Wajuzi wa mita za LUKU piteni hapa

Wajuzi wa mita za LUKU piteni hapa

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
wataalam wa hizi mita hebu nipeni uzoefu wenu wa namna navyoweza kuikwepa ile kodi ya mwezi wenyewe wanaita service charge ambayo kwa sasa ni kama elf sita na upuuzi.
Kuna mtu hapa ananambia kuwa eti ukinunua katikati ya mwezi unapata umeme mwingi na haukatwi hii kitu je kuna ukweli katika hili?
Hebu tushauriane hapa namna tunavyoweza kufanya kupunguza hizi gharama
 
Yaani hata ukinunua umeme wa mwaka mzima, system inakuwekea deni lako miezi yote ambayo hukulipa, so ukirudi tuu lazma ulipe kwanza deni la service charge then ndo upate umeme.
 
Sio kweli hata ukinunua leo umeme wa miaka kumi siku ukiisha ukinunua watakata service charge za miezi yote ya miaka kumi yani miezi 120.., service charge ni kila mwezi...

Kupunguza gharama ni kupunguza matumizi tu (kama kutumia energy saver kwenye taa n.k.), pia angalia kama unatumia chini ya units 75 kwa mwezi kila mwezi basi waambie tanesco wakubadilishie tariff utalipa tshs 100 tu kwa unit na hautalipa service charge
 
Hata ukinunua units za kutumia miezi 6,siku utakayo nunua lazima ulipe charges za miezi yote.Kifupi charges hazikwepeki....
 
thanx wakuu nimewapata vyema hapa dawa ni kuwaibukia tanesco wanibadilishie tarrif tu manake sifikishi unit sabini kwa mwezi naishi mwenyewe tu hivyo control ya umeme ni kubwa sn kwangu
 
Sio kweli hata ukinunua leo umeme wa miaka kumi siku ukiisha ukinunua watakata service charge za miezi yote ya miaka kumi yani miezi 120.., service charge ni kila mwezi...

Kupunguza gharama ni kupunguza matumizi tu (kama kutumia energy saver kwenye taa n.k.), pia angalia kama unatumia chini ya units 75 kwa mwezi kila mwezi basi waambie tanesco wakubadilishie tariff utalipa tshs 100 tu kwa unit na hautalipa service charge

Hee kumbe ni 75 mimi nilifikiri 50 ngoja niwaibukie ila kusema la ukweli umeme tanzania unatuumiza sana waliotembelea nchi za wenzetu hembu tuambieni kama umeme wao ni wamawazo kama hapa kwetu yaani sijui nihamie libya.
 
VP naweza kuichakachua
Chakachua hiyo meter at your risk, kwa kuwa hao TANESCO walivyo na usongo na hao 'vibaka' wadogo wadogo wa umeme, wakigundua, siyo tu afhabu yao, watanyofoa hiyo mita na kuirudisha 'kwao' bali pia watakutoza faini, hadi 5 million Tshs!

Lakini cha ajabu watanzania, tunavyoibiwa mabilioni na makampuni ya nje, kama vile Symbion, IPTL na Aggreko, wao TANESCO wanajifanya, wamejipa upofu wa kudumu, kiasi ambacho, wanajifanya hawauoni 'ujambazi' huo tunaofanyiwa watanzania!
 
Back
Top Bottom