GE2025 Wajumbe wampitisha Mavunde ubunge Jimbo jipya la Mtumba Dodoma

GE2025 Wajumbe wampitisha Mavunde ubunge Jimbo jipya la Mtumba Dodoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Wajumbe Wa CCM wa Jimbo jipya La Mtumba wameamua Kwenda na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ✅✅✅ -
1145505264.jpg

Zoezi la kupiga kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwapata wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani katika Jimbo la Mtumba, mkoani Dodoma, limekamilika rasmi katika kata saba, huku aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, akiongoza kwa tofauti kubwa dhidi ya wapinzani wake.

Katika kata mbalimbali, Mavunde amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wajumbe, jambo lililodhihirika wazi wakati wa kuhesabu kura ambapo ameibuka mshindi katika kila kata, ikiwa ni pamoja na Kata ya Kiwanja cha Ndege ambako alipata kura 124 kati ya kura halali 143. Wagombea wengine waliopambana naye waliambulia kura chache mno.

Katika Kata ya Msalato, Mavunde alipata kura 153 kati ya 187 zilizohesabiwa kuwa halali, huku katika Kata ya Mtumba akiibuka na kura 189 kati ya 270. Uungwaji mkono uliendelea kudhihirika katika Kata ya Iyumbu ambako alipata kura 138 kati ya kura 153 zilizopigwa.

Mwelekeo huo wa ushindi ulijirudia pia katika Kata ya Ipagala, ambapo alipata kura 192, na Kata ya Kikombo ambako alipata kura 347 kati ya 459 zilizopigwa. Kata ya Makole ilikamilisha mzunguko wa kata saba, ambako Mavunde alipata kura 107 kati ya kura 118 zilizopigwa

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom