Wakati jirani anaunda "AntiCounterfeit Agency" sisi tunatakiwa tufanye nini??


M

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
1,693
Likes
174
Points
160
M

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
1,693 174 160
Jana katika taarifa za habari nimeona wenzetu Kenya wameunda Anti-Counterfeit Agency taasisi ambayo itafanya kazi kwa uhuru zaidi bila kutegemea KBS (ya kwetu ni TBS).
Maana yake ni nini? Watazuia bidhaa zote feki kuingia au/na kuuzwa nchni mwao. Na hawa watu siku hizi wanafanya mambo yao kuwa kweli. Kilichoniogopesha na kunishangaza zaidi ni pale mtaalam mmoja aliposimulia kuwa kuna dawa feki za malaria ambazo mgonjwa akimeza huwa zinakwama tumboni na kusababisha madhara kiasi cha kupelekea mgonjwa kupasuliwa. Huenda kwetu zimeshafika ila bado TBS na wataalam ie. Mkemia Mkuu wetu na watu hawajazigundua au kuzishtukia?

Cha muhimu zaidi kuliko vyote ni kuitaka serikali yetu kuwa macho sana eidha ichukue tahadhari stahili mapema maana hizo bidhaa zitakazozuiliwa kuuzwa Kenya zitapitishwa njia za panya na kuingia Tanzania kwa wingi sana. Itakuwa aibu Tanzania kufanywa a dumping place ya jirani zetu.
Nawasilisha!
 

Forum statistics

Threads 1,236,946
Members 475,327
Posts 29,274,022