Wajuvi wa mambo mtusaidie: Nini mapungufu ya Mikataba ya Madini?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,728
Tumechoka kusikia imesainiwa hotelini?
Tunaibiwa madini- hapa tume ya kitaalam imetuonyesha...
Je Tulichoonyeshwa ndio kilichokuwa kimefichwa kwenye mikataba?
Je mikataba kuwa siri ndio Kigezo cha kuhisi mikataba inamapungufu?

Katika tafakari ya kizalendo, hadi sasa sijui nini kilikosewa kwenye hiyo mikataba zaidi ya kusikia kelele na vilio vya wazalendo kuwa tunaibiwa kwa sababu mikataba ilikosewa Bila kuambiwa imekosewaje na nini kifanyike kuiweka iwe Sawa...

Angalau sasa tumepata mwanga tuliibiwaje japo mtuhumiwa nae anabisha lkn hili la mikataba bado hisia zimetanda kwa ukubwa kuliko facts...
 
Umewaza mbali sana,kweli inabidi tujue hiyo hujuma iko kwenye nn na tulipaswa kupataje?
Wajuzi wa mambo inabidi watufafanulie hapa.
 
Huwa tunatumia vigezo gani kusema mikataba ndio imetufikisha hapa au mikataba ikirekebishwa tutafaidi.
Hapa nadhani wakina lisu wanatakiwa watusaidie zaidi...
Kuna mikataba watu wamepewa wachimbe madini miaka 99.
Kuna mikataba watu wameingia hakuna kutoa kodi mpaka arudishe hela yake.
Kuna mikataba wameingia 30% ya serikali 70% mwekezaji.
Miaka nenda rudi madini yanachimbwa hela haionekani.
Tanzanite ikitoka ikifika sauzi.inaenda kuandikwa made in south africa.
 
Hapo bado kunamagap na michanganyiko Mingi mkuu.
Inaonekana wote wa madini sio hawa wawili wanatakiwa kurudisha pesa yao kwanza ndio Walipe kodi 30%. Ndio maana tunalipwa hiyo 4% katika kipindi cha mpito.
Kama ni kweli kwa nini miaka nenda rudi migodi ipo pesa haionekani. Mfano tukiacha hii ya miaka ya 90/2000 mwadui almasi wapo kabla ya uhuru na bado hakuna kitu hadi kesho mwanya uko wapi hapo. Ni wakati wa kuyajua haya mambo katika mizizi yake..
 
Kuna mikataba 50/50 ya faida kati ya serikali na mwekezaji ila serikali hajatoa hata mia katika investment ya kuchimba hayo madini,
Unadhani mfanyabiashara atafanyaje hapa kama sio kupata hasara kila mwaka
Ni wakati sasa serikali ifanye investment yenyewee ili iwe na access na control ya madini kwa ukaribu zaidi
Hii ya kukaa wizarani afu unasubiria mfanyabiashara akuletee faida tutachora chini
 
Mkataba kuwa siri ushakuwa na mapungufu hata kama ni mzuri. Ni chaka la rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka. Hata Benki ya Dunia siku hizi wanahimiza mikataba kuwa wazi.Soma hapa.

Hata kama hatuibiwi, mikataba ikiwa ya siri, tutaona tunaibiwa.

Pia mikataba ya royalties za 3%-4% ni bora usichimbe madini.

Kipindi kirefu katika utawala wa Nyerere nilikuwa sielewi, kwa nini Tanzania ina madini mengi sana lakini Nyerere anakataa kuchimba madini? Migodi ilikuwa michache sana. Nikamuona Nyerere ni mnoko sana tu ana madini hataki kuchimba watu wapate maendeleo ya kiuchumi.

Baadaye baada ya hizi royalties za 3%-4% kujulikana ndipo nikajua kwamba yule Mzee alikataa kuchimba madini kwa sababu terms zenyewe zilikuwa zinatutukana akili zetu.

Bora tungacha kuchimba madini labda vizazi vijavyo vingeweza.

3%-45 royalty ni ujinga. Hata mimi nikienda dinner waiter akinihudumia vizuri kutoa tip ya 3%-4% siwezi, nitaona aibu.

Seuze watu wanaokuja kuchukua madini yenye thamani sana nchini mwetu?

Hapo ndipo utajua akili ni mali kuliko hizi resources, na hawa wageni hawana resources lakini kwa namna fulani wamewazidi viongozi wetu akili kwa kuwaendekeza ulafi wao.
 
Ndo maana tunatakiwa tuifunua mikataba yote
Japo chenge anapinga.
Saudia,dubai n.k.
Wanatumia mafuta tu lakini ni matajiri wa kutupwa.na sio kama hawana wawekezaji.
Wawekezaji wapo.
ila sheria zao ni kali lazma nchi inufaike sawa na mwekezaji

HAUTAKI WANA KWAMBIA SEPAAAA.NA HAWATANII.
 
Tumechoka kusikia imesainiwa hotelini?
Tunaibiwa madini- hapa tume ya kitaalam imetuonyesha...
Je Tulichoonyeshwa ndio kilichokuwa kimefichwa kwenye mikataba?
Je mikataba kuwa siri ndio Kigezo cha kuhisi mikataba inamapungufu?

Katika tafakari ya kizalendo, hadi sasa sijui nini kilikosewa kwenye hiyo mikataba zaidi ya kusikia kelele na vilio vya wazalendo kuwa tunaibiwa kwa sababu mikataba ilikosewa Bila kuambiwa imekosewaje na nini kifanyike kuiweka iwe Sawa...

Angalau sasa tumepata mwanga tuliibiwaje japo mtuhumiwa nae anabisha lkn hili la mikataba bado hisia zimetanda kwa ukubwa kuliko facts...
Hapa suala lisiishie kwenye mchanga tu inabidi mikataba yote ifumuliwe hii 4% mrahaba ni wizi mtupu. Nchi hii ni nchi ya ajabu kwani wakati wabunge walipokuwa wakiuuliza mikataba jibu ilikuwa mktaba ni siri leo watanzania ndio tunaona joto la usiri huo. Rais Magufuli ameonyesha dhamira yake hata kabla hajawa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Tusubiri zile kamati 2 zilizobaki zitoe ripoti ndipo tuone maumivu yote yaliyotupata.
 
Kuna mikataba 50/50 ya faida kati ya serikali na mwekezaji ila serikali hajatoa hata mia katika investment ya kuchimba hayo madini,
Unadhani mfanyabiashara atafanyaje hapa kama sio kupata hasara kila mwaka
Ni wakati sasa serikali ifanye investment yenyewee ili iwe na access na control ya madini kwa ukaribu zaidi
Hii ya kukaa wizarani afu unasubiria mfanyabiashara akuletee faida tutachora chini
Serikali imewekeza mgodi unaitwa stamigold lakn unasuasua na kuyumba balaa
 
Mkataba kuwa siri ushakuwa na mapungufu hata kama ni mzuri. Ni chaka la rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka. Hata Benki ya Dunia siku hizi wanahimiza mikataba kuwa wazi.Soma hapa.

Hata kama hatuibiwi, mikataba ikiwa ya siri, tutaona tunaibiwa.

Pia mikataba ya royalties za 3%-4% ni bora usichimbe madini.

Kipindi kirefu katika utawala wa Nyerere nilikuwa sielewi, kwa nini Tanzania ina madini mengi sana lakini Nyerere anakataa kuchimba madini? Migodi ilikuwa michache sana. Nikamuona Nyerere ni mnoko sana tu ana madini hataki kuchimba watu wapate maendeleo ya kiuchumi.

Baadaye baada ya hizi royalties za 3%-4% kujulikana ndipo nikajua kwamba yule Mzee alikataa kuchimba madini kwa sababu terms zenyewe zilikuwa zinatutukana akili zetu.

Bora tungacha kuchimba madini labda vizazi vijavyo vingeweza.

3%-45 royalty ni ujinga. Hata mimi nikienda dinner waiter akinihudumia vizuri kutoa tip ya 3%-4% siwezi, nitaona aibu.

Seuze watu wanaokuja kuchukua madini yenye thamani sana nchini mwetu?

Hapo ndipo utajua akili ni mali kuliko hizi resources, na hawa wageni hawana resources lakini kwa namna fulani wamewazidi viongozi wetu akili kwa kuwaendekeza ulafi wao.
Royality sio utaratibu wa Tanzania tu Bali ni dunia nzima mkuu na kwenye madini huwa hauzidi 5%.
Migodi inapewa unafuu wa kulipa Royality kama unafuu maana wanakuwa Wamewekeza matrillion na hawajaanza kurudisha hata nukta ya faida. Hata kama tungeacha hadi 2050 muwekezaji lazima angeanza na royalty ndio Walipe kodi otherwise na sisi tushiriki kuwekeza hata 40%. Au twende tukajifunze Botswana.....
Pili kwa nini Williamson diamond mining /mwadui wapo tangu enzi za nyerere hadi kesho lakni nao inasemekana hakuna chochote tunafaidi. Wakati ukoo wa Williamson unafaidi na kuwa mabillionea mkuu.
Tupe uzoefu maana wengine miaka hiyo hatukuwepo na reasoning zake zilikuwa nini hasa...

Nakubaliana na wewe transparency ya mikataba itasaidia kuondoa hofu tunaibiwa au hatuibiwi na nchi nyingi sasa kutokana na tatizo tulilonalo wameamua kuweka wazi na nusu wazi hasa mikataba ya madini na other natural resources....
 
Wandugu,

1. Nitaomba tuvumiliane. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.

ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.

ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.

iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?

vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.

FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA

11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.

Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) national framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) state-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.

Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.

Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye

resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana. Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.

Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.

MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.

SUALA LA MCHANGA WA MADINI

Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.

Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so. And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!

Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa?
KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.
 
Kuna mikataba watu wamepewa wachimbe madini miaka 99.
Kuna mikataba watu wameingia hakuna kutoa kodi mpaka arudishe hela yake.
Kuna mikataba wameingia 30% ya serikali 70% mwekezaji.
Miaka nenda rudi madini yanachimbwa hela haionekani.
Tanzanite ikitoka ikifika sauzi.inaenda kuandikwa made in south africa.
Mikataba ni siri. We we uliisoma wapi?
 
