Wakati nchi moja barani Afrika ikizundua Mtambo wake wa Mawasiliano kusoma Meseji za Watu Rwanda wao waja Kivingine!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,554
108,895
Huku nchi moja barani Afrika ( jina nimeisahau nikikumbuka nitaitaja ) ikiwa si muda mrefu tu imetoka Kuzindua ' mfumo ' wake wa Kimawasiliano ukiwa na lengo Kuu la ' Kuchungulia ' meseji za Raia wake na ' Kuwadhibiti ' Watumiaji wake wawe wanaandika tu Habari za Kusifu na Kupamba hatimaye nchi ya Rwanda yaja Kivingine na huenda hili likawa ni ' Funzo ' kwa hiyo nchi niliyoisahau jina.

Ni kwamba Mwezi ujao ( namaanisha February 2019 ) nchi ya Rwanda itakuwa ni ' Mwenyeji ' wa ' Kongamano ' kubwa la Masuala mazima ya Teknolojia na Mawasiliano litakalowakutanisha ' Wadau ' mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani huku lengo Kuu likiwa siyo ' Kuchungulia ' Meseji za Watu bali ni kuwasaidia Wananchi Wao kutumia Teknolojia na Mawasiliano katika Kudumisha Ufahamu, Bishara, Elimu na pia kutoa Uhuru wa Kutosha kwa Wananchi katika Kuzikosoa nchi zao lakini pia kudumisha ' Demokrasia ' katika nchi zao.

Wakati katika hiyo nchi niliyoisahau Jina Wageni waalikwa walikuwa ni 700 ambao kati ya hao 658 hawana ' Utaalam ' wowote bali walialikwa tu ili wakasifu na kushangilia kisha baadae wakalishwe ' Pilau ' la bure na wapewe Tsh 5,000/ kama Nauli na asante yao ya Kupoteza muda wao walipoalikwa, wakati kwa Rwanda Wageni waalikwa wa hilo ' Kongamano ' kubwa ni 400 ambapo wote hao ni Wataalam ( Experts ) tena wakubwa sana duniani katika masuala mazima ya Teknolojia na Mawasiliano.

Ni vyema hiyo nchi niliyoisahau Jina ikajifunza zaidi mambo mengi ya Kimaendeleo kutoka kwa nchi ndogo tu ya Rwanda yenye ' Ubarikio ' wa Watu wenye ' akili ' zinazowakaribia ' Wayahudi ' ili basi iweze kuendesha mambo yake. Teknolojia na Mawasiliano yawe ni ' chachu ' ya Kimaendeleo katika nchi na siyo ' adhabu ' kwa Wananchi kwa kuanza ' Kuwadhibiti ' na ' Kuchungulia ' hovyo Meseji zao na Wapenzi Wao au kama kutaka ' Kuwakomoa ' vile.

Akhsanteni Rwanda
Mungu ibariki Rwanda
Mwenyezi Mungu mbariki GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE

Nawasilisha.

Kwa wale watakaotaka Kusoma zaidi hasa juu ya hilo ' Kongamano ' Kubwa linaloandaliwa na Rwanda na litakalofanyika Mwezi ujao nendeni moja kwa moja katika Mtandao wa Habari wa CNBC Africa tafadhali.
 
Kwa hyo unataka nchi isizindue huo mtambo.
una lalamika kusoma meseji hujui zitasomwa meseji zote hata ambazo zinataka kuhatarisha usalama wetu kama nchi?

Mnapenda case study iwe Rwanda baadae mnalala mika
 
Ni Tanzania mkuu msiwe waoga kusema ukweli penye ukweli na usemwe.....
 
Ngoja Nikaoe Rwanda labda naweza kupata uraia huko, hili li nchi linaelekea kuzama muda si mrefu.

Hapana Mkuu tayari tumeshasitisha rasmi utoaji wa Uraia kwa Wageni halafu hata hivyo Siku hizi pia Rwanda tumeweka utaratibu mpya wa kuwataka Wanawake wetu waolewe tu na Wanaume Vipanga / Werevu ( very Intelligent ) ili ule ' Uhalisia ' wetu wa Kinyarwanda hasa wa ' Kitutsi ' usipotee hivyo sina uhakika sana kama nchi unayotokea Wewe huwa mna Watu wenye ' akili ' sana mpaka tukuruhusu Uoe Rwanda.

Kwa Tanzania Makabila ambayo tumewarusu Wanawake wetu ' Waolewe ' nao ni haya tu pekee kwakuwa tumegundua kuwa ndiyo yana uwezo mkubwa wa ' Akili ' ama unaokaribia au unaofanana na Wanyarwanda ila Makabila mengine ambayo hutoyaona hapa nikiyaorodhesha ' wasisumbuke ' kuja Kuoa Wanawake wa Kinyarwanda:

1. Wazanaki ( Mara )
2. Wahaya ( Kagera )
3. Waha ( Kigoma )
4. Wanyiramba ( Singida )
5. Warangi ( Kondoa, Dodoma )
6. Wangoni ( Ruvuma )
7. Wahehe ( Iringa )
8. Wanyakyusa ( Mbeya )
9. Wamakuwa ( Mtwara )
10. Wamaasai ( Arusha )
11. Wapare ( Kilimanjaro )

Kama Kabila lako halipo hapo au sijalitaja hapo juu usipoteze muda wako kutaka Kuoa Wanawake ' Majiniasi ' wa Kinyarwanda.
 
Hivi kwa akili yako unaamini toka uanze kutumia simu, simu yako au meaeji zako hazirekodiwi?
Hii kweli akili ya kihutu.
 
Kwa hyo unataka nchi isizindue huo mtambo.
una lalamika kusoma meseji hujui zitasomwa meseji zote hata ambazo zinataka kuhatarisha usalama wetu kama nchi?

Mnapenda case study iwe Rwanda baadae mnalala mika

Unaizungumzia nchi gani labda hapa Mkuu? Manake sikuelewi kwani Mimi mwenyewe hiyo nchi nimeisahau na siikumbuki kabisa ila nashangaa Wewe mwenzangu unaijua. Kwani kuitumia nchi ya Rwanda kama ' Case Study ' katika Maendeleo ni dhambi au mwiko hasa Kitaaluma? Hata tunapokuwa Darasani huwa tunashauriwa kuwa karibu na kushirikiana na wale Wanafunzi Werevu ( wenye akili ) ili watusaidie na Sisi wengine kujua jinsi ya ' Kufikiri ' kama Wao hivyo sioni tatizo sana sana naona umeandika ' Upuuzi ' tu hapa.
 
Ni Tanzania mkuu msiwe waoga kusema ukweli penye ukweli na usemwe.....

Bado naendelea Kuikumbuka hiyo nchi na mpaka sasa bado sijaikumbuka hata hivyo nikiikumbuka hapo baadae nitaitaja. Ila sina uhakika wa 100% kama hii nchi yako uliyoitaja hapa ndiyo yenyewe halafu hata sina taarifa kama hiyo nchi imefanya Jambo lolote la Kihabari labda Wewe unihabarishe zaidi Mkuu.
 
Hapana Mkuu tayari tumeshasitisha rasmi utoaji wa Uraia kwa Wageni halafu hata hivyo Siku hizi pia Rwanda tumeweka utaratibu mpya wa kuwataka Wanawake wetu waolewe tu na Wanaume Vipanga / Werevu ( very Intelligent ) ili ule ' Uhalisia ' wetu wa Kinyarwanda hasa wa ' Kitutsi ' usipotee hivyo sina uhakika sana kama nchi unayotokea Wewe huwa mna Watu wenye ' akili ' sana mpaka tukuruhusu Uoe Rwanda.

Kwa Tanzania Makabila ambayo tumewarusu Wanawake wetu ' Waolewe ' nao ni haya tu pekee kwakuwa tumegundua kuwa ndiyo yana uwezo mkubwa wa ' Akili ' ama unaokaribia au unaofanana na Wanyarwanda ila Makabila mengine ambayo hutoyaona hapa nikiyaorodhesha ' wasisumbuke ' kuja Kuoa Wanawake wa Kinyarwanda:

1. Wazanaki ( Mara )
2. Wahaya ( Kagera )
3. Waha ( Kigoma )
4. Wanyiramba ( Singida )
5. Warangi ( Kondoa, Dodoma )
6. Wangoni ( Ruvuma )
7. Wahehe ( Iringa )
8. Wanyakyusa ( Mbeya )
9. Wamakuwa ( Mtwara )
10. Wamaasai ( Arusha )
11. Wapare ( Kilimanjaro )

Kama Kabila lako halipo hapo au sijalitaja hapo juu usipoteze muda wako kutaka Kuoa Wanawake ' Majiniasi ' wa Kinyarwanda.
Mkuu hapo kwenye makabila umetusahau WASUKUMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom