wana biashara kubwa kwenye makampuni binafsi mfano simu za mkononi, Barrick Gold ambako fisadi papa ameshamiri, anajenga hekalu kama Mugabe alivyofanya kule Zimbabwe au Gadafi alivyokuwa anafuja mali za Libyans. Mkapa Bank M pamoja na wizi wa Kiwira bila kusahau biashara alizokuwa anafanya wakati yuko madarakani.

Tamaa yao ya pesa za walipa kodi ambao hawawezi hata ku-afford one meal a day, huu ni unyonyaji wa damu ya walipa kodi, wamevimbiwa lakini bado hawatosheki. Ni jukumu la kila Mtanzania kuona keki ya taifa inainua uchumi wa nchi hii na sio makundi ya mafisadi tu. Lazima shinikizo liwekwe kubadili sheria hii ya kuwalipa ambayo ipo kwa muda mrefu na imepitwa na wakati.

Pili

Wageni ambao wapoTanzania kwa ajira ni lazima waanze kulipa kodi kwa sababu hatuna shida ya wataalam kivile kama ilivyokuwa wakati tunapata uhuru. kama hawataki waondoke.

Makampuni yao yanaweza kuwalipia vinginevyo watafute wazawa sio lazima wakae au wafanye kazi Tanzania. Hatuwezi kuwa na kundi ambalo wanatumia ulaghai na sheria zilizopitwa na wakati kuja kupata mishahara mikubwa na minono ambayo haina kodi kwa kutegemea ubavu wa walipa kodi.

Wafanyakazi wengi wazawa wanalipwa fedha kidogo wanalipa kodi iweje wageni wengi wanasamehewa kwa kisingizio cha mikataba mibovu? Umefika wakati kupinga sera hizi za kifisadi. Nchi zote zilizoendelea hazina huu upuuzi wa tax holiday au kutolipa kodi kutoka kwenye mapato ya kila mwezi kwa raia wa kigeni.


Kama expert analipwa zaidi ya USD 100,000.00 kwa mwaka na halipi hata senti moja kwenye kodi inakuwaje anaendelea kuvuta hewa kwenye nchi yetu na kufaidi matunda ya walipa kodi wa nchi hii? Wakati vile vile umefika kwa Idara ya uhamiaji kuoanisha extension za permit na kodi ambazo mfanyakazi wa kigeni amelipa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom