Wajinga comedy lyrics

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,134
5,242
🎵🎤🎤🎤📻📼🎧🎤🎤🎤🎤🎵
Naanza kuwaza/Ujinga wa hawa
mafaza.🎶

Sisi ni wa afya bora/wao wa isiyo imara
Tupo mbali sana/wao nyuma kinoma
Tutatoa misaada/ikitokea kwao maafa🎼🎵

Wako gizani/nuru hawana asilani
Si mchina mjerumani/wote twawaona hayani
Watutazama kwa hiyana/haya maajabu twayafanya
Malaria sugu hatuna/wao yawatafuna
Ukimwi tunaponya/wa siyo macho kuona🎹🎵🎵

Mabeberu si mabwana/kwetu sisi ni wavulana🎸🎵
Tazama wetu vijana/hawaendi kwao kusoma💨🎵🎵
Waomba,omba sana/mpaka twawachoka hahaaha😂😂

Vipi kuhusu korona/wao wazidi pukutika😷😷🎶
Sisi afya tumeimarisha/watuomba ifurumisha😂😂🎶

Itali inaangamia/sisi tunasubiria😯
Kwetu ikifika/corona😷😷 twaipukutisha
Tuna madaktari imara/India yatuhara
Tukusanyike misafara/Tuisifu yetu Sera
🎺🎷🎶🎶
Wajinga nyinyi/hamtuoni sisi
Tu matajiri/kila mmoja ala firigisi
Mu dunia ya pilipili/sisi ya kwanza halisi
Corona aina ya kirusi/kilicho tengenezwa na sisi💉💉💉

Imani yetu imara/Twafahamu ya mola
Tusubiri ikiripuka/Kama tutawaita
Mipaka kufunga/Tusubiri malaika
Ajali ikifika/saa na dAkikia tutaifurumisha!!!📀🎶🎶🎵

Wajinga wazungu/akili iliyo na ukungu
Sisi ni walimu/mwakosa ufahamu🎶
Hamuijui afrika/sisi twaitikisa!!!
Tanzania ya dunia/afrika yajivunia🎶
Technolojia yakua/vingi twa vumbua.📼
🎶🎵

Wazungu wazungu/acheni majungu
Akili za beberu/mjinga waruwaru.🎶🎶

******sent using daraja LA mfugale*****
 
#jikinge na corona,covid-19.
-inaua bila kuchagua-
 
Back
Top Bottom