chambimagaka
JF-Expert Member
- Nov 17, 2017
- 288
- 338
*WAJIBU WA DEREVA KWA ABIRIA WAKE*
*Je, ni upi wajibu wa dereva kwa abiria* au kwa lugha nyingine dereva ana wajibu kwa watu wa ngapi? Labda tuanza na swali hili.
*Watu ambao dereva anawajibika kwao*
1. Abiria;
2. Watumiaji wengine wa barabara;
3. Mmiliki wa chombo.
Leo tutaangazia wajibu wa dereva kwa abiria wake na misingi yake kisheria.
*Msingi wa Wajibu wa Dereva kwa Abiria*
Dereva kama alivyo rubani au mtu anayemiliki nyumba au mwenye udhibiti na mazingira Fulani anawajibika kwa wale wanaomtembelea kwenye nyumba, mazingira, au eneo hilo analolidhibiti. Wajibu huu kisheria za madhara huitwa *Occupier’s liability*
*Occupier’s liability ni wajibu wa kisheria wa kujali au kuchukua tahadhari (DUTY OF CARE) unaomkuta mtu yeyote anayemiliki au kusimamia mali au kitu kwa watu wanaotembelea au kukatisha kwenye mali hiyo. Sheria inataka mtu yeyote anayetembelea eneo unalolimiki au hata kuingia isivyo halali, uhakikishe kwamba ametoka salama kwenye eneo hilo. Kwa hiyo mmiliki au mwenye usimamizi wa eneo hilo atawajibika kwa ajali au hali ya hatari itakayokuwepo kwenye eneo hilo lililo chini ya udhibiti wake.
Kisheria *visitor* au kwa lugha rahisi mgeni (mtu anayezuru kwako) ni mtu yeyote ambaye unamkaribisha au kumpa ruhusu ya kuingia kwenye makazi yako, eneo au kitu unachokimiliki au kuwa na udhibiti nacho bila kujali mtu huyu atatumia au kuwepo tu kwenye makazi au eneo hilo. Kumruhusu kunaweza kuwa kwa maneno (expressly) au kwa vitendo (impliedly). Hivyo, ndio kusema mtu akija kwako lazima uhakikisha ameingia na kutoka salama, kama kuna vyupa, misumari, au hatari yoyote unatakiwa kuhakikisha umeviondoa ili asiumie. Vivyo hivyo kama unajua nyumbanmi kwako kuna kivutio kama vile embe mtini. Machungwa au chochote kile basi tegemea wageni mfano watoto. Hivyo kisheria unatakiwa uweke mazingira salama ili wageni hao wakifika, hata kama hawakuomba ruhusa kuingia wamalize shughuli zao watoke salama. Hii inahusisha hadi wezi wanaokuja kukuibia hakikisha hawaumii wanaporuka ukuta na kuingia ndnai kwako.
Vinginevyo unatakiwa kujitoa lawama kwa kuweka kitu kinachoitwa *a disclaimer of liability*, yaani *kujiondoa kwenye lawama* kwa kuandika mfano *MBWA MKALI*; *FENSI INA UMEME*; *TAHADHARI MISUMARI CHINI* au *TAHADHARI DARI FUPI* na maandishi haya yaonekane.
*Dereva kama mmiliki wa chombo au mdhibiti*
Dereva, kwa kumruhusu mtu aingie kwenye gari lake na kukaa, moja kwa moja anakubali kubeba majukumu ya kisheria ya kuhakikisha usalama wa mtu yule. Gari ni premise, na mdhibiti wa gari hilo kwa wakati huo ni dereva. Hivyo dereva ana wajibu wa kuhakikisha kuwa abiria au mtu yeyote aliyeingia kwenye gari anaingia humo na kutoka salama.
*Maana yake ni nini*?
Maana yake ni kwamba ndani ya gari msiwe hatarishi, kama kuna vitu vinavyoweza kumjerushi mtu kama vile vyupa, vitu vyenye ncha kali nk vitolewe. Dereva anatakiwa kuhakikisha hata abiria hadhuriki toka kwa abiria mwenzake, wala mzigo wake hauibiwi au kupotea. Katika kesi ya Carver v. Chase, 128 Fla. 287, 174 So. 408 (1937). Mahakama ilipata kusema kwamba *anyone who allows a person to ride in their vehicle as their guest (passenger) has a duty to that passenger to exercise ordinary and reasonable care in the operation of their vehicle and to keep that passenger safe.* Kwamba mtu yeyote anayemruhusu mwingine kupanda gari lake ana wajibu kwa abiria huyo kuhakikisha anachukua tahadhari za kawaida za kujali katika kuendesha gari na kumfanya abiria huyo awe salama*
Hii ina maana kwamba dereva unapojua kabisa umepakia abiria kisha ukaanza kuendesha kwa hatari mfano unaovateki ovyo maeneo ya hatari, unayumbisha gari hadi watu wanagongana vichwa, au unaendesha kwa speed kubwa kuliko inayotakiwa. Iwapo abiria yeyote ataumia anayo haki ya kukushtaki wewe binafsi na akakudai fidia nje hata ya mmiliki. Madai haya ni nje ya ile kesi ya kitrafiki utakayoishtakiwa na Jamhuri kwa kukiuka sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali ambayo imeleta majeruhi au kifo.
Ndio maana katika kuhakikisha abiria wanakuwa salama mwanzo hadi mwisho wa safari, dereva anwajibika kuwatangazia wafunge mikanda, kuwatangazia wasiotoe mikono au vichwa nje wakati gani inatembea, n ahata kama sehemu kuna wizi, basi kuwatahadharisha kuwa makini na wezi eneo hilo. Pia dereva ana wajibu wa kutomuacha au kumshusha abiria eneo lisilo na usalama. Kupuuzia mambo haya kunaweza kukufikisha pabaya sana kama dereva. Siku ukikutana na abiria anayejua haki zake anaweza kukushtaki wewe, na kama huna hela ya kumlipa anaweza kuiomba mahakama akamate mali zako zozote na kukufilisi kabisa kufidia hasara.
*KUMBUKA KWAMBA*: Malipo ya bima pekee yahamzuii abiria aliyeumia au ndugu wa abiria aliyekufa kwenye ajali kwend akudai fidia Zaidi kwa hasara iliyopatikana. Kwa mfano mtu anaona anastahili fidia ya shilingi milioni 50, bima wamemlipa milioni 5, bado mtu huyu anaweza kwenda mahakamani kufungua kesi kudai malipo Zaidi, na safari hii ni kutoka kwa mmiliki na dereva maana bima washatekeleza sehemu yao. Madereva tungekuwa tunajua mambo haya tungekuwa tunachukua tahadhari ya kutosha.
Kwa ufupi au urefu huo ndio wajibu wa dereva kwa abiria wake.
RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.