Elections 2010 Wajue wapinzani mahiri waliokaliwa kooni majimboni

Remmy siko juu hata kidogo ndugu yangu najaribu tu kutoa tathmini ya hali halisi kwa upande wa upinzani, kwani kuna post humu jf inaonyesha wa ccm walio kikaangoni majimboni

Ni ukweli ulioongea ktk post yako lakini ningependa kila mwana jf atoe tasmini na maoni yake kupitia jimbo alilopo ili kupata ukweli kuliko kuamini habari za kusikia. Mimi nipo kikazi jimbo la HAI kwa kimpindi cha wiki mbili sasa hapa HAI mjini mji wa BOMANG'OMBE MBOWE anawapeleka puta sana CCM asikuambie mtu kwa utafiti wangu mdogo usio rasmi nilioufanya FUYA KIMBITA mgombea wa CCM mbunge anayemaliza muda wake hali yake si nzuri kisiasa jimboni humu labda sikuzilizo baki kuelekea uchaguzi mambo yabadilike lakini mjini na vijijini mpaka sasa MBOWE amewashika CCM
 
Halima mdee na J mbatia, wanadaiwa kugawana kura na kumuacha ccm akipeta
Hali kama hiyo ipo na ubngo, Mtatiro na myika
Segerea mpendazoe hoi
Kwa Zitto hali si shwari kabisa hadi anafikia kuilaumu cuf kusimamisha mgombea strong anagawa kura.
Mrema alianza vizuri lakini sasa mambo yamemkalia vibaya sana vunjo
Mtu mzima Mbowe anatumia nguvu nyingi sana lakini hadi sasa hali yake si ya uhakika
Bwana lema mzee wa kigeugeu hapo arusha watu hawana imani nae kabisa sasa anatishia kuua.
Tundu lisu ndio kabisaa hoi sgd.
Mwenye taarifa zaidi aiweke nawasilisha


Jamani tuwe wakweli na tujadili hoja kwa hoja na si kiushabiki. Naona Zitto anatajwa kuwa maji ya shingo jimboni kwake hivi kweli Zitto angekuwa anapelekwa mbio angeondoka jimboni na kwenda Jimbo la kibaha, mkoani lindi na sasa Bukombe kupiga kampeni. Embu tutafakari kwa umakini ungekuwa wewe ndio Zitto na jimboni mambo hayaendi vizuri ungeenda kuwapigia kampeni wagombea wa chama chako au ungebaki jimboni kupambana? embu vaa viatu vya Zitto halafu ujibu hii changamoto
 
hii ndo demokrasia msiwe waoga! sisi wananchi tunataka kiongozi anayefaa mwisho wa siku chuma na chuma visuguane tupate kitu cha ukweli! CCM hawana jipya ukiona hao tu ndo wanaozungumziwa hamna anye wajali!
 
Mayu
Hakuna habari ya unafiki hapa, kama wewe ni mkaazi wa Dar hebu fikiria nguvu ya Mtatiro, nakisha ya Mnyika upande wa ubungo, niwazi watagawana kura tu,
vipi kuhusu Mbezi kwa Mdee na Mbatia
mkuu hizi ni taarifa zilizo fanyiwa kazi na sio uzushi kama unavyo weza fikiria

Kwa nini useme watagawana kura na kumwacha CCM anapeta? Mie nakwambia kuwa watachukua za CCM, hivyo mgombea wa CCM atapata kura kidogo na hao wapinzani ndo watakaoshindana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom