GE2025 Wajumbe Tabata watakiwa kutoka nje baada ya kupiga kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,608
Wajumbe wa Kata ya Tabata Jimbo la Segerea, jijini Dar es Salaam wametakiwa kutoka ndani ya ukumbi mara baada ya kupiga kura.​

1754304454439.png
Hata hivyo, tangazo la kuwataka watoke ndani kwenda nje limeibua malalamiko leo Jumatatu, Agosti 4, 2025 katika ukumbi wa Green Light kutoka kwa wajumbe.

Hatua hiyo imefuatia baada ya matangazo kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa mchakato huo (hakutaka kutaja jina) alipowatangazia wajumbe wanapaswa kutoka nje mara baada ya kupiga kura.

"Ndugu wajumbe tunaanza rasmi zoezi letu la upigaji kura, na kwa sasa hatutoruhusu mtu yeyote kuingia ndani. "Wajumbe baada ya kupiga kura utaratibu mtatoka nje, nje ya geti kabisa na ndani tutaendelea na utaratibu mwingine," amesikika akitangaza.

Hata hivyo, kauli hiyo ilizua malalamiko kutoka kwa wajumbe ambao walikiwemo katika ukumbi huo wakipinga utaratibu Mtoa matangazo huyo alisikika akisisitiza:"Utaratibu utakaotumika ni kama nilivyotangaza na kama mna wasiwasi mawakala wako hapa."​
 
Dah. Tunanaogopana sisi kwa sisi?
 
Tunasubiri kwa hamu jioni tupate taarifa idadi ya walioumizwa na waliouwawa kwenye kumbi mbali mbali za mikutano ya kuteua wagombea .
 
Hahahaha! watu wamestukia mchezo.... inaonekana watu wanataka kupiga Tiktaka kuibeba ile takataka ambayo haipendwi na raia jimboni.
 
It's very sad kwamba huu ndio uchaguzi wa wabunge na madiwani 2025. Baada ya hapa tutakuwa tunajua mbunge wa jimbo fulani ni nani.

Hakuna sababu ya kupoteza fedha za umma kuandaa uchaguzi, coz ukweli ni kwamba zinapotea tu.
Kweli kabisa aisee. Yaani leo ndio uchaguzi mkuu wenyewe
 
Back
Top Bottom