Maserati
JF-Expert Member
- Jun 15, 2014
- 11,602
- 20,098
Habari za siku mingi bhandugu zangu wa Jf...leo nakuja na mada kama ilivyo ainishwa hapo juu. moja kwa moja niende kwwnye mada,Kudate na mtu wa chuo ni headache hasa chuo kimoja ndo majangaaaa. Utakuta enzi za mapenzi yenu mtataka kila rafiki ajue uhusiano wenu, kwa vile tu mnavyopendana. Na watu wanasema mapenzi upofu basi aagha! wenyewe mnajiachia japokuwa ni private issue sasa inakuwa public matter yaani kila mtu atajua. Hayo nane, tisa mgombane, yallabi! Joto la dar haliingii ndani, mna ha ha kama mmekosa maji ya kunywa siku mbili, kisa mmegombana.
Eti unaanza kusumbua wenzako darasani na hostel kwenu yaani kujiliza liza, mara sijisikii hamu ya kula wala sijisikii hamu ya kitu chochote, muongo mkubwa wewe. Unajisikia sana, na baadae ndo utawasikia eti ooh! Njaa inaniuma sana siku nzima sikula jana, ulitumwa?kujitesa bure. Hilo tisa, kumi muachane sasa mamaa weee! Mtoto wa kike hapo ndo analia eti "ooh,kaniumiza... kanipotezea muda wangu...kumpenda kote kule.na utasikia wanasema "wanaume hawaridhiki sijui hawatosheki" na wakaka wazima nao wanavyokosa aibu hadi kulia mnalia siku hizi, mxiuuu. Chefuu, utasikia "ooh! Mm nilimpa kila alichokitaka, sasa sijui kwann kaniacha. Mara ooh! Kaniumiza sana, mara ooh nilimpenda sana...nikampa moyo wangu wote. Na wao utawasikia "wanawake hawatosheki" utampaje mwenzio moyo wakati umefichwa ndani ya kifua chako? Huna hata alama ya mshono ujikute umempa mwenzio moyo wako wote. Acheni ulimbukeni wadada kwa wakaka, na hili liwahusu hata nyie wa mitaani, ambao hamuendi mbali yaani mtaani hapo hapo. Kujipa shida na vijiba vya roho tu.
Mfate lilichowapeleka, na kama ni mapenzi basi mjue hapo ndio mwanzo wa kumtafuta mtu wa maisha coz wotw mtakuwa mmesoma, lakini wa sasa mlivyo. Still mnaleta mambo ya kitoto wakati ni watu wazima nyie. Na nina imani asilimiaa kubwa ya mnaoingia vyuoni ni above eighteen na wengi wenu mshatoka kwenye u teenager but akili zenu sijui hazija komaa bado...au sijui kujitambua zero. Eti amenitumia tu ameniacha, si ulitaka mwenyewe. Sasa unamlalamikia nani?? Kwani mlivyoanza mahusiano hamkujua kama mtatumiana ipasavyo? Ndo mkome sasa. Na iwe fundisho kwetu vijana, tusikurupuke kuingia katika mahusiano bila kumfahamu ipasavyo. Na wengi siku hizi mahusiano yao hayadumu kwasababu ya kuwa na watu ambao hamuendani kitabi wala ki life style ya maisha.
Mjipange, la sivyo mtaumizwa sana. Poleni.