Sijaelewa lengo hasa la mada yako. Yaani unataka kuja nini hasa?
Danke verr.Danke.
Mm Niko Uvinza ila Kila nikiuliza wenyeji maana ya jina Hilo hawana majibu yakutosheleza..Kama nimekuelewa vizuri basi mchango wangu ni huu: Kwanza, kama ulivyosema, kuna baadhi ya maeneo kama Arusha,Kilimanjaro na Moshi, ambako Wajerumani waliendelea kutumia majina waliyoyakuta. Hata hivyo waliyaandika majina hayo kulingana na jinsi ambavyo wao waliweza kuyatamka (tunaita sound-spelling). Mfano mzuri hapa ni Kilimandscharo (Kilimanjaro), Aruscha (Arusha) na Moschi (Moshi). Linganisha: sauti [sh] (kiswahili) ----> [sch] (Kijerumani); sauti [nj] (Kiswahili) ----> [ndch] (Kijerumani), na sauti [j] (Kiswahili) ----> [dz] (Kijerumani).
Pili, katika maeneo mengine, Wajerumani (hata wakoloni wengine) hawakutumia majina waliyoyakuta kwa wenyeji Bali wakaleta majina mapya. Majina haya yalitokana na majina ya watawala wao na watu wao wengine maarufu. Mifano mzuri hapa inaweza kuwa Wilhelmstal/Wilhelmsdorf (Lushoto/Handeni?), Bismarckburg (Kasanga/Rukwa?) na Langenburg (Tukuyu). Ikumbukwe kuwa Wilhelm ilikuwa mtawala wa Ujerumani na Bismarck alikuwa ni Kansela maarufu wa Ujerumani (ndo yule wa Berlin conference).
Pia yapo maeneo yaliyopachikwa majina ya miji, vitongoji na mitaa ya Ujerumani. Nadhani hapa mifano kama Neu-Trier (Mbulu), Neu-Hornow (Honnow?), Neu Bonn (Mikese?), Weidhafen (Manda?) n.k. inahusika.
Nadhani nitakuwa nimekupa dondoo kidogo.
Ukitumia neno shule katika Kiswahili, ujue hilo ni neno la Kijerumani tumetohoa kutoka "schule". Ndiyo maana Zanzibar walipokuwa na infkuence ya Uingereza zaidi hawatumii sana neno shule, wanatumia skuli.Sijui kwanini wamlitutawala lakini hawakuacha urithi wa rugha kabisa π€π€
Sijui kwanini wamlitutawala lakini hawakuacha urithi wa rugha kabisa π€π€
Usemavyo ni kweli. Ukisoma kwenye kitabu cha von Lettow Vorbeck "My Reminiscences of East Africa" anaonyesha dhamira, malengo na maono ya Wajerumani kwenye koloni lao la Afrika Mashariki. Pia, anakuonyesha kiwango cha maendeleo kilichokuwepo kipindi hicho. Kwenye kitabu "Battle for the Bundu" kilichoandikwa na John Miller anatueleza Wajerumani walikuja Afrika Mashariki kuishi na siyo kuchuma. Walikuwa na mipango thabiti ya kuendeleza eneo hili. Maeneo mengi yalyokuwa maarufu kipindi hicho leo ni dhooful hali. Hata Kilimatinde ulikuwa mji maarufu enzi za Wajerumani lakini leo hii chali.Nipo kyela...
Hii nchi ingekuwa ulaya ndogo kama tungetawaliwa na huyu bwana.
Tusingekuwa wavivu na tungekuwa na asili ya kujituma.
Alikuwa anania kubwa sana ya kutuendeleza kama jimbo la taifa lake.
Alikuwa ana Plan ya kupitisha Reli kwenye kata ya Mwaya ambayo kwa sasa dah imechoka sana nashindwa kueleza.
Nimefurahi sana kuona maeneo kama Lumbila na ikombe tayari yalipewa majina na mgermany miaka hiyo... kwa sasa ni porini na eneo kama ikombe kyela ni eneo lisilofikika... miaka 70 ya uhuru wanaikombe wanashuhudia kwa mara ya kwanza umeme ukiwashwa kwao 2023 na barabara ikijengwa kwao 2024... that is disaster
Hela, Shule......Sijui kwanini wamlitutawala lakini hawakuacha urithi wa rugha kabisa π€π€
Kwa wewe walikuachia moyo tu kwa huu uandishi wako. Hakuna ambacho wangeweza kukuachia cha maana.Sijui kwanini wamlitutawala lakini hawakuacha urithi wa rugha kabisa π€π€