Kwanza si "roayality" ni royalty.

sio utaratibu wa Tanzania tu Bali ni dunia nzima mkuu na kwenye madini huwa hauzidi 5%.

Hilo ni jambo ninalolifahamu, sijaandika kwa kutolifahamu.

Jambo likikubalika dunia nzima, hilo halimaanishi kwamba ni sawa. Kuna wakati karibu dunia nzima iliamini na kukubali jua linazunguka dunia na dunia halizunguki jua. Hilo halikumaanisha kwamba jua lilizunguka dunia.

Migodi inapewa unafuu wa kulipa Royality

I take it that you mean royalty.

kama unafuu maana wanakuwa Wamewekeza matrillion na hawajaanza kurudisha hata nukta ya faida. Hata kama tungeacha hadi 2050 muwekezaji lazima angeanza na royalty ndio Walipe kodi otherwise na sisi tushiriki kuwekeza hata 40%.
Hiki si kitu ambacho sikijui, ni kitu ambacho ninakijua. Ndiyo maana nikaandika hpo juu labda Nyerere alivyofikiri tuwaachie vizazi vyetu waje kujifunza ku manage madini haya vizuri si jambo baya, kwa sababu royalty ya 4% ni biashara kichaa, Naelewa wanatumia hela nyingi kuwekeza, lakini bila madini hizo hela ni ndogo sana, kwa sababu wangetakiwa kutumia hela mara mia zaidi kutengeneza madini yao, if at all that is possible.
Au twende tukajifunze Botswana.....

Sasa kujifunza Botswana umeona ni jambo la ajabu sana kulinganisha na 4% royalty?

Botswana Seretse Khama alikuwa anajielewa kutoka alivyokuwa London 1947. Watu wameongelea haki za Watswana kuhusu madini yao kwenye Bunge la House of Lords wakati Winston Churchill anapigania kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

Kasome kitabu kinaitwa "The Colour Bar: The Triumph of Seretse Kama and His Nation"

Pili kwa nini Williamson diamond mining /mwadui wapo tangu enzi za nyerere hadi kesho lakni nao inasemekana hakuna chochote tunafaidi. Wakati ukoo wa Williamson unafaidi na kuwa mabillionea mkuu.

This question is only as relevant as someone can say "two wrongs are still wrongs, but they do not make a right"

Labda Mwadui ni somo lililomfanya Nyerere ajue kwamba mikataba ya madini haiko fair na hatuna haja ya kuingia mikataba zaidi mpaka dunia itakapokuwa fair zaidi.

Kumbuka Nyerere alikuwa champion wa South to South Cooperation na aliweza kutingisha dunia kwenye haya mambo. Aliweka mfano si kwa Tanzania pekee, bali kwa dunia nzima.

Tupe uzoefu maana wengine miaka hiyo hatukuwepo na reasoning zake zilikuwa nini hasa...

Mimi mwenyewe nilikuwa mdogo.Lakini naweza kuelewa kwamba hata dalali anayekutafutia nyumba Sinza hawezi kukubali royalty ya 4%, seuze serikali inayochukua mkataba wa muda mrefu.

Nakubaliana na wewe transparency ya mikataba itasaidia kuondoa hofu tunaibiwa au hatuibiwi na nchi nyingi sasa kutokana na tatizo tulilonalo wameamua kuweka wazi na nusu wazi hasa mikataba ya madini na other natural resources....

Kama nilivyosema mwanzo, bila transparency, hata kama wafanyakazi wengi watiifu na adilifu wa serikali watatupa mikataba mizuri sana, nchi inaweza kuingia katika mgogoro unaoweza kusababisha vita vinavyotokana na wananchi kuona wanaibiwa kwa sababu tu mikataba haiko wazi.
 
Zitto alishaiona na akasema ni ya kawaida sana na wala haijaandikwa siri, wapigaji tu ndio wanaotudanganya kuwa ni siri.
Naweza kukubaliana na wewe kwa asilimia flani. Maana vyote ambayo tunatumia vigezo vya kusema mikataba ni mibovu ni vitu visivyo vya kimikataba mfano 4% na exportation of concentrates sioni kama ni mikataba maana mineral agreement act sidhani kama ni mikataba. Ndio maana sera ya madini baadae chini ya jk ilizuia makinikia kwenda nje ya nchi hadi leo ila changamoto ikawa ni mtambo wa kufanya hiyo kazi hapa. Hata Leo serikali ikisema inanunua huo mtambo na wakasema gold, copper, silver tunachukua mrabaha au kodi yetu 30% yanayobaki yote tunayauza yote kwa faida maana muwekezaji anasema kilichobaki chote akishauza hizo products Tatu ni mali ya smelter basi tukimiliki smelter kama taifa basi madini yaliyosemwa na tume yatakuwa yetu yote ukitoa hayo matatu. Changamoto ni je ni kweli smelter hizo ni cheap kama tunavyoambiwa na wataalamu wetu au costful karibu trillion moja kama anavyosema muwekezaji. That is our dilemma....
 
Back
Top Bottom