Pentatonix ni kundi la muziki wa acapella (mara nyingine hufupishwa kama PTX) ni vijana walioshinda tuzo za Grammy mara mbili kama BEST ACAPELLA GROUP kutoka Marekani vijana hawa wanatokea eneo lijulikanalo kama Arlington, Texas; na majina yao ni Mitch Grassi, Scott Hoying, Kirstie Maldonado (Muimbaji wa kike pekee), Kevin Olusola (Mtengeneza midundo ya mdomo au BEAT BOXING nna Mmarekani mwenye asili ya Nigeria ambaye Baba yake ni daktari huko Marekani), na Avi Kaplan (ambaye huimba sauti nzito na kujazia beat pia).
Kazi zao ambazo ni katika aina ya muziki wa Pop, wamekuwa wakirudia nyimbo mbalimbali na kuzifanya ziwe tamu zaidi au kwa kizungu tutasema wanafanya COVERS.
Ndugu zangu wanaJF nimeambatanisha baadhi ya video ili mjionee utundu na utamu wa hawa vijana na pia kama kuna mdau anawajua zaidi anakaribishwa.