Wajumbe wa Bunge Maalum wasusia Bunge

Wajumbe wa Bunge Maalum wasusia Bunge

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Wakati Bunge Maalumu la Katiba linatarajia kuanza kujadili Rasimu ya Katiba kesho, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo wameanza kuondoka bungeni, kupinga mwenendo wa Bunge hilo.

Hatua hiyo ya wabunge hao inakuja wakati Bunge Maalumu la Katiba juzi lilipitisha azimio la kutumia kura ya siri na wazi katika kuamua vifungu vya rasimu.

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samia Saluhu alisema baada ya kupitishwa kwa utaratibu wa kupiga kura za siri na wazi katika Bunge hilo, kuanzia Jumatatu wataanza kujadili sura ya kwanza na sita ambayo inahusu Muundo wa Muungano.

Katika sura ya kwanza, mambo ambayo yanatakiwa kujadiliwa ni Jina, Mipaka, Alama, Lugha na Tunu za Taifa wakati sura ya sita mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa ni Muundo wa Muungano.

Lema atangaza kurudi jimboni Arusha

Mjumbe wa Bunge hilo, Godbless Lema alisema anakusudia kuondoka bungeni, kutokana na kutoridhishwa na maridhiano ya kupiga kura za siri na wazi katika kufikia uamuzi katika Bunge hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Lema alisema hakubaliani na utaratibu uliopitishwa, kwani unalenga kulazimisha kila jambo ambalo chama tawala kinalitaka lipitishwe.

“Huu utaratibu wa kura kupigwa kwa wazi na siri katika kitu kimoja, haupo sehemu yoyote duniani. Sasa sisi kukubali ni kuwasaliti wananchi, kwani hata Dodoma tunaandaa rasimu ya Katiba ya wananchi wote siyo ya CCM pekee,” alisema Lema.

Alisema pia hakubaliani na utaratibu wa kujadili rasimu ya Katiba, ambao umetolewa na Kamati ya Uongozi kwa kuanza na sura ya kwanza na ya sita, kwani vinalenga kufumua Rasimu ya Jaji Warioba.

“Hapa CCM wanataka kulazimisha Serikali mbili kwa kujadili kwanza vifungu hivi, kama vitapita basi watakuwa na uwezo wa kubadili rasimu yote kitu ambacho mimi siwezi kukaa kwenye Bunge hili na kusaliti wananchi waliotoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba,” alisema Lema.

Jussa atabiri Bunge kuvunjika.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mjimkongwe, Ismail Jussa, alisema uchaguzi wa vifungu hivyo ambavyo ndivyo vinabeba Rasimu ya Katiba, vinaashiria kuvunjika kwa Bunge hilo katika hatua za awali.source mwananchi
 
Sasa utasemaje kuwa wabunge wanakachanbunge kumbe ni ujinga wa Lema tu?
 
Ni mtu asiye makini tu ambaye anaweza kuamini kuna kitu kinaitwa katiba mpya,kama itapatikana katiba itakuwa ni ya ccm ,mchakato utakwama wiki ijayo tu kwenye suala la muundo wa serikali 2 au 3.
 
usiseme wajumbe, sema mjumbe Lema. Ingawa tunajua hawezi kuacha laki 3 labda kama baba yake kamtuma chalinze kwa posho nono.
 
piganeni kiume jamani kuondoka na kumsusia paka samaki atakula hadi miba., Kama ni kuvunjika basi lije livunjike kuwe hakuna option kote pande 2 kuweza kuendelea, we trust you Jussa & UKAWA
 
Tusitegemee kupata katiba mpya ya wananchi,tutegemee kupata katiba mpya ya CCM.
Mbombo ngafu.
 
Wameondoka kweli na posho wameacha ? Hawahawa tunaowaona kila siku wameondoka na kuacha posho? Waite waambie nao wamo japo walikula kibongobongo watarudiii. Waite
 
Wasiondoke japo hatukuwatuma ktk bunge la katiba tuliwatuma ktk bunge la jamuhuri hayo maamuzi walijifanyia wao baada ya maccm kupitisha vufungu hivyo basi wakae huko wawabane mpaka tuone malengo ya maccm yalikua nini hasa watafunguka tu tusiwawahishe sana.bunge lao la bajet nalo linawasubiri na wanatakiwa wakae miezi mitatu kabla ya mwezi wa 7 tuwe tumepata bajet sasa kazi kwao yetu macho na serikali za mitaa hausogezwi mbele wala nn tutapachimba so wabaneni huko ili wakija uraian kila mtu awe amesha wasoma na unafk wao wa uwazi ktk vifungu ila mikataba ndio siri na wanaapshwaga kwa baibo na Qaran hawa.
 
Sasa utasemaje kuwa wabunge wanakachanbunge kumbe ni ujinga wa Lema tu?

Kwa jinsi ccm wanataka maoni yao yawekwe kwenye rasimu hii, jee kutakua na jambo jipya tofauti na katiba ya sasa?
 
Tusitegemee kupata katiba mpya ya wananchi,tutegemee kupata katiba mpya ya CCM.
Mbombo ngafu.

Mi kwa ushauri wangu wasiondoke na waendelee kufanya kama walivyokuwa wakifanya hapo awali yaani wanapoona maCCM wanaendesha mambo ya hovyo wazomee mwanzo mwisho hadi vikao viwe vanahairishwa tu.
 
Sasa akitoka si kura yake haitahesabiwa, ikiwa hivyo basi waite mtu mwingine kujaza nafasi yake ili tuone mwenendo wa kura. Mie nampendekeza mtanganyika mmoja. Kura yake ni muhimu nashangaa kwa nini haelewi hili
 
Mi kwa ushauri wangu wasiondoke na waendelee kufanya kama walivyokuwa wakifanya hapo awali yaani wanapoona maCCM wanaendesha mambo ya hovyo wazomee mwanzo mwisho hadi vikao viwe vanahairishwa tu.
Kibogo upo sahihi kabisa hata mm nakubaliana nawe hapo iwe ZOMEAZOMEA tu mpaka watakapochoka na kuliahirisha bunge au kulivunja kabisa maana hii ni kulazimishana
Wazanzibar wanataka Nchi yao sisi Tanganyika hatutaki no aibu ya nini tunaogopa?
Kama Mume shamba linakushinda si uwaache wenzio (Oman, Dubai (UAE) na wengineo) wakalilime. Mke hakutaki ni miaka 50 sasa huna uwezo mwache aende zake
 
Back
Top Bottom