ngajapo
JF-Expert Member
- Jun 3, 2012
- 1,782
- 3,524
Mimi ni mjasiliamali ambaye baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu, niliamua kufungua kampunu ya kibiashara inayohusiana na masuala ya (BUSINESS TRAINING, PROMOTION AND ADVERTISEMENT). wazo hili lilikuja baada ya kusota saana mtaani kutafuta kazi bila mafanikio. bahati nzuri nikafanikiwa kupata fedha kidogo ambazo zilinisaidia kufanya usajili na mambo mengine muhimu kama vile kupata leseni kutoka mamlaka mbalimbali zinazohusiana na kazi ya kampuni husika lakini pia nikiwa nimebakiza fedha kidogo za kutosha kukodisha pango kama ofisi ya kufanyia kazi za kampuni nk.
Dunia ni kama kizungumkuti. baada ya kumaliza taratibu zote zinazotakiwa (nikimaanisha kuwa kampuni imekamilisha taratibu zote za kisheria ikiwamo kulipia kodi zote zinazotakiwa ili niweze kuendesha shughuli za kampuni kwa uhuru zaidi) lakini kabla sijaanza kazi nilipata na janga la kifamilia. matatizo ya kuuguza na misiba vikanitawala kiasi kwamba nikajikuta fedha zoote nilizokuwa nazo kwa ajili ya kuendeshea shughuli za kampuni zikapukutika, mpaka hivi ninavyoongea sina hata senti ya kunifanya niendeleze kampuni.
Je wadau mnanisaidieje kimawazo?
izingatiwe kwamba mpaka sasa vitu vinavyotakiwa ni pamoja na hela ya pango, na namna ya kupata kazi za kufanya.
pamoja na kuomba msaada wa mawazo lakini pia nakaribisha wadau ambao wanaweza kuongeza mtaaji ili tufanye kazi kwa pamoja kwa maelewano maalumu/kisheria.
hapa chini ni orodha ya shughuli ambazo kampuni imepanga kuzifanya:
v Promotion and advertisement of companies’ products
v Music promotion & entertainment
v Events management, planning and coordinating
v Brand awareness campaign
v market research and trainings
naomba kama una mawazo mengi zaidi ya haya unitumie private message tutawasiliana zaidi