Haya ndio madhara ya kujifanyia "land reclamation" kienyeji enyeji. Mtu unachukua tu likifusi unalimwaga then unajenga kwenye mkondo wa maji.....yatapita wapi?
Hata hao mabingwa wa reclamation, The Netherlands huwa hawaifukuzi bahari moja kwa moja. Wanatengeneza channels za maji kupita ili yapate njia pindi yanapohitaji kufanya hivyo. Na channels hizo hutumika kama njia za usafiri kufika katika maeneo mbalimbali mijini.
Maji huwa hayafukuzwi moja kwa moja kwenye njia yake. Ukitaka kuyafukuza kutoka eneo moja ni lazima uyatengenezee njia mbadala, la sivyo utakiona cha mtema kuni.