Wakala wa benki alinifanya niishi katika lindi la ufukara, sasa zamu yake

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,765
36,354
Habari!

Nitasimulia kwa ufupi kisa hiki kisichosisimua ila kinafundisha.

Mwaka 2016 nilitembelewa na huyu wakala wa benki kazini. Akanishawishi nikakopa pesa kwa mara ya kwanza. Niliikopa pesa kwaajili ya kujiendeleza kielimu na nyingine nifungue biashara. Bahati mbaya sikujaza vizuri ikapelekea kutokuchaguliwaa University. Nikajaza vizuri nikachaguliwa second batch.

Wakati nasibiria second selection pesa ya shule nikaamua ninunulie kiwanja.

Na nyingine nikafungulia duka.

Due to poor management na ubize wa kazi duka likanishinda.

Benki nadaiwa life limeanza kuchange. Siku moja nikaonana naye akanishawishi nifanye top up. Sasa ile nimefanya top up najua kabisa napata kiasi fulani kesho nawekewa pesa ananiambia kuwa nitapata kiasi fulani tofauti na nilivyojaza(nahisi walimibadilishia form).

Pesa ikaingia nayeye anataka ya ganji kana kwamba Mimi ndiye mwajiri wake. Nikaona isiwe tabu nikamtoa. Ile salary slip ya mwezi uliofuata nikicheki naona deni limekuwa kubwa zaidi. Nikamcheki nikaenda kwa meneja wake tukalonga bado majibu hayajajitosheleza.

Nikawaambia nakwenda mahakamani kufungua kesi. Huyu wakala akasema nenda. Nikawaza nikaona tapoteza muda.

Nikaishi kigumu Mungu akanifungulia milango mingine sikutetereka, nikasimama, nikajenga, nikafungua business na kufanya mambo mengine.

Mwaka huu akaja job kachoka mpaka nauli ya daladala anagongea.

Nikaahidi kumsaidia kifedha au kumshika mkono aajiriwe kazini kwetu. Baadaye nikakumbuka hujuma zake nikakaushia. Sasa hata kunitafuta anaona aibu.

Funzo: Kila nafasi unayoipata watedee watu kwa haki na upendo.
 
Malipo yapo hapa hapa, kama moyo wako unakataa kumpa ajira kwako mwache usije juta baadaye, kama una amani ya moyo mpe kazi, ila kumbuka fisi ni fisi tu na mbuzi ni mbuzi!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Kweli ndugu.

Ni heri mtu umsaidie apate kazi sehemu nyingine.

Akigeuka mwiba kazini mko wote inauma sana
 
Kama kazi yenu ina security hauwezi kutoka kwa fitna za mtu mmoja, msaidie apate kazi

Ila kama ni zile kazi unaondolewa kwa neno la mtu mmoja achana nae
 
Kweli ndugu.

Ni heri mtu umsaidie apate kazi sehemu nyingine.

Akigeuka mwiba kazini mko wote inauma sana
Unajua tabia nikama ngozi, ukute hapo baada ya kumfanyia huyu alifanya yakufanya kwa watu wengine kisha akatimuliwa, hivyo aangalie moyo wake unasemaje bila kujilazimisha!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom