Wakati Mwingine unatamani kusikia Magazeti yetu yakiwa na vichwa vya habari zifuatazo

Bora huyu aloota ndoto yake kuliko nyie mnaoquote Uzi mzima.... Yaani nyie ni sawa na bashite tu.. Unakuta jitu linaquote Uzi mzima kana kwamba wachangiaj wengine hawajausoma!!
 
Nimeipenda hiyo ya "Kuingia kwe mgogoro na jumuiya ya kimataifa kwa kutengeneza silaha za nyuklia", huku serikali ikisisitiza kuwa ni kwa ajili ya nishati ya umeme tu...

...Bado tuna safari ndefu kufika huko, kama tumekuwa watu wa kumsikiliza "mange kimambi" toka marikani, na habari "ujinga" wake una trend kuliko habari yoyote ndani ya nchi, ana fans malaki huko insta, haya njoo kuyaandika in the next 500yrs.
 

Tunavyopenda hivi umbeya, habari za Maki tutamwachia nani!?
 
 
mm ningependa kuskia haya.

Chato yawa Mkoa Rasmi.

Bashite atumbuliwa na kuamuwa kurudi shule.

Rais Magufuli atoswa na CCM kugombea URais 2020.

kwa Mara ya Kwanza Upinzani Washinda Uchaguzi mkuu.

Tanzania yajenga barabara 10 Ubungo Chalinge
nimeipenda ya 3
 
Ukiachilia mbali wananchi wanaopenda kula Ubuyu daily, Je viongozi wenye dhamana katika maeneo husika wamewekeza kiasi cha resource ili tufikie hatua hiyo ?

So far viongozi tulionao wamejikita kwenye udaku na vijembe wakiongozwa na Dr Yohana mwenyewe.
 
College of engineering UDSM wafanikiwa kujenga daraja nimeipenda hyo sasa sijui lini
 
Mawazo yako mazuri, ila kwa kwa Tanzania ya sasa tunavutia sana na habari zinazoongelea maovu ya wenzentu
Nchini Marekani wabunge wa Republican wameungana na Wa Democratic kumpinga mteuliwa wa bwana Trump kutokana kashfa aliyonayo.

Je unataka kutumbia wamewaiga nyinyi watanzani ?
 
Mkuu huoni kama akina bashite wakipotea hayo yote yanawezekana.? Tuwadhibiti hawa akina bashite ktk elimu zetu na uongozi matokeo hayo unayowaza yatafanyika.
 
Yaaani uongozwe na bashite ufikie maendeleo hayooo????tupambane na ubashilism kwanza
 
Si rahisi, koromije ndio shida

 
Tatizo Mkuu ni huu uongozi uchwara uliopo nchini ambao kila kukicha wanaendelea kukumbatia maovu mbali mbali nchini na watenda maovu.

Angalia ndani ya nchi yetu hata kujadili njaa sasa ni kosa la kumpeleka Mtanzania lupango. Angalia hili la Bashite zaidi ya wiki sasa Rais aliyepigia debe uhakiki wa vyeti vya watumishi wa Serikali hili anaendelea kuuchuna kama hajalisikia kabisa. Angalia la Wabunge wa MACCM kupokea rushwa ya milioni 10 Majaliwa kakubali kuuficha ukweli kuhusu huu ufisadi uliofanyika pale mtaa wa lumumba na Rais naye kimyaaa!

Kwa hiyo utaona Serikali ndiyo iko mstari wa mbele kukumbatia maovu na watenda maovu na hivyo hii hali kusambaa nchi nzima na hata kuanza kuathiri elimu yetu kwa kiwango cha kutisha.

Ikiwa hali halisi ndiyo hii hayo ambayo wengi tungependa kuyasoma na kuyasikia yatabaki kuwa ndoto kwa mingi ijayo.

Leo hii kukemea maovu nchini unaonekana ati ni MCHOCHEZI!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…