Wakati Acacia ikifungasha virago, tukumbushane mambo ya kijinga tuliyokuwa tunafanya mgodini

Zungumzia na makinikia kidogo tupate kuyafahamu
Kuhusu makinikia

Uchenjuaji wa dhahabu hapo buly huusisha madini ya Copper; haya huwa yana sifa ya kutumia Cyanide ( chemikali inayonasa dhahabu) kwa haraka zaidi kuliko dhahabu yenyewe. Hivyo Hiyo Shaba hutolewa mapema ktk process iitwayo flotation. Utoaji huu mzigo wake ndo unaitwa Makinikia ndani yake kuna madini Copper; dhahabu ; Silver; Lead ; Zinc ; Iron na madini mengine kwa kiasi tofauti tofauti.

Mabaki yanyotokana na uchenjuaji huu humaliziwa kwa process ijulikanayo kama CIL Hapo ndo huja kupatikana vitofali ambavyo ilikuwa mara nyingi alhamisi vinarushwa n helkopter
 
c8f9534bd8e9f913482f120db2032fc1.jpg
mtu wa watu
Jamaa muungwana sijapata ona hakika.....
 
hapo kwa jamaa kufyala chakula cha emergence ni balaa.Ila hakuna bimaadamu anakua kiumri aisee inategemea tu yuko na nani.

Kuna mtu ananiambia alikuwa akisuuza galon kwa diesel kuondoa oil,nusu galon kisha anatikisa anamwaga.awakomoe makaburu.

Hiyo ya jamaa 4 kufukiwa na mwamba na kufa vibaya ilisababisha karibia nusu ya miners kuomba kuacha kazi,mpaka makaburu wakaanza kubembeleza.

Sema tufupi mno,embu refusha basi atleast tukisoma tufurahi zaidi.
Najitahidi kiongozi lkn ni vizuri muulize nanyi maswali ili niwe nawajibu kwa sehemu ambayo hamkuelewa au mahitaji kufahamu zaidi.
 
Part III lini mkuu
Bado natafakali maana ndiyo itakuwa ya mwisho, naomba niwaulize katika party III kama mtakuwa na maswali ili niwasaidie kuwapatia jibu. Nashukuru hapa nimepata ma retired miners na ma miners wezangu ambao tutasaidiana nao kuwapa elimu. Narudia tena, maisha ya underground mining ni zaidi ya maisha ya jeshi, paipu ya upepo ikipasuka inaweza pia kukuua kabisa.
jiwedogo
 
Huo ndio ukweli hawawezi kufanya hyo,kazi wamesanda Tulawaka, wabongo wababaishaji wanaweza kuchimba maduara na kufunga matimba mashine kubwa kwao ni moko.
Mgodi wa Bulyanhulu miners wakitoka hapo na kwenda nje ya nchi wanapokelewa kama ma expert na wataalamu. Mgodi unaoweza kutembea na gari (LV) spidi ya 80km/hr chini ya ardhi
 
Bado natafakali maana ndiyo itakuwa ya mwisho, naomba niwaulize katika party III kama mtakuwa na maswali ili niwasaidie kuwapatia jibu. Nashukuru hapa nimepata ma retired miners na ma miners wezangu ambao tutasaidiana nao kuwapa elimu. Narudia tena, maisha ya underground mining ni zaidi ya maisha ya jeshi, paipu ya upepo ikipasuka inaweza pia kukuua kabisa.
jiwedogo
Duhhh.....
Umenikumbusha tukio la mbali kidogo mkuu...
Mwaka 2000 kama sijasahau, nakumbuka kuna jamaa flani mchaga aliwahi kupata ajali wakati wa uchimbaji wa main shaft, kutokana na pipe ya upepo.
Kwa kawaida baada ya kulipua mwamba, kuna timu ya watu kama 8-12 walikua wakishuka kuhakikisha kama baruti zote zilizo tegeshwa zimelipuka na wakati huo pia walikua wakishuka kule shimoni ili waangushe miamba ilio legea ili pawe salama kwa timu nyingine iliofuata kwaajili ya kutoa kifusi cha mawe pamoja na kazi zingine.
Sasa yale mawe legevu yalikua yakiangushwa kwa kutumia upepo, na pipe hiyo ya upepo ilikua ikishikiliwa na watu wasiopungua 8.
Sikumoja ilitokea ile pipe ikawaponyoka jamaa walio ishikilia na mmoja wa washika pipe alipitiwa na upepo wa ile pipe na kusambaza koo, meno na fizi kabla ya koki ya pipe haijafungwa.
Duhhh......
Naikumbuka sana hii ajali ilikua mbaya sana, ingawa jamaa alipelekwa south Africa kwa matibabu na akapona, lakini jamaa alirejea akiwa amebadilika sura kabisaaaaaaaa
 
Part III lini mkuu
PART III NITAONGEZEA NAMNA TULIVYOKUWA TUNACHENJUA DHAHABU CHINI HUKO ILI TUTOTE KIMAISHA PASIPO MAFANIKIO KUTOKANA NA NATURE YA DHAHABU YA BULYANHULU, PIA TAONGELEA KWA UJUMLA KAMA NILIVYOAHIDI KTK PART II NAMNA DHAHABU NA USHIRIKINA VINAVYOENDANA Kumbuka nimezaliwa usukumani kipindi mgodi huu unaitwa Bariadi nilikuwa tayari nina akili pevu, MJI WA KAKOLA NA LIFE STYLE YAKE, MAAMBUKIZO YA MAGOJWA YA DHINAA NA UKIMWI hasa Kakola yenyewe, Bugarama, Ilogi, Kahama na Geita. Then taanza kujibu maswali na kumaliza
 
Bado natafakali maana ndiyo itakuwa ya mwisho, naomba niwaulize katika party III kama mtakuwa na maswali ili niwasaidie kuwapatia jibu. Nashukuru hapa nimepata ma retired miners na ma miners wezangu ambao tutasaidiana nao kuwapa elimu. Narudia tena, maisha ya underground mining ni zaidi ya maisha ya jeshi, paipu ya upepo ikipasuka inaweza pia kukuua kabisa.
jiwedogo
Mkuu isiwe ya mwisho mi navojua kuna vitu vingi vitawainspire wanaotaka waende huko

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu isiwe ya mwisho mi navojua kuna vitu vingi vitawainspire wanaotaka waende huko

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
Nafahamu ni mambo mengi sana, Nilitaka nielezee namna Makaburu walivyo wabaguzi na namna wanaletana huku wengine hawajui kazi yoyote na walivyo na akili, akimleta ndugu yake ambaye hajui chochote basi anapangiwa shift ya usiku ili awe anajifunza kupitia ma black Watanzania wezangu huku akilipwa mshahara mkuuubwa!!! KUMBUKA USIKU WALE MA BOSS WAKUBWA WA MGODI HUWA WAMELALA NA WAKE ZAO so inakuwa ngumu sana kumtambua kaburu mzungaji chini,( kuna kaburu mmoja alikuwa anajipaka matope wakati wa mwisho wa shift ili akitoka shimoni aonwe na wazungu wezake kuwa alikuwa amepindika kweli kweli) Namna wazungu wa Kiastralia walivyo wakarimu na namna Watanzania wezetu waliopewa mamlaka makubwa mgodini walivyokuwa wanawanyanyasa Watanzania wezao kisa tu umsujudie au una bifu nae la nje ya kazi. Mambo ni mengi sana.....
 
Mwembe maua sio mwembe giza. Hilo sitalizungumzia mkuu ila ukweli ndo huo ni sehemu ya sadaka ya damu kama mgodi ulivyo kila mwisho wa mwaka au baada ya mwaka mpya (Naomba nisiulizwe maswali katika hili maana liko ki imani zaidi)

Sawa kabisa mkuu ni mwembe maua
 
Ni kweli mkuu muda mwingine nakuwa na kazi za kuhudumia watu na pia kuweka kumbukumbu, kumbuka haya nayatoa kichwani kwa kukumbuka zaidi ya miaka sita iliyopita nikiwa nafanya kazi hapo Bulyanhulu
Aisee nilisotea kazi za migodini ikiwemo ggm, buzwagwi (acacia) na nyamongo lakini sikuwahi kutuma wala kuwaza kupeleka barua yangu bulyagh'ulu kwa kuwa tu ule mgodi ni underground ukikutana na walio kuwa wanafanya kazi huko story wanazokupa zinatisha kidogo japo walikuwa na packages nzuri kwenye baadhi ya vitengo sikuthubutu hata kidogo.

Hongera sana kwa kufanya kazi bulyaghulu na kutoka salama na leo unatupatia story, endelea kutudadavulia ili tupate kuelewa na kujifunza baadhi ya mambo ya underground mining.
 
Back
Top Bottom