GE2025 Wajumbe CCM Zanzibar wazuiwa kuingia ukumbi kisa sare

GE2025 Wajumbe CCM Zanzibar wazuiwa kuingia ukumbi kisa sare

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Baadhi ya wajumbe wa kupiga kura za maoni Jimbo la Mfenesini wamezuiwa kuingia ndani ya ukumbi kwa kile kilichoelezwa hawakuvaa sare za chama kama walivyoelekezwa
Wajumbe wa jimbo hilo wameanza kuingia ndani saa 3:00 asubuhi kwa ajili ya matayarisho ya upigaji kura za maoni kwa wabunge, wawakilishi na madiwani.

Jimbo hilo lenye wadi tisa ikiwemo ya Mfenesini, Mwakaje, Mwachealale, Kitundu, Bumbwisudi, Chuini, Kikaangoni na Kihinani.

Katika wadi hiyo wajumbe wote walitakiwa kuvaa sare za chama ikiwemo nyeusi na kijani, ambao hawakuvaa mavazi hayo hawakuruhusiwa kuingia ndani jambo ambalo liliwashangaza wengi na kusababisha mvutano wa maneno, wengine wakiondoka katika eneo hilo na baadhi yao kusubiria uamuzi utakaochukuliwa.

Hata wajumbe ambao wamevaa nguo za kijani zenye nembo za Chama cha Mapinduzi (CCM) hawakuruhusiwa kuingia ndani na walitakiwa kurudi makwao ili kuepusha usumbufu kwa sababu ilidaiwa kuwa tangazo ndivyo lilivyosema.

Baadhi ya wajumbe waliofika katika eneo hilo wakiwa na mavazi ambayo hayaruhusiwi walidai kuwa tangazo hilo lilichelewa kutoka na wengine wakidai kutolisikia kabisa.

Akizungumza na Mwananchi, Msimamizi Msaidizi wa wadi ya Mfenesini, Juma Mohamed Haji amesema sababu ya wajumbe hao kuzuiliwa kuingia ndani ya ukumbi huo ni kutovaa sare za chama zilizoelekezwa kwa mkutano huo.

Baadhi ya wajumbe wa kupiga kura za maoni Jimbo la Mfenesini wamezuiwa kuingia ndani ya ukumbi k.jpg
Chanzo: Mwananchi Digital
 
Back
Top Bottom