illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Kwa watumishi wa serikali huwa tunaamini kwamba wenzetu wanaofanya kazi kwenye agencies wana mishahara mikubwa kuliko local na central gvmnt,zipo agencies nyingi ambazo binafsi sioni wakitekeleza majukumu yao ipasavyo.
Juzi nilikuwa nahitaji mbao kwa ajili ya kuezekea kibanda cha mzee wangu nikatembelea maeneo ya Buguruni Tazara ambayo ndiyo maarufu kwa kuuza mbao za kupaua nilikuta mbao zinauzwa 4 by 2 kwa shilingi elfu moja kwa futi.
Nilihitaji mbao themanini wahusika wakaanza kushusha mbao moja moja na kupima, nikawaomba tutumie futi tofauti baada ya kuona hali ya sintofahamu kwenye futi waliyokuwa wanatumia, hivyo nikanunua futi katika duka la jirani ambapo niligundua tofauti ya futi moja hadi moja na nusu kwa kila mbao ya futi ishirini na kuendelea. Jamaa walipoona nimekuwa makini walikataa kuniuzia na kusema niende sehemu nyingine, nimezunguka sehemu kama nne tofauti nimegundua kasoro zilezile.
Ndipo jamaa mmoja akasema hapa huna ujanja itabidi ukubaliane na vipimo vyao kama kweli unataka mbao kwani wote ndivyo wafanyavyo, akanielekeza kwamba huwa wana kata futi na kuiunga sehemu katikati na wewe huwezi kupata muda wa kukagua, kuna maofisa wanalipwa mshahara wanapigwa na kiyoyozi wakati walipa kodi tunaumizwa.