The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,160
Mossad walishatathimini uwezo wa Iran kabla ya kuanzisha vita. Walianzisha vita baada ya kuhesabu garama. Walijua kwamba Iran itajibu kwa kishindo kulingana na uwezo ilionao wa makombora. Na ndio maana wiki mbili kabla ya vita Israeli walihamisha vitu muhimu kwa taifa lao. Waliondoa ndege zao katika uwanja wa Ben Gurion na zana muhimu katika bezi zao. Wakati huo Iran ikiwa off guard wakizungushwa na Trump katika meza ya mazungumzo. Na ajabu Mossad wamemuua hadi yule aliyekuwa anaongoza mazungumzo kwa upande wa Iran.
Wakati Iran imelala usingizi, Mossad walikuwa bize kutafiti makazi ya viongozi wa Iran, kuingia na kutoka kwao na sehemu muhimu ambazo zinasadikiwa kuwa ni ngome za uundaji wa makombora, urutubishaji wa Uranium kuelekea bomu la nyuklia. Na zote zimeshambuliwa. Hivyo sasa Iran hakuna production inayoendelea ya makombora, wanatumia hazina waliyonayo. Maana viwanda vimeharibiwa kwa target za IDF.
Mossad pia walifanikiwa kupanda majasusi wao katika ngazi za usalama wa taifa wa Iran, katika jeshi na sehemu muhimu za kitaifa. Usalama wa Iran ukawa usingizini maana wadau wake ni mawakala wa Israeli. Ndio maana utaona Mossad waliweza kufungua hadi viwanda vya drones ndani ya Tehran na sehemu zingine za Iran. Na utastajaabu kwamba drones zilizoua wakuu wa Iran kwa 80% zimeundwa hapo hapo Iran. Ndio utaelewa kwamba jinsi Iran ilivyozembea au kuzembeshwa na adui anayekaa ndani yake. Hebu tuwaangalie kidogo hawa Mossad ni nani:
Mossad
Ni shirika la kijasusi la Israeli liloanzishwa mnamo 13, december 1949 chini ya usimamizi wa Ben Gurion waziri mkuu wa kwanza wa Israeli. Jamii ya kijasusi ya Israeli imegawanyika katika idara kuu tatu:
1)Aman: (Military Inteligence). Hii ni idara kuu katika Israeli Defense force (IDF) yaani jeshi la ulinzi wa Israeli.
2) Shin Beit: (Internal security). Hii inashughulika na usalama wa ndani wa nchi, kama kuwagundua maadui wa ndani, kuzuia magaidi na ugaidi na ndio inafanya operation zake katika maeneo yote ya nchi ikiwemo makazi ya Wapalestina ikiwemo Gaza.
3) Mossad: Foreigner intelligence service). Wanashughulika na usalama wa nje wa Israeli.
Mashirika haya matatu yote yana ripoti kwa waziri mkuu wa Israeli. Ngoja tuwazungumzie kidogo Mossad.
Hawa ndio shirika hatari sana katika Israeli na moja katika mashirika ya kijasusi bora duniani. Mossad ndio walifanya misheni zenye ufanisi mkubwa katika kuwakamata maofisa wa NAZI waliofanya mauaji ya halaiki kwa Wayahudi. Waliwasaka kila kona ya dunia na kufanikiwa kuwaua na wengine kukamatwa.
Logo: yao ni kinara cha taa saba (7) kinachopatikana katika kitabu cha Kutoka 25:31-20. Kikiwa kimezungukwa kwa maneno ya maandiko kwa Kiebrania katika Mithali 11:14. Yanayosema:
Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.Mit 11:14 SUV
Motto: wa shirika la Mossad unapatikana katika Mithali 24:6 inayosema:
Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu. Mit 24:6 SUV
Mossad wametapakaa katika ulimwengu wakilinda usalama na maslahi ya Israeli na raia wa Israeli wanaoishi nje ya Israeli. Na ndani ya Mossad kuna vikosi vitano (5) vya operation. Nitazungumzia vikosi viwili kati yake ambavyo ni;
1) Caesarea kwa jina la Kiebrania ni Bayonet. Hawa kwa jina lingine wanaitwa kundi la mauaji (group of assassins). Na assasin anajulikana kwa jina la KIDON. Hivyo Bayonet inajulikana pia kama nyumba ya wauaji ambao wanafunzwa kwa miaka miwili jinsi ya kuua. Hawa ndio wanaoendesha operation ya assassination ya viongozi wakubwa, viongozi ambao wana nia mbaya na Israeli. Viongozi wa Hezbollah na sasa wa Iran wanauawa na hawa Kidon.
2) Metsada: kundi maalum (special unit) ambao wanaenda kwa kikundi katika misheni maalum kuzimisha tukio lolote au kuua kabisa.
Mtumishi wa Mossad anaandaliwa toka akiwa kichanga akiangaliwa uwezo wake na kipawa alichonacho katika makuzi yake. Akifikisha miaka 18 anaingizwa katika misheni. Mossad wamefanikiwa kupandikiza vizazi vya Kiyahudi katika nchi nyingi duniani ambavyo vinawapa taarifa za kijasusi toka nchi hizo. Mfano kwa Iran, maofisa wengi wana chembe chembe ya damu ya Kiyahudi na hao wameunda mawakala wengi ndani ya Iran ambao wengi wao ni Waajemi wenyewe ambao wengine wanatumika kwa maslahi ya Israeli wakijua na wengina pasipo kujua. Iran enzi za Mohamed Nejad rais wa Iran mstaafu, waliunda shirika la kijasusi la kuzuia majasusi wa Mossad ndani ya Iran, wakaja kushtuka baadae kuanzia mkubwa wa shirika hilo hadi uongozi wote wa ngazi ngazi kushuka hadi 20 ni majasusi wa Mossad. Walipotaka kuwatia nguvuni, wakakuta walishakimbia kitambo na kutokomea Israeli hadi leo hii.
Angalia siries hizi: Tehran na Fauda. Humo unajifunza jinsi Shein Bet na Mossad wanavyofanya kazi zao za kijasusi ndani na nje ya Israel. Sio rahisi kukabiliana na hao watu labda ulifute kabisa taifa lao. Maana ni wasomi wa hali ya juu katika sayansi, tekinolojia na siri za ulimwengu huu. Na pia moja ya misheni yao ni kuunda matajiri wa Kiyahudi na kuwalinda duniani. Maana Wayahudi wanaamini uchumi ni msingi mama wa ulinzi.
Juu ya Mossad nitakuja na makala maalum juu yake. Na nimeahidi kutoa makala kadhaa lakini sijazitoa kulingana na kuwa bize kusaka taarifa na kuripoti juu ya vita ya Iran na Israeli inayoendelea. Lakini nitaleta makala hizo ikiwemo makala ya operation rising Lion. Mniombee.
Na Jeff Massawe
Mhubiri, Mwalimu, Mchambuzi wa mambo ya kijamii na siasa.
0757722557 (whatsapp inapatikana pia